Marko 9:33-50, Marko 10:1-12 NEN

Marko 9:33-50

Mabishano Kuhusu Aliye Mkuu Zaidi

(Mathayo 18:1-5; Luka 9:46-48)

9:33 Mt 4:13; Mk 1:29Basi wakafika Kapernaumu na baada ya kuingia nyumbani akawauliza, “Mlikuwa mnabishana nini kule njiani?” 9:34 Lk 22:24Lakini hawakumjibu, kwa sababu njiani walikuwa wakibishana kuhusu nani miongoni mwao alikuwa mkuu zaidi ya wote.

9:35 Mt 20:26; Lk 22:26Akaketi chini, akawaita wote kumi na wawili, akawaambia: “Kama mtu yeyote akitaka kuwa wa kwanza, hana budi kuwa wa mwisho na mtumishi wa wote.”

9:36 Mk 10:16Kisha akamchukua mtoto mdogo, akamsimamisha katikati yao. Akamkumbatia, akawaambia, 9:37 Mt 10:40“Mtu yeyote amkaribishaye mmoja wa hawa watoto wadogo kwa Jina langu, anikaribisha mimi. Naye anikaribishaye mimi, amkaribisha Baba yangu aliyenituma.”

Yeyote Asiye Kinyume Nasi Yuko Upande Wetu

(Luka 9:49-50)

9:38 Hes 11:27-29Yohana akamwambia, “Mwalimu, tumemwona mtu akitoa pepo wachafu kwa jina lako, nasi tukamkataza, kwa sababu yeye si mmoja wetu.”

9:39 1Kor 12:3Yesu akasema, “Msimkataze, kwa kuwa hakuna yeyote atendaye miujiza kwa Jina langu ambaye baada ya kitambo kidogo aweza kunena lolote baya dhidi yangu. 9:40 Mt 12:30; Lk 11:23Kwa maana yeyote asiye kinyume chetu, yuko upande wetu. 9:41 Mt 10:42Amin, nawaambia, yeyote awapaye ninyi kikombe cha maji kwa Jina langu kwa sababu ninyi ni mali ya Kristo, hakika hataikosa thawabu yake.”

Kusababisha Kutenda Dhambi

(Mathayo 18:6-9; Luka 17:1-2)

9:42 Mt 5:29; 18:6; Lk 17:2“Kama mtu yeyote akimsababisha mmojawapo wa wadogo hawa wanaoniamini kutenda dhambi, ingekuwa bora kwake afungiwe jiwe kubwa la kusagia shingoni mwake, na kutoswa baharini. 9:43 Mt 5:29-30; 18:8; 25:41Kama mkono wako ukikusababisha kutenda dhambi, ukate. Ni afadhali kwako kuingia katika uzima ukiwa na mkono mmoja, kuliko kuwa na mikono miwili lakini ukaingia jehanamu, mahali ambako moto hauzimiki. [ 9:44 Isa 66:24Mahali ambako funza wake hawafi wala moto wake hauzimiki.] 9:45 Mt 5:29; 18:8Kama mguu wako ukikusababisha kutenda dhambi, ukate. Ni afadhali kwako kuingia katika uzima ukiwa kiwete, kuliko kuwa na miguu miwili lakini ukaingia jehanamu. [ Mahali ambako funza wake hawafi wala moto hauzimiki.] 9:47 Mt 5:29; 18:9Nalo jicho lako likikusababisha kutenda dhambi, lingʼoe. Ni afadhali kwako kuingia katika Ufalme wa Mungu ukiwa na jicho moja, kuliko kuwa na macho mawili lakini ukatupwa jehanamu, 9:48 Isa 66:24; Mt 25:41mahali ambako

“ ‘funza wake hawafi,

wala moto wake hauzimiki.’

9:49 Law 2:13Kila mmoja atatiwa chumvi kwa moto.

9:50 Mt 5:13; Lk 14:34-35; Kol 4:6; Rum 12:18; 1The 5:13“Chumvi ni nzuri, lakini ikipoteza ladha yake utaifanyaje ili iweze kukolea tena? Mwe na chumvi ndani yenu, mkaishi kwa amani, kila mmoja na mwenzake.”

Read More of Marko 9

Marko 10:1-12

Mafundisho Kuhusu Talaka

(Mathayo 19:1-12; Luka 16:18)

10:1 Yn 10:40; 11:7; Mt 4:23; Mk 4:2Yesu akaondoka huko, akavuka Mto Yordani, akaenda sehemu za Uyahudi. Umati mkubwa wa watu ukaenda kwake tena, naye kama ilivyokuwa desturi yake, akawafundisha.

10:2 Mk 2:16Baadhi ya Mafarisayo wakaja ili kumjaribu kwa kumuuliza, “Je, ni halali mtu kumwacha mke wake?”

Yesu akawajibu, “Je, Mose aliwaamuru nini?”

10:4 Kum 24:1-4; Mt 5:31Wakajibu, “Mose aliruhusu kwamba mume anaweza kumwandikia mkewe hati ya talaka na kumwacha.”

10:5 Za 95:8; Ebr 3:15Yesu akawaambia, “Mose aliwaandikia sheria hiyo kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu. 10:6 Mwa 1:27; 5:2Lakini tangu mwanzo wa uumbaji, ‘Mungu aliwaumba mwanaume na mwanamke. 10:7 Mwa 2:2; 1Kor 6:16; Efe 5:31Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake na kuambatana na mkewe, na hao wawili watakuwa mwili mmoja.’ 10:8 Mwa 2:24; 1Kor 6:16Kwa hiyo hawatakuwa wawili tena, bali mwili mmoja. Basi, alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.”

Walipokuwa tena ndani ya nyumba, wanafunzi wake wakamuuliza kuhusu jambo hili. 10:11 Mt 5:32; Lk 16:8Akawajibu, “Mtu yeyote amwachaye mkewe na kuoa mke mwingine, anazini naye. 10:12 Rum 7:3; 1Kor 7:10-11Naye mwanamke amwachaye mumewe na kuolewa na mume mwingine, anazini.”

Read More of Marko 10