Mithali 12:28, Mithali 13:1-9 NEN

Mithali 12:28

12:28 Kum 30:15; Rum 5:21; Mit 10:2Katika njia ya haki kuna uzima;

katika mapito hayo kuna maisha ya milele.

Read More of Mithali 12

Mithali 13:1-9

Mema Ya Muda Mfupi Na Yale Ya Kudumu

13:1 1Sam 2:25; Mit 10:1; 12:1; 15:5Mwana mwenye hekima husikia mafundisho ya babaye,

bali mwenye dharau hasikilizi maonyo.

13:2 Mit 12:14Kutoka tunda la midomo yake mtu hufurahia mambo mema,

bali wasio waaminifu wanatamani sana jeuri.

13:3 Za 12:2; Yak 3:2; Mit 10:6; Ay 1:22Yeye alindaye midomo yake hulinda nafsi yake,

bali yeye asemaye kwa haraka ataangamia.

13:4 Mit 21:25-26Mvivu hutamani sana na hapati kitu,

bali nafsi ya mwenye bidii

hutoshelezwa kikamilifu.

13:5 Kol 3:9; Rum 12:9Mwenye haki huchukia uongo,

bali waovu huleta aibu na fedheha.

13:6 Mit 11:3-5; Yer 44:5Haki humlinda mtu mwadilifu,

bali uovu humwangusha mwenye dhambi.

13:7 2Kor 6:10Mtu mmoja hujifanya tajiri, kumbe hana chochote;

mwingine hujifanya maskini, kumbe ana utajiri mwingi.

13:8 Mit 15:16Utajiri wa mtu waweza kukomboa maisha yake,

bali mtu maskini hasikii kitisho.

13:9 Ay 18:5; Mit 4:18-19Nuru ya mwenye haki hungʼaa sana,

bali taa ya mwovu itazimwa.

Read More of Mithali 13