Mithali 31:1-9 NEN

Mithali 31:1-9

Misemo Ya Mfalme Lemueli

31:1 Mit 22:17Misemo ya Mfalme Lemueli, usia wa mama yake aliyomfundisha:

31:2 Amu 11:30; Isa 49:15“Ee mwanangu, ee mwana wa tumbo langu,

ee mwana wa nadhiri zangu,31:2 Au: Ewe uliye jibu la maombi yangu.

31:3 Neh 13:26; Kum 17:17; Hos 4:11; 1Fal 11:3Usitumie nguvu zako kwa wanawake,

uhodari wako kwa wale wanaowaharibu wafalme.

31:4 Mhu 10:17; Isa 5:22“Ee Lemueli, haifai wafalme,

haifai wafalme kunywa mvinyo,

haifai watawala kutamani sana kileo,

31:5 1Fal 16:9; Mit 16:12; Hos 4:11wasije wakanywa na kusahau vile sheria inavyoamuru

na kuwanyima haki zao wote walioonewa.

31:6 Mwa 14:18Wape kileo wale wanaoangamia,

mvinyo wale walio na uchungu,

31:7 Es 1:10Wanywe na kusahau umaskini wao

na wasikumbuke taabu yao tena.

31:8 1Sam 19:4; Es 4:16; Ay 29:12-17“Sema kwa ajili ya wale wasioweza kujisemea,

kwa ajili ya haki za wote walioachwa ukiwa.

31:9 Law 19:15; Yer 22:16; Kum 1:16; Isa 1:17Sema na uamue kwa haki,

tetea haki za maskini na wahitaji.”

Read More of Mithali 31