Mithali 4:10-19 NEN

Mithali 4:10-19

4:10 Kum 11:21; Mit 3:2Sikiliza mwanangu, kubali ninachokuambia,

nayo miaka ya maisha yako itakuwa mingi.

4:11 1Sam 12:23; 2Sam 22:37; Za 5:8Ninakuongoza katika njia ya hekima

na kukuongoza katika mapito yaliyonyooka.

4:12 Ay 18:7; Yer 13:16; Za 18:36Utembeapo, hatua zako hazitazuiliwa;

ukimbiapo, hutajikwaa.

4:13 Mit 3:22Mkamate sana elimu, usimwache aende zake;

mshike, maana yeye ni uzima wako.

4:14 Za 1:1; Mit 1:15Usiuweke mguu wako katika njia ya waovu

wala usitembee katika njia ya watu wabaya.

Epukana nayo, usisafiri katika njia hiyo;

achana nayo, na uelekee njia yako.

4:16 Za 36:4; Mik 7:3Kwa kuwa hawawezi kulala mpaka watende uovu;

wanashindwa hata kusinzia mpaka wamwangushe mtu.

4:17 Mwa 49:5; Za 73:6; Mit 1:10-19; Isa 59:6; Yer 22:3; Hab 1:2; Mal 2:16Wanakula mkate wa uovu,

na kunywa mvinyo wa jeuri.

4:18 Mt 5:14; Ay 17:9; Isa 26:7; Dan 12:3; Yn 8:12Njia ya wenye haki ni kama nuru ya kwanza ya mapambazuko,

ambayo hungʼaa zaidi na zaidi mpaka mchana mkamilifu.

4:19 Ay 18:5; Yn 12:35Lakini njia ya waovu ni kama giza nene;

hawajui kinachowafanya wajikwae.

Read More of Mithali 4