Mathayo 19:16-30 NEN

Mathayo 19:16-30

Kijana Tajiri

(Marko 10:17-31; Luka 18:18-30)

19:16 Mt 25:46; Lk 10:25Mtu mmoja akamjia Yesu na kumuuliza, “Mwalimu mwema, nifanye jambo gani jema ili nipate uzima wa milele?”

19:17 Law 18:5Yesu akamjibu, “Mbona unaniuliza habari ya mema? Aliye mwema ni Mmoja tu. Lakini ukitaka kuingia uzimani, zitii amri.”

19:18 Yak 2:11Yule mtu akamuuliza, “Amri zipi?”

Yesu akamjibu, “Usiue, usizini, usiibe, usishuhudie uongo, 19:19 Kut 20:12-16; Kum 5:16-20; Law 19:18; Mt 5:43waheshimu baba yako na mama yako, na umpende jirani yako kama nafsi yako.”

Yule kijana akasema, “Hizi zote nimezishika. Je, bado nimepungukiwa na nini?”

19:21 Mt 5:48; Lk 12:33; Mdo 4:34-35; Mt 6:20Yesu akamwambia, “Kama ukitaka kuwa mkamilifu, nenda, ukauze vitu vyote ulivyo navyo, na hizo fedha uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni. Kisha njoo, unifuate.”

19:22 Za 62:10Yule kijana aliposikia hayo, akaenda zake kwa huzuni, kwa sababu alikuwa na mali nyingi.

Hatari Za Utajiri

19:23 Mt 13:22; 1Tim 6:9-10Ndipo Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Amin, nawaambia, itakuwa vigumu kwa mtu tajiri kuingia katika Ufalme wa Mbinguni. Tena nawaambia, ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita kwenye tundu la sindano kuliko mtu tajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu.”

Wanafunzi wake waliposikia haya, walishangaa sana na kuuliza, “Ni nani basi awezaye kuokoka?”

19:26 Zek 8:6; Rum 4:21; Lk 18:28; Kum 33:9; Mt 4:20; Lk 5:11Lakini Yesu akawatazama, akawaambia, “Kwa mwanadamu jambo hili haliwezekani, lakini mambo yote yanawezekana kwa Mungu.”

19:27 Mt 4:19Ndipo Petro akamjibu, “Tazama, sisi tumeacha kila kitu na kukufuata! Tutapata nini basi?”

19:28 Mt 20:21; 25:31; Lk 22:28-30; Ufu 3:21; Lk 22:28, 29, 30; 1Kor 6:2, 3; Ufu 2:26Yesu akawaambia, “Amin, nawaambia, wakati wa kufanywa upya vitu vyote, Mwana wa Adamu atakapoketi kwenye kiti chake kitukufu cha enzi, ninyi mlionifuata pia mtaketi katika viti vya enzi kumi na viwili, mkiyahukumu makabila kumi na mawili ya Israeli. 19:29 Mt 6:33; 25:46; Mk 10:29, 30; Lk 18:29, 30Kila mtu aliyeacha nyumba, au ndugu zake wa kiume au wa kike, baba au mama, watoto au mashamba kwa ajili yangu, atapokea mara mia zaidi ya hayo, na ataurithi uzima wa milele. 19:30 Mk 10:33; Lk 10:30Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho, na walio wa mwisho watakuwa wa kwanza.

Read More of Mathayo 19