Mithali 29:10-18 NEN

Mithali 29:10-18

29:10 Mwa 4:5-8; 1Yn 3:12Watu wamwagao damu humchukia mtu mwadilifu

na hutafuta kumuua mtu mnyofu.

29:11 Ay 15:13; Mit 12:16Mpumbavu huonyesha hasira yake yote,

bali mwenye hekima hujizuia.

29:12 2Fal 21:9; Ay 34:30Kama mtawala akisikiliza uongo,

maafisa wake wote huwa waovu.

29:13 Mit 22:2; Mt 5:45Mtu maskini na mtu anayeonea wanafanana kwa jambo hili:

Bwana hutia nuru macho yao wote wawili.

29:14 Mit 29:4; Za 72:1-5; Mit 16:12Kama mfalme akiwaamua maskini kwa haki,

kiti chake cha enzi kitakuwa thabiti siku zote.

29:15 Mit 29:17; 13:24Fimbo ya maonyo hutia hekima,

bali mtoto aliyeachiwa bila maonyo

humwaibisha mama yake.

29:16 Za 37:36; 58:10; 91:8Wakati waovu wanapostawi,

pia dhambi vivyo hivyo,

lakini wenye haki wataliona anguko lao.

29:17 Mit 13:24; 29:15Mrudi mwanao, naye atakupa amani,

atakufurahisha nafsi yako.

29:18 Za 19:11; Yn 13:17; Amo 8:11-12; 1Sam 3:1Mahali pasipo na ufunuo, watu kujizuia,

bali ana heri mtu yule aishikaye sheria.

Read More of Mithali 29