Mathayo 14:22-36, Mathayo 15:1-9 NEN

Mathayo 14:22-36

Yesu Atembea Juu Ya Maji

(Marko 6:45-52; Yohana 6:15-21)

14:22 Mk 6:45-46Mara Yesu akawaambia wanafunzi wake waingie kwenye mashua watangulie kwenda ngʼambo ya bahari, wakati yeye alikuwa akiwaaga wale makutano. 14:23 Lk 3:21; 6:12; 9:18Baada ya kuwaaga, akaenda zake mlimani peke yake kuomba. Jioni ilipofika, Yesu alikuwa huko peke yake. Wakati huo ile mashua ilikuwa mbali kutoka nchi kavu ikisukwasukwa na mawimbi, kwa sababu upepo ulikuwa wa mbisho.

Wakati wa zamu ya nne ya usiku,14:25 Zamu ya nne ya usiku ni kati ya saa tisa na saa kumi na mbili asubuhi. Yesu akawaendea wanafunzi wake akiwa anatembea juu ya maji. 14:26 Lk 24:37; Ay 9:8Wanafunzi wake walipomwona akitembea juu ya maji, waliingiwa na hofu kuu, wakasema, “Ni mzimu.” Wakapiga yowe kwa kuogopa.

14:27 Mt 9:2; Mdo 23:11; Dan 10:12; Mdo 18:9Lakini mara Yesu akasema nao, akawaambia, “Jipeni moyo! Ni mimi. Msiogope.”

Petro akamjibu, “Bwana, ikiwa ni wewe, niambie nije kwako nikitembea juu ya maji.”

Yesu akamwambia, “Njoo.”

Basi Petro akatoka kwenye chombo, akatembea juu ya maji kumwelekea Yesu. Lakini alipoona upepo mkali aliingiwa na hofu, naye akaanza kuzama, huku akipiga kelele, “Bwana, niokoe!”

14:31 Mt 6:30Mara Yesu akaunyoosha mkono wake na kumshika, akamwambia, “Wewe mwenye imani haba, kwa nini uliona shaka?”

Nao walipoingia ndani ya mashua, upepo ukakoma. 14:33 Za 2:7; Mt 4:3Ndipo wote waliokuwa ndani ya ile mashua wakamwabudu Yesu, wakisema, “Hakika, wewe ndiwe Mwana wa Mungu.”

Yesu Awaponya Wagonjwa Genesareti

(Marko 6:53-56)

Walipokwisha kuvuka, wakafika nchi ya Genesareti. Watu wa eneo lile walipomtambua Yesu, walipeleka habari sehemu zote za jirani. Watu wakamletea wagonjwa wao wote, 14:36 Mt 9:20-21wakamsihi awaruhusu wagonjwa waguse tu pindo la vazi lake, nao wote waliomgusa, wakaponywa.

Read More of Mathayo 14

Mathayo 15:1-9

Mapokeo Ya Wazee

(Marko 7:1-13)

15:1 Mk 7:1-23Ndipo baadhi ya Mafarisayo na walimu wa sheria wakamjia Yesu kutoka Yerusalemu na kumuuliza, 15:2 Kum 4:2; Lk 11:38; Kum 4:2; Lk 11:38“Mbona wanafunzi wako wanakiuka mapokeo ya wazee? Kwa maana wao hawanawi mikono yao kabla ya kula!”

Yesu akawajibu, “Mbona ninyi mnavunja amri ya Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu? 15:4 Kut 20:12; Efe 6:2; Kut 21:17; Law 9:20; Kut 20:12; Efe 6:2; Kut 21:17; Law 9:20Kwa maana Mungu alisema, ‘Waheshimu baba yako na mama yako,’ na, ‘Yeyote amtukanaye baba yake au mama yake, na auawe.’ 15:5 Mk 7:11, 12Lakini ninyi mwafundisha kwamba mtu akimwambia baba yake au mama yake, ‘Kile ambacho ningeweza kukusaidia kimewekwa wakfu kwa Mungu,’ basi hana tena sababu ya kumheshimu baba yake nacho. Basi kwa ajili ya mafundisho yenu mnavunja amri ya Mungu. 15:7 Isa 29:13Ninyi wanafiki! Isaya alikuwa sawa alipotabiri juu yenu kwamba:

15:8 Isa 29:11; Eze 33:31“ ‘Watu hawa huniheshimu kwa midomo yao,

lakini mioyo yao iko mbali nami.

15:9 Kol 2:20-22; Isa 29:13; Mal 2:2Huniabudu bure;

nayo mafundisho yao

ni maagizo ya wanadamu tu.’ ”

Read More of Mathayo 15