Mithali 25:11-20
25:11 Mit 15:23; Isa 50:4Neno lisemwalo kwa wakati ufaao
ni kama matunda ya mtofaa ya dhahabu
yaliyowekwa kwenye vijalizo vya fedha.
25:12 Za 141:5; Mit 15:31Kama vile kipuli cha dhahabu
au pambo la dhahabu safi,
ndivyo lilivyo karipio la mtu mwenye hekima
kwa sikio lisikilizalo.
25:13 Mit 13:17; 10:26Kama vile ubaridi wa theluji wakati wa mavuno
ndivyo alivyo mjumbe mwaminifu kwa wale wamtumao,
huburudisha roho za bwana zake.
25:14 Mit 20:6; Yud 12Kama vile mawingu na upepo pasipo mvua
ndivyo alivyo mtu ajisifuye kwa zawadi ambazo hatoi.
25:15 Mhu 10:4; Mit 15:1; Mwa 32:4; 1Sam 25:24Kwa njia ya uvumilivu mtawala aweza kushawishiwa,
nao ulimi laini waweza kuvunja mfupa.
25:16 Mit 25:27Ukipata asali, kula kiasi tu cha kukutosha,
ukila zaidi, utatapika.
Ingiza mguu wako nyumbani kwa jirani yako mara chache,
ukizidisha, atakukinai na atakuchukia.
25:18 Za 57:4; Mit 12:18Kama vile rungu au upanga au mshale mkali
ndivyo alivyo mtu atoaye ushuhuda wa uongo dhidi ya jirani yake.
25:19 Ay 6:14-20; 2Tim 4:16Kama vile jino bovu au mguu uliolemaa,
ndivyo ilivyo kumtegemea mtu asiye mwaminifu wakati wa shida.
25:20 Dan 6:18; Rum 12:15Kama vile avuaye mavazi siku ya baridi,
au kama siki iliyomwagwa juu ya magadi,
ndivyo alivyo yeye amuimbiaye nyimbo mtu mwenye moyo mzito.