Zaburi 39:1-13 NEN

Zaburi 39:1-13

Zaburi 39

Maombi Ya Mtu Anayeteseka

Kwa mwimbishaji. Mtindo wa Yeduthuni. Zaburi ya Daudi.

39:1 1Fal 2:4; Kol 4:5; Ebr 2:1; Ay 1:22; 6:24; Yak 1:26; 3:2; Za 34:13; 119:9, 59; Mit 4:26, 27; 20:11Nilisema, “Nitaziangalia njia zangu

na kuuzuia ulimi wangu usije ukatenda dhambi;

nitaweka lijamu kinywani mwangu

wakati wote waovu wanapokuwa karibu nami.”

39:2 Za 6:3; 25:17; 39:9; 77:4; 31:10; Ay 31:34Lakini niliponyamaza kimya na kutulia,

hata pasipo kusema lolote jema,

uchungu wangu uliongezeka.

39:3 Yer 20:9; Lk 24:32; Za 1:2; 119:15; Yer 5:14; 20:9; 23:29Moyo wangu ulipata moto ndani yangu,

nilipotafakari, moto uliwaka,

ndipo nikasema kwa ulimi wangu:

39:4 Ay 14:5; 14:2; 7:7; Mwa 47:9“Ee Bwana, nijulishe mwisho wa maisha yangu

na hesabu ya siku zangu;

nijalie kujua jinsi maisha yangu

yanavyopita upesi.

39:5 Ay 10:20; 7:7; Za 62:9; 90:4; 89:45; 102:23Umefanya maisha yangu mafupi kama pumzi;

muda wangu wa kuishi ni kama

hauna thamani kwako.

Maisha ya kila mwanadamu

ni kama pumzi.

39:6 Ay 8:9; 27:17; Mhu 6:12; Lk 12:20; Yak 4:14; 1:11; Za 102:11; 127:2Hakika kila binadamu ni kama njozi

aendapo huku na huko:

hujishughulisha na mengi lakini ni ubatili;

anakusanya mali nyingi,

wala hajui ni nani atakayeifaidi.

39:7 Za 9:18“Lakini sasa Bwana, nitafute nini?

Tumaini langu ni kwako.

39:8 Isa 53:5, 8, 10; 43:28; Kum 28:37; Za 69:7; 51:1, 14; 32:1; 6:4; 79:4; Dan 9:16Niokoe kutoka kwenye makosa yangu yote,

usinifanye kuwa dhihaka ya wapumbavu.

39:9 Za 38:13; Isa 38:15Nilinyamaza kimya,

sikufumbua kinywa changu,

kwa sababu wewe ndiwe uliyetenda hili.

39:10 2Nya 21:14; Eze 7:9; 24:16; Kut 9:3Niondolee mjeledi wako,

nimeshindwa kwa mapigo ya mkono wako.

39:11 Kum 28:20; Isa 26:16; 51:8; 66:15; Eze 5:15; 2Pet 2:16; Za 94:10; 90:7; Ay 7:7; 13:28; Lk 12:33; Yak 5:2Unakemea na kuadhibu wanadamu

kwa ajili ya dhambi zao;

unaharibu utajiri wao kama nondo aharibuvyo:

kila mwanadamu ni kama pumzi tu.

39:12 Za 17:1; 1Nya 29:15; Ebr 11:13; Law 25:23; Kum 1:45; 2Fal 20:5; Mwa 23:4; 47:9“Ee Bwana, usikie maombi yangu,

usikie kilio changu unisaidie,

usiwe kiziwi kwa kulia kwangu.

Kwani mimi ninaishi na wewe kama mgeni,

kama walivyokuwa baba zangu wote,

39:13 Ay 10:20, 21Tazama mbali nami, ili niweze kufurahi tena

kabla sijaondoka na nisiwepo tena.”

Read More of Zaburi 39