Zaburi 119:137-144 NEN

Zaburi 119:137-144

Haki Ya Sheria Ya Bwana

119:137 Kut 9:27; Ezr 9:15; Neh 9:13, 33; Yer 12:1; Dan 9:7Ee Bwana, wewe ni mwenye haki,

sheria zako ni sahihi.

119:138 Za 119:75, 86; 19:7Sheria ulizoziweka ni za haki,

ni za kuaminika kikamilifu.

119:139 Za 69:9; Yn 2:17Jitihada yangu imenidhoofisha, kwa kuwa adui zangu

wanayapuuza maneno yako.

119:140 Yos 23:14; Za 12:6; 119:47Ahadi zako zimejaribiwa kikamilifu,

mtumishi wako anazipenda.

119:141 Za 22:6; 119:61, 134; Mit 15:16; Amo 7:2; Lk 6:20; 2Kor 8:9; Yak 2:5Ingawa ni mdogo na ninadharauliwa,

sisahau mausia yako.

119:142 Za 119:151, 160; 19:7, 9; Yn 17:17; Efe 1:3Haki yako ni ya milele,

na sheria yako ni kweli.

119:143 Za 119:24, 47Shida na dhiki zimenipata,

lakini amri zako ni furaha yangu.

119:144 Za 119:34Sheria zako ni sahihi milele,

hunipa ufahamu ili nipate kuishi.

Read More of Zaburi 119