Zaburi 148:1-6 NEN

Zaburi 148:1-6

Zaburi 148

Mwito Kwa Ulimwengu Kumsifu Mungu

148:1 Za 33:2; 103; 1; 19:1; 69:34; 150:1Msifuni Bwana.

Msifuni Bwana kutoka mbinguni,

msifuni juu vileleni.

148:2 Za 103:20; 1Fal 22:19; Dan 7:10; Ebr 1:7Msifuni, enyi malaika wake wote,

msifuni yeye, enyi jeshi lake lote la mbinguni.

148:3 Za 19:1Msifuni yeye, enyi jua na mwezi,

msifuni yeye, enyi nyota zote zingʼaazo.

148:4 Kum 10:14; Mwa 1:7; 1Fal 8:27Msifuni yeye, enyi mbingu zilizo juu sana,

na ninyi maji juu ya anga.

148:5 Za 145:21; 147:15; Ebr 11:3Vilisifu jina la Bwana

kwa maana aliamuru navyo vikaumbwa.

148:6 Yer 31:35-36; 33:25; 33:25Aliviweka mahali pake milele na milele,

alitoa amri ambayo haibadiliki milele.

Read More of Zaburi 148