Mithali 17:15-24
17:15 Za 94:21; Kut 23:6-7; Mit 18:5; Mao 3:34-36; Isa 5:23Yeye asemaye kuwa asiye na haki ana haki,
naye asemaye kuwa mwenye haki hana haki:
Bwana huwachukia sana wote wawili.
17:16 Mit 23:23Fedha ina faida gani mikononi mwa mpumbavu,
wakati yeye hana haja ya kupata hekima?
17:17 2Sam 15:21; Mit 27:10Rafiki hupenda wakati wote
naye ndugu amezaliwa kwa ajili ya wakati wa shida.
17:18 Mit 6:1-5; 11:5Mtu mjinga hupana mkono ili kuweka rehani,
naye huweka dhamana kwa jirani yake.
Yeye apendaye ugomvi apenda dhambi;
naye ainuaye sana lango lake17:19 Kuinua lango maana yake ni kusema kwa majivuno. hutafuta uharibifu.
Mtu mwenye moyo mpotovu hawezi kufanikiwa;
naye ambaye ulimi wake ni mdanganyifu huanguka kwenye taabu.
17:21 Mit 10:1Kuwa na mwana mpumbavu huleta huzuni;
hakuna furaha kwa baba wa mpumbavu.
17:22 Kut 12:46; Za 22:15Moyo wenye furaha ni dawa nzuri,
bali roho iliyopondeka hukausha mifupa.
17:23 Kut 18:21; 1Sam 8:3Mtu mwovu hukubali rushwa kwa siri
ili kupotosha njia ya haki.
17:24 Ay 31:1; Mhu 2:14Mtu wa ufahamu huitazama hekima,
lakini macho ya mpumbavu huhangaika
hadi kwenye miisho ya dunia.