Mithali 11:19-28 NEN

Mithali 11:19-28

11:19 Kum 30:15; Mit 10:2; 1Sam 2:6; Za 89:48; Mit 1:18-19; Mhu 7:2; Yer 43:1Mtu mwenye haki kweli kweli hupata uzima,

bali yeye afuatiliaye ubaya huendea kifo chake.

11:20 1Nya 29:17; Za 52:7Bwana huwachukia sana watu wenye moyo wa upotovu,

bali hupendezwa na wale ambao njia zao hazina lawama.

11:21 Mit 16:5; Za 112:2Uwe na hakika na hili: Waovu hawataepuka kuadhibiwa,

bali wenye haki watakuwa huru.

Kama pete ya dhahabu katika pua ya nguruwe

ndivyo alivyo mwanamke mzuri ambaye hana busara.

11:23 Rum 2:8, 9Shauku ya mwenye haki huishia tu kwenye mema,

bali tumaini la mwovu huishia tu kwenye ghadhabu.

11:24 Za 112:9Kuna mtu atoaye kwa ukarimu, hata hivyo hupata zaidi,

mwingine huzuia, lakini huwa maskini.

11:25 Mit 22:9; 2Kor 9:6-9; Mt 5:7Mtu mkarimu atastawi;

yeye awaburudishaye wengine

ataburudishwa mwenyewe.

11:26 Amo 8:5; Ay 29:13Watu humlaani mtu awanyimae watu nafaka,

bali baraka itamkalia kichwani kama taji

yeye aliye radhi kuiuza.

11:27 Es 7:10; Za 7:15-16Yeye atafutaye mema hupata ukarimu,

bali ubaya huja kwake yeye autafutaye.

11:28 Yer 9:23; 17:8; Mk 10:25; Za 52:8Yeyote ategemeaye utajiri wake ataanguka,

bali mwenye haki atastawi kama jani bichi.

Read More of Mithali 11