Zaburi 106:16-31 NEN

Zaburi 106:16-31

106:16 Hes 16:1-3Kambini walimwonea wivu Mose,

na pia Aroni aliyekuwa amewekwa wakfu kwa Bwana.

106:17 Kum 11:6; 15:12; Hes 16:1Ardhi ilifunguka ikawameza Dathani,

ikawazika Abiramu na kundi lake.

106:18 Law 10:2Moto uliwaka katikati ya wafuasi wao,

mwali wa moto uliwateketeza waovu.

106:19 Kut 32:4; Mdo 7:41Huko Horebu walitengeneza ndama,

na kuabudu sanamu ya kusubu kwa chuma.

106:20 Yer 2:11; Rum 1:23Waliubadilisha Utukufu wao

kwa sanamu ya fahali, ambaye hula majani.

106:21 Za 78:11; 75:1; Kum 10:21Walimsahau Mungu aliyewaokoa,

aliyekuwa ametenda mambo makuu huko Misri,

106:22 Za 78:51; Kut 3:20; Kum 4:34miujiza katika nchi ya Hamu

na mambo ya kutisha huko Bahari ya Shamu.

106:23 Kut 32:10-14; Hes 11:2; Eze 13:5; 20:13; Kum 9:19Kwa hiyo alisema kwamba angewaangamiza:

kama Mose mteule wake,

asingesimama kati yao na Mungu

kuizuia ghadhabu yake kuwaangamiza.

106:24 Ebr 3:18; Yer 3:19; Hes 14:11, 30, 31; Kum 8:7Kisha waliidharau ile nchi nzuri,

hawakuiamini ahadi yake.

106:25 Kut 15:24; Kum 1:27; 1Kor 10:10Walinungʼunika ndani ya mahema yao,

wala hawakumtii Bwana.

106:26 Hes 14:23; Ebr 4:3; 3:17; Kum 2:14Kwa hiyo akaapa kwa mkono ulioinuliwa

kwamba atawafanya waanguke jangwani,

106:27 Law 26:33kuwatawanya wazao wao waanguke miongoni mwa mataifa,

na kuwatawanya katika nchi zote.

106:28 Hes 23:28; 25:2, 3; Kum 4:3; Hos 9:10; Ufu 2:14Walijifunga nira na Baali wa Peori,

wakala dhabihu zilizotolewa kwa miungu isiyo na uhai.

106:29 Za 64:2; 141:4; Hes 16:46; 25:3, 8Waliichochea hasira ya Bwana,

wakamkasirisha kwa matendo yao maovu,

nayo tauni ikazuka katikati yao.

106:30 Kut 6:25; Hes 25:8Lakini Finehasi alisimama na kuingilia kati,

nayo tauni ikazuiliwa.

106:31 Mwa 15:6; Za 49:11; Hes 15:11-13Hili likahesabiwa kwake haki,

kwa vizazi visivyo na mwisho vijavyo.

Read More of Zaburi 106