Marko 7:1-30 NEN

Marko 7:1-30

Kilicho Safi Na Kilicho Najisi

(Mathayo 15:1-20)

7:1 Mt 15:1Mafarisayo na baadhi ya walimu wa sheria waliokuwa wametoka Yerusalemu wakakusanyika mbele ya Yesu. 7:2 Mdo 11:8; Rum 14:14Wakawaona baadhi ya wanafunzi wake wakila chakula kwa mikono iliyo najisi, yaani, bila kunawa kama ilivyotakiwa na sheria ya dini ya Wayahudi. 7:3 Mk 7:5-13; Lk 11:38-39(Kwa kuwa Mafarisayo na Wayahudi wote hawali chakula pasipo kunawa kwa kufuata desturi za wazee wao. 7:4 Mt 23:25Wanapotoka sokoni hawawezi kula pasipo kunawa. Pia kuna desturi nyingine nyingi wanazofuata kama vile jinsi ya kuosha vikombe, vyungu na vyombo vya shaba.)

7:5 Gal 1:14; Kol 2:8Kwa hiyo wale Mafarisayo na walimu wa sheria wakamuuliza Yesu, “Mbona wanafunzi wako hawafuati desturi za wazee, na badala yake wanakula kwa mikono najisi?”

7:6 Isa 29:13; Mt 15:8Yesu akawajibu, “Nabii Isaya alisema ukweli alipotabiri juu yenu, ninyi wanafiki. Kama ilivyoandikwa:

“ ‘Watu hawa huniheshimu kwa midomo yao,

lakini mioyo yao iko mbali nami.

7:7 Isa 29:13Huniabudu bure,

nayo mafundisho yao ni maagizo ya wanadamu tu.’

7:8 Mk 7:3Ninyi mmeziacha amri za Mungu na kushika desturi za watu.”

7:9 Mk 7:3Naye akawaambia, “Ninyi mnayo njia nzuri ya kukataa amri za Mungu ili mpate kuyashika mapokeo yenu! 7:10 Kut 20:21; Kum 5:16; Kut 21:17; Law 20:9Kwa mfano, Mose alisema, ‘Waheshimu baba yako na mama yako,’ na, ‘Yeyote amtukanaye baba yake au mama yake, na auawe.’ 7:11 Mt 23:16-18Lakini ninyi mwafundisha kwamba mtu akimwambia baba yake au mama yake, ‘Kile ambacho ningeweza kukusaidia ni Korbani’ (yaani kimewekwa wakfu kwa Mungu), basi hawajibiki tena kumsaidia baba yake au mama yake. 7:13 Ebr 4:12; Mk 7:3Kwa njia hiyo ninyi mnabatilisha neno la Mungu kwa mapokeo yenu mliyojiwekea. Nanyi mnafanya mambo mengi ya aina hiyo.”

7:14 Mt 15:10Yesu akaita tena ule umati wa watu, akawaambia, “Nisikilizeni, kila mmoja wenu na mwelewe jambo hili. 7:15 Mdo 10:14, 15Hakuna kitu kinachomwingia mtu kimtiacho unajisi, lakini kile kimtokacho ndicho kimtiacho unajisi. [ 7:16 Mt 11:15Kama mtu yeyote ana masikio ya kusikia na asikie.]”

7:17 Mk 9:28Akiisha kuuacha ule umati wa watu na kuingia ndani, wanafunzi wake wakamuuliza maana ya mfano ule. Akawajibu, “Je, hata nanyi hamwelewi? Je, hamfahamu kwamba kitu kimwingiacho mtu hakimtii unajisi? 7:19 Kol 2:16; 1Tim 4:3-5; Mdo 10:15Mtu akila kitu hakiingii moyoni mwake bali tumboni, na baadaye hutolewa nje ya mwili wake.” (Kwa kusema hivi, Yesu alivihalalisha vyakula vyote kuwa ni “safi.”)

Akaendelea kusema, “Kile kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi. 7:21 Mwa 6:5; 8:21; Mt 15:21-28Kwa maana kutoka ndani ya moyo wa mtu hutoka mawazo mabaya, uasherati, wizi, uuaji, uzinzi, 7:22 Mt 20:15tamaa mbaya, uovu, udanganyifu, ufisadi, wivu, matukano, kiburi na upumbavu. Maovu haya yote hutoka ndani ya mtu, nayo ndiyo yamtiayo mtu unajisi.”

Imani Ya Mwanamke Msirofoinike

(Mathayo 15:21-28)

7:24 Mt 21:21Ndipo Yesu akaondoka hapo akaenda sehemu za Tiro. Akaingia katika nyumba moja, naye hakutaka mtu yeyote ajue kwamba yuko humo. Lakini hakuweza kujificha. 7:25 Mt 4:24Mara mwanamke mmoja, ambaye binti yake mdogo alikuwa na pepo mchafu, akaja na kumpigia magoti miguuni pake. Basi huyo mwanamke alikuwa Myunani, aliyezaliwa Foinike ya Siria.7:26 Kulikuwa na Foinike ya Siria (ndio Shamu) na Foinike ya Libya. Akamsihi Yesu amtoe binti yake huyo pepo mchafu.

Yesu akamwambia, “Waache watoto washibe kwanza, kwa maana si vyema kuchukua chakula cha watoto na kuwatupia mbwa.”

Lakini yule mwanamke akamjibu, “Bwana, hata mbwa walio chini ya meza hula makombo ya chakula cha watoto.”

Ndipo Yesu akamjibu, “Kwa sababu ya jibu lako, nenda zako nyumbani; yule pepo mchafu amemtoka binti yako.”

Akaenda zake nyumbani akamkuta binti yake amelala kitandani, yule pepo mchafu akiwa amemtoka.

Read More of Marko 7