Zaburi 17:6-12 NEN

Zaburi 17:6-12

17:6 Za 84:7; 116:2; 4:1Ee Mungu, ninakuita, kwa kuwa utanijibu,

nitegee sikio lako na usikie ombi langu.

17:7 Za 31:21; 69:13; 106:45; 107:43; 117:2; 10:12; 2:12Uonyeshe ajabu ya upendo wako mkuu,

wewe uokoaye kwa mkono wako wa kuume

wale wanaokukimbilia kutokana na adui zao.

17:8 Hes 6:24; Isa 34:15; Kum 32:10; Mit 7:2; Za 27:5; 31:20; 32:7; 36:7; 63:7; Rum 2:12Nilinde kama mboni ya jicho lako,

unifiche chini ya kivuli cha mbawa zako

17:9 Za 109:3kutokana na waovu wanaonishambulia,

kutokana na adui wauaji wanaonizunguka.

17:10 Za 73:7; 119:70; Isa 6:10; 2:3Huifunga mioyo yao iliyo migumu,

vinywa vyao hunena kwa majivuno.

17:11 Za 88:17; 1Sam 23:26Wamenifuatia nyayo zangu, sasa wamenizingira,

wakiwa macho, waniangushe chini.

17:12 Za 7:2; Yer 5:6; 12:8; Mao 3:10; Mwa 49:9Wamefanana na simba mwenye njaa awindaye,

kama simba mkubwa anyemeleaye mafichoni.

Read More of Zaburi 17