Zaburi 107:23-32 NEN

Zaburi 107:23-32

107:23 Isa 42:10; Za 104:26Wengine walisafiri baharini kwa meli,

walikuwa wafanyabiashara kwenye maji makuu.

107:24 Za 64:9; 111:2; 143:5Waliziona kazi za Bwana,

matendo yake ya ajabu kilindini.

107:25 Za 105:31; 50:3; 93:3Kwa maana alisema na kuamsha tufani

iliyoinua mawimbi juu.

107:26 Za 22:14; Isa 13:7; Nah 2:10; Lk 8:23; Yos 2:11Yakainuka juu mbinguni, yakashuka chini hadi vilindini,

katika hatari hii ujasiri wao uliyeyuka.

107:27 Isa 19:14; 24:20; 28:7Walipepesuka na kuyumbayumba kama walevi,

ujanja wao ukafikia ukomo.

107:28 Za 107:19; 4:1; Yon 1:6Ndipo walipomlilia Bwana katika shida yao,

naye akawatoa kwenye taabu yao.

107:29 Lk 8:24; Za 93:3; 65:7; Mk 4:39-41; Yon 1:15; Isa 50:2; Mt 8:26Akatuliza dhoruba kwa mnongʼono,

mawimbi ya bahari yakatulia.

107:30 Za 107:7Walifurahi ilipokuwa shwari,

naye akawaongoza hadi bandari waliyoitamani.

107:31 Za 107:15; 6:4; 75:1; 106:2Basi na wamshukuru Bwana kwa upendo wake usiokoma,

na kwa matendo yake ya ajabu kwa wanadamu.

107:32 Za 30:1; 34:3; 99:5; 1:5; 22:22; 26:12; 35:18Na wamtukuze yeye katika kusanyiko la watu,

na wamsifu katika baraza la wazee.

Read More of Zaburi 107