Mithali 8:12-21 NEN

Mithali 8:12-21

8:12 Mit 1:4“Mimi hekima, nakaa pamoja na busara;

ninamiliki maarifa na busara.

8:13 Kut 20:20; Yer 44:4; Zek 8:17; Mit 16:6Kumcha Bwana ni kuchukia uovu;

ninachukia kiburi na majivuno,

tabia mbaya na mazungumzo potovu.

8:14 Mhu 7:19; Ay 9:4Ushauri na hukumu sahihi ni vyangu;

nina ufahamu na nina nguvu.

8:15 Dan 2:21; Mt 28:18; Rum 13:1Kwa msaada wangu wafalme hutawala

na watawala hutunga sheria zilizo za haki,

8:16 2Nya 1:10; Mit 29:4kwa msaada wangu wakuu hutawala,

na wenye vyeo wote watawalao dunia.

8:17 Za 91:14; Yn 14:21-24; 1Sam 2:30; Yak 1:5Nawapenda wale wanipendao,

na wale wanitafutao kwa bidii wataniona.

8:18 Mt 6:33; 1Fal 3:13; Kum 8:18; Mit 3:16Utajiri na heshima viko kwangu,

utajiri udumuo na mafanikio.

8:19 Mit 3:13-14; 10:20Tunda langu ni bora kuliko dhahabu safi;

kile nitoacho hupita fedha iliyo bora.

Natembea katika njia ya unyofu

katika mapito ya haki,

8:21 Mit 15:6; 24:4nawapa utajiri wale wanipendao

na kuzijaza hazina zao.

Read More of Mithali 8