Zaburi 106:1-15 NEN

Zaburi 106:1-15

Zaburi 106

Wema Wa Bwana Kwa Watu Wake

106:1 Ezr 3:11; Za 63:7; 22:23; 103:2; 119:68; 136:1-26; Yer 33:11; Mt 19:17Msifuni Bwana.

Mshukuruni Bwana, kwa kuwa ni mwema;

upendo wake wadumu milele.

106:2 Za 40:5; 71:16Ni nani awezaye kusimulia matendo makuu ya Bwana

au kutangaza kikamilifu sifa zake?

106:3 Yer 22:15, 16; Mt 22:37; Za 15:2; 112:5; Hos 12:6Heri wale wanaodumisha haki,

ambao daima wanafanya yaliyo mema.

106:4 Za 25:6-7; 77:7; Mwa 50:24Ee Bwana, unikumbuke unapowatendea mema watu wako,

uwe msaada wangu unapowaokoa,

106:5 Kum 30:15; Za 1:3; 105:6; 20:5; 27:5; 47:5; 118:15; Kut 34:9ili niweze kufurahia mafanikio ya wateule wako,

niweze kushiriki katika furaha ya taifa lako,

na kuungana na urithi wako katika kukusifu.

106:6 1Fal 8:47; Neh 1:7; Dan 9:5; Rum 3:9; 2Nya 30:7; Law 26:40Tumetenda dhambi, kama vile baba zetu walivyotenda,

tumekosa na tumetenda uovu.

106:7 Amu 3:7; Za 78:42; Kut 14:11, 12Wakati baba zetu walipokuwa Misri,

hawakuzingatia maajabu yako,

wala hawakukumbuka wingi wa fadhili zako,

bali waliasi kando ya bahari, Bahari ya Shamu.

106:8 Kut 9:16; 14:30-31; Za 80:3; 107:13; 23:3; 143:11; Isa 25:9; Yoe 2:32; Yos 7:9; Yer 14:7, 21Hata hivyo aliwaokoa kwa ajili ya jina lake,

ili apate kudhihirisha uweza wake mkuu.

106:9 Nah 1:4; Isa 50:3; 63:11-14; Kut 14:21; Za 18:15; 78:13Alikemea Bahari ya Shamu, nayo ikakauka,

akawaongoza katika vilindi vyake kama vile jangwani.

106:10 Kut 14:30; Za 107:13; 78:42, 53; Isa 35:9; 62:12Aliwaokoa mikononi mwa adui;

kutoka mikononi mwa adui aliwakomboa.

106:11 Kut 14:28Maji yaliwafunika adui zao,

hakunusurika hata mmoja.

106:12 Kut 15:1-21; Za 105:43Ndipo walipoamini ahadi zake,

nao wakaimba sifa zake.

106:13 Kut 15:24; 16:28; Hes 27:21Lakini mara walisahau aliyowatendea,

wala hawakungojea shauri lake.

106:14 1Kor 10:9; Kut 17:2; Za 78:40; 68:7Jangwani walitawaliwa na tamaa zao,

walimjaribu Mungu nyikani.

106:15 Isa 10:16; Hes 11:33; Kut 16:13; Za 78:29Kwa hiyo aliwapa kile walichoomba,

lakini akatuma juu yao ugonjwa wa kudhoofisha.

Read More of Zaburi 106