Mithali 1:1-7 NEN

Mithali 1:1-7

Utangulizi: Kusudi Na Kiini

1:1 1Fal 4:29-34Mithali za Solomoni mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli:

Kwa kupata hekima na nidhamu;

kwa kufahamu maneno ya busara;

1:3 Mit 2:1; 2:1, 9kwa kujipatia nidhamu na busara,

kufanya lililo sawa, haki na bila kupendelea;

1:4 Mit 8:5, 12; 2:10-11huwapa busara wajinga,

maarifa na akili kwa vijana;

1:5 Mit 9:9wenye hekima na wasikilize nao waongeze elimu yao,

wenye kupambanua na wapate mwongozo;

1:6 Za 78:2; Mt 13:10-17; Hes 12:8; Amu 14:12kwa kufahamu mithali na mifano,

misemo na vitendawili vya wenye hekima.

1:7 Kut 20:20; Ay 28:28Kumcha Bwana ndicho chanzo cha maarifa,

lakini wapumbavu hudharau hekima na adabu.

Read More of Mithali 1