Zaburi 119:105-112 NEN

Zaburi 119:105-112

Nuru Kutoka Kwenye Sheria Ya Bwana

119:105 Mit 6:23; 20:27; 2Pet 1:19; Za 119:130Neno lako ni taa ya miguu yangu

na mwanga katika njia yangu.

119:106 Neh 10:29; Za 119:7Nimeapa na nimethibitisha,

kwamba nitafuata sheria zako za haki.

119:107 Za 119:25Nimeteseka sana, uhifadhi maisha yangu, Ee Bwana,

sawasawa na neno lako.

119:108 Za 51:15; 109:30; 63:5; 119:64; 71:8; Ebr 13:15; Hos 14:2Ee Bwana, pokea sifa za hiari za kinywa changu,

nifundishe sheria zako.

119:109 Amu 12:3; Za 119:61; Ay 13:14Ingawa maisha yangu yako hatarini siku zote,

sitasahau sheria yako.

119:110 Za 25:15; 64:5; 119:10; Isa 8:14; Amo 3:5Waovu wamenitegea mtego,

lakini sijayakiuka maagizo yako.

119:111 Kum 33:4; Za 119:14, 162Sheria zako ni urithi wangu milele,

naam ni furaha ya moyo wangu.

119:112 Za 108:1; 119:33Nimekusudia moyoni mwangu

kuyafuata maagizo yako mpaka mwisho.

Read More of Zaburi 119