Zaburi 31:1-8 NEN

Zaburi 31:1-8

Zaburi 31

Maombi Na Sifa Kwa Kuokolewa Kutoka Kwa Adui

Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.

31:1 Za 7:1; 5:8Ee Bwana, nimekukimbilia wewe,

usiache nikaaibika kamwe,

kwa haki yako uniokoe.

31:2 Za 6:4Nitegee sikio lako,

uje uniokoe haraka;

uwe kwangu mwamba wa kimbilio,

ngome imara ya kuniokoa.

31:3 Za 18:2; 23:3; Yer 14:7Kwa kuwa wewe ni mwamba wangu na ngome yangu,

uniongoze na kunilinda kwa ajili ya jina lako.

31:4 1Sam 28:9; Ay 18:10; Za 9:9Uniepushe na mtego niliotegewa,

maana wewe ndiwe kimbilio langu.

31:5 Lk 23:46; Ebr 6:18; Mdo 7:59; Isa 45:19; 65:16; 2Tim 1:12Ninaikabidhi roho yangu mikononi mwako,

unikomboe Ee Bwana, uliye Mungu wa kweli.

31:6 Kum 32:21; Za 4:5Ninawachukia wale wanaongʼangʼania sanamu batili;

mimi ninamtumaini Bwana.

31:7 Yn 10:27; Lk 22:44; Za 25:17Nitafurahia na kushangilia upendo wako,

kwa kuwa uliona mateso yangu

na ulijua maumivu ya nafsi yangu.

31:8 Za 18:19; Kum 32:30; 2Sam 22:20Hukunikabidhi kwa adui yangu

bali umeiweka miguu yangu mahali penye nafasi.

Read More of Zaburi 31