Mithali 22:7-16 NEN

Mithali 22:7-16

22:7 Yak 2:6Matajiri huwatawala maskini

naye akopaye ni mtumwa wa akopeshaye.

22:8 Hos 10:13; 8:7; Kut 1:20; Gal 6:7-8; Za 125:3Yeye aupandaye uovu huvuna taabu,

nayo fimbo ya ghadhabu yake itaangamizwa.

22:9 Kum 14:29; 2Kor 9:6; Mit 11:25; 28:27Mtu mkarimu yeye mwenyewe atabarikiwa

kwa kuwa hushiriki chakula chake na maskini.

22:10 Mit 26:20; Mwa 21:9, 10; Za 101:5Mfukuze mwenye dhihaka,

na mvutano utatoweka;

ugomvi na matukano vitakoma.

22:11 Mit 16:13; Mt 5:8Yeye apendaye moyo safi na yeye ambaye maneno yake ni ya neema,

mfalme atakuwa rafiki yake.

Macho ya Bwana hulinda maarifa,

bali huyapinga maneno ya asiye mwaminifu.

22:13 Mit 26:13Mvivu husema, “Yuko simba nje!”

au, “Nitauawa katika mitaa!”

22:14 Mit 6:12; Mhu 7:26Kinywa cha mwanamke kahaba ni shimo refu;

yeye aliye chini ya ghadhabu ya Bwana

atatumbukia ndani yake.

22:15 Mit 13:24; 20:30Upumbavu umefungwa ndani ya moyo wa mtoto,

bali fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali naye.

22:16 Ay 20:19-23; Amo 2:6-8; Isa 3:14-15; Yak 2:13Yeye amwoneaye maskini ili kujiongezea mali,

naye ampaye tajiri zawadi, wote huwa maskini.

Read More of Mithali 22