Zaburi 32:1-11 NEN

Zaburi 32:1-11

Zaburi 32

Furaha Ya Msamaha

Zaburi ya Daudi. Funzo.

32:1 Za 85:2; 103:3; Rum 4:6Heri mtu yule ambaye amesamehewa makosa yake,

ambaye dhambi zake zimefunikwa.

32:2 Rum 4:7-8; 5:13; Yn 1:47; Ufu 14:5; 2Kor 1:12; Law 17:4Heri mtu yule ambaye Bwana

hamhesabii dhambi,

na ambaye rohoni mwake

hamna udanganyifu.

32:3 Ay 31:34; 31:10; 3:24; Za 6:6Niliponyamaza, mifupa yangu ilichakaa

kwa kulia kwa maumivu makali mchana kutwa.

32:4 1Sam 5:6; Ay 9:34; Za 38:2; 39:10; 22:15Usiku na mchana

mkono wako ulinilemea,

nguvu zangu zilinyonywa

kama vile katika joto la kiangazi.

32:5 Ay 31:33; Mit 28:13; Lk 15:18; Za 103:12; Law 26:40; Yn 1:9Kisha nilikujulisha dhambi yangu

wala sikuficha uovu wangu.

Nilisema, “Nitaungama

makosa yangu kwa Bwana.”

Ndipo uliponisamehe

hatia ya dhambi yangu.

32:6 Za 69:13; Yn 7:34; Isa 55:6; Za 69:1; 43:2; Kut 15:10; 1Tim 1:16Kwa hiyo kila mtu mcha Mungu akuombe

wakati unapopatikana,

hakika maji makuu yatakapofurika

hayatamfikia yeye.

32:7 Za 9:9; Amu 9:35; 5:1; Mit 18:10; Isa 4:6; Mt 23:37; Kol 3:3Wewe ndiwe mahali pangu pa kujificha,

utaniepusha na taabu

na kunizunguka kwa nyimbo za wokovu.

32:8 Za 25:8; 34:11; 33:18; Isa 48:17Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea;

nitakushauri na kukuangalia.

32:9 Ay 30:11; 39:10; Yak 3:3Usiwe kama farasi au nyumbu

wasio na akili,

ambao ni lazima waongozwe kwa lijamu na hatamu

la sivyo hawatakukaribia.

32:10 Rum 2:9; Za 4:5; Mit 16:20; Yer 17:7; Mit 13:21; 16:20Mtu mwovu ana taabu nyingi,

bali upendo usio na kikomo wa Bwana

unamzunguka mtu anayemtumaini.

32:11 Za 64:10Shangilieni katika Bwana na mfurahi, enyi wenye haki!

Imbeni, nyote mlio wanyofu wa moyo!

Read More of Zaburi 32