Mathayo 10:1-31 NEN

Mathayo 10:1-31

Yesu Awatuma Wale Kumi Na Wawili

(Marko 3:13-19; 6:7-13; Luka 6:12-16; 9:1-6)

10:1 Mk 3:13-15; Lk 9:1-5Ndipo Yesu akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, naye akawapa mamlaka juu ya pepo wachafu, ili waweze kuwatoa na kuponya kila ugonjwa na maradhi ya kila aina.

10:2 Lk 6:13-16Haya ndiyo majina ya hao mitume kumi na wawili: wa kwanza, Simoni aitwaye Petro, na Andrea nduguye; Yakobo mwana wa Zebedayo, na Yohana nduguye; Filipo, na Bartholomayo; Tomaso, na Mathayo mtoza ushuru; Yakobo mwana wa Alfayo, na Thadayo; 10:4 Mk 14:10; Mdo 1:16Simoni Mkananayo, na Yuda Iskariote aliyemsaliti Yesu.

10:5 1Fal 16:24; Lk 10:33Hawa kumi na wawili, Yesu aliwatuma akawaagiza: “Msiende miongoni mwa watu wa Mataifa, wala msiingie mji wowote wa Wasamaria. 10:6 Yer 50:6; Mt 15:24Lakini afadhali mshike njia kuwaendea kondoo wa nyumba ya Israeli waliopotea. 10:7 Mt 3:2; Lk 19:9Wakati mnapokwenda, hubirini mkisema, ‘Ufalme wa Mbinguni umekaribia.’ 10:8 Mdo 20:33Ponyeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo wachafu. Mmepata bure, toeni bure. 10:9 Lk 22:35Msichukue dhahabu, wala fedha, wala shaba kwenye vifuko vyenu. 10:10 1Tim 5:18; Hes 18:31Msichukue mkoba wa safari, wala kanzu mbili, wala jozi ya pili ya viatu, wala fimbo, kwa maana mtendakazi anastahili posho yake.

10:11 Lk 10:8“Mji wowote au kijiji chochote mtakapoingia, tafuteni humo mtu anayestahili, nanyi kaeni kwake mpaka mtakapoondoka. 10:12 1Sam 25:6; Lk 10:5-6Mkiingia kwenye nyumba, itakieni amani. 10:13 Lk 10:5; Za 35:13Kama nyumba hiyo inastahili, amani yenu na iwe juu yake. La sivyo, amani yenu na iwarudie ninyi. 10:14 Neh 5:13; Mk 6:11Kama mtu yeyote hatawakaribisha ninyi, wala kusikiliza maneno yenu, kungʼuteni mavumbi kutoka kwenye miguu yenu mtakapokuwa mnatoka kwenye nyumba hiyo au mji huo. 10:15 Mwa 18:20; Yud 7; Mdo 17:30; Mt 11:22-24Amin, nawaambia, itakuwa rahisi zaidi kwa miji ya Sodoma na Gomora kustahimili katika hukumu kuliko mji huo.

Mateso Yanayokuja

(Marko 13:9-13; Luka 21:12-17)

10:16 Lk 10:3; Mdo 20:29; Rum 16:19; 1Kor 14:20“Tazama, ninawatuma kama kondoo katikati ya mbwa mwitu. Kwa hiyo mwe werevu kama nyoka na wapole kama hua.

10:17 Mt 5:22; Mdo 22:19; 26:11“Jihadharini na wanadamu; kwa maana watawapeleka katika mabaraza yao na kuwapiga kwenye masinagogi yao. 10:18 Mdo 25:24-26Nanyi mtaburutwa mbele ya watawala na wafalme kwa ajili yangu, ili kuwa ushuhuda kwao na kwa watu wa Mataifa. 10:19 Kut 4:12; Lk 12:11-12Lakini watakapowapeleka humo, msisumbuke kufikiria mtakalosema, kwa maana mtapewa la kusema wakati huo. 10:20 Mdo 4:8; Yn 14:26Kwa sababu si ninyi mtakaokuwa mkinena, bali ni Roho wa Baba yenu atakayekuwa akinena kupitia kwenu.

10:21 Mik 7:6; Mt 10:35-36“Ndugu atamsaliti ndugu yake ili auawe, naye baba atamsaliti mtoto wake. Watoto nao wataasi dhidi ya wazazi wao na kusababisha wauawe. 10:22 Lk 21:19; Ufu 2:10Watu wote watawachukia kwa ajili ya Jina langu. Lakini yule atakayevumilia hadi mwisho ataokolewa. 10:23 Mt 16:28; Lk 17:30Wakiwatesa katika mji mmoja, kimbilieni mji mwingine. Amin, amin nawaambia, hamtamaliza miji yote ya Israeli kabla Mwana wa Adamu kuja.

10:24 Lk 6:40; Yn 15:20“Mwanafunzi hawezi kumzidi mwalimu wake, wala mtumishi hamzidi bwana wake. 10:25 Mk 3:22; Mt 12:24Yatosha mwanafunzi kuwa kama mwalimu wake, na mtumishi kuwa kama bwana wake. Ikiwa mkuu wa nyumba ameitwa Beelzebuli,10:25 Beelzebuli kwa Kiyunani ni Beelzebubu, yaani mkuu wa pepo wachafu. je, si watawaita zaidi wale wa nyumbani mwake!

Anayestahili Kuogopwa

(Luka 12:2-9)

10:26 Mk 4:22; Lk 8:17“Kwa hiyo msiwaogope hao, kwa maana hakuna kilichofichika ambacho hakitafunuliwa, wala hakuna siri ambayo haitajulikana. Ninalowaambia gizani, ninyi lisemeni mchana peupe. Na lile mnalosikia likinongʼonwa masikioni mwenu, lihubirini juu ya nyumba. 10:28 Isa 8:12-13; Ebr 10:31Msiwaogope wale wauao mwili lakini hawawezi kuua roho. Afadhali mwogopeni yeye awezaye kuiangamiza roho na mwili katika jehanamu.10:28 Jehanamu kwa Kiyunani ni Gehena, maana yake ni Kuzimu, yaani motoni. Je, shomoro wawili hawauzwi kwa senti moja tu? Lakini hakuna hata mmoja wao atakayeanguka chini pasipo Baba yenu kujua. 10:30 1Fal 1:52; Lk 21:18Hata nywele za vichwa vyenu zote zimehesabiwa. 10:31 Mt 6:26; 12:12Hivyo msiogope; kwa maana ninyi ni wa thamani kubwa kuliko shomoro wengi.

Read More of Mathayo 10