Marko 3:31-35, Marko 4:1-29 NEN

Marko 3:31-35

Mama Na Ndugu Zake Yesu

(Mathayo 12:46-50; Luka 8:19-21)

3:31 Mt 12:46; Lk 8:19Kisha wakaja ndugu zake Yesu pamoja na mama yake. Wakasimama nje, wakamtuma mtu kumwita. Umati wa watu ulikuwa umeketi kumzunguka, nao wakamwambia, “Mama yako na ndugu zako wako nje, wanakutafuta.”

Akawauliza, “Mama yangu na ndugu zangu ni nani?”

Kisha akawatazama wale watu waliokuwa wameketi kumzunguka pande zote, akasema, “Hawa ndio mama yangu na ndugu zangu. Mtu yeyote anayetenda mapenzi ya Mungu, huyo ndiye ndugu yangu, na dada yangu na mama yangu.”

Read More of Marko 3

Marko 4:1-29

Mfano Wa Mpanzi

(Mathayo 13:1-9; Luka 8:4-8)

4:1 Mk 2:13; 3:7Yesu akaanza kufundisha tena kando ya bahari. Umati wa watu uliokuwa umekusanyika kumzunguka ulikuwa mkubwa, kiasi kwamba ilimbidi Yesu aingie kwenye mashua iliyokuwa baharini na kuketi humo, nao watu wote walikuwa ufuoni mwa bahari. 4:2 Mk 2:11; 3:23Akawafundisha mambo mengi kwa mifano, naye katika mafundisho yake akasema: 4:3 Mk 4:26“Sikilizeni! Mpanzi alitoka kwenda kupanda mbegu zake. Alipokuwa akitawanya mbegu, nyingine zilianguka kando ya njia, nao ndege wakaja na kuzila. Nyingine zilianguka kwenye ardhi yenye mwamba isiyo na udongo wa kutosha. Zikaota haraka, kwa kuwa udongo ulikuwa haba. Lakini jua lilipozidi, mimea ikanyauka na kukauka kwa kuwa mizizi yake haikuwa na kina. Mbegu nyingine zilianguka kwenye miiba, nayo miiba hiyo ikakua, ikaisonga hiyo mimea, hivyo haikutoa mazao. 4:8 Yn 15:5; Kol 1:16Mbegu nyingine zilianguka kwenye udongo mzuri, zikaota vizuri na kukua, zikatoa mazao, moja mara thelathini, nyingine mara sitini, na nyingine mara mia moja.”

4:9 Mk 4:23; Mt 11:15Kisha Yesu akasema, “Mwenye masikio ya kusikia, na asikie.”

Sababu Za Mifano

(Mathayo 13:10-17; Luka 8:9-10)

4:10 Mt 13:10; Lk 8:9Alipokuwa peke yake, watu waliokuwepo naye pamoja na wanafunzi wake kumi na wawili wakamuuliza kuhusu mifano yake. 4:11 Mt 3:2; 1The 4:12; 1Tim 3:7Naye akawaambia, “Ninyi mmepewa kujua siri ya Ufalme wa Mungu. Lakini kwa wale walioko nje, kila kitu husemwa kwao kwa mifano, 4:12 Isa 6:9-10; Mk 13:13-15ili,

“ ‘daima waone lakini wasitambue,

daima wasikie lakini wasielewe;

wasije wakageuka, wakatubu na kusamehewa!’ ”

Yesu Afafanua Maana Ya Mfano Wa Mbegu

(Mathayo 13:18-23; Luka 8:11-15)

Kisha Yesu akawauliza, “Hamwelewi maana ya mfano huu? Basi mtaelewaje mifano mingine? 4:14 Mdo 16:6; Flp 1:14Yule mpanzi hupanda neno. 4:15 Mt 4:10Hawa ndio wale walio kando ya njia ambako neno lilipandwa. Walisikiapo neno, Shetani huja mara na kulinyakua lile neno lililopandwa ndani yao. Nazo zile mbegu zilizoanguka kwenye udongo wenye miamba, ni wale wanaolisikia neno, na mara hulipokea kwa furaha. Lakini kwa kuwa hawana mizizi, wao hudumu kwa muda mfupi tu. Kisha dhiki au mateso yanapoinuka kwa ajili ya lile neno, mara wao huiacha imani. Lakini wengine, kama mbegu iliyopandwa kwenye miiba, hulisikia lile neno; 4:19 1Tim 6:9-17; 1Yn 2:15-17lakini masumbufu ya maisha haya, na udanganyifu wa mali na tamaa ya mambo mengine huja na kulisonga lile neno na kulifanya lisizae. Wengine, kama mbegu iliyopandwa kwenye udongo mzuri, hulisikia lile neno, wakalipokea na kuzaa mazao. Wao huzaa mara thelathini, au mara sitini, au mara mia ya mbegu iliyopandwa.”

Mfano Wa Taa

(Luka 8:16-18)

4:21 Mt 5:15Akawaambia, “Je, taa huwashwa na kufunikwa chini ya kikapu au mvunguni mwa kitanda? Je, haiwashwi na kuwekwa juu ya kinara chake? 4:22 Yer 16:17; Lk 12:2Kwa kuwa hakuna kilichofichika ambacho hakitafunuliwa, wala hakuna jambo lolote la siri ambalo halitaletwa nuruni. 4:23 Mk 4:9; Mt 11:15Mwenye masikio ya kusikia, na asikie.”

4:24 Mt 7:2; Lk 6:38Naye akawaambia, “Kuweni waangalifu na yale mnayosikia. Kipimo kile mpimacho, ndicho mtakachopimiwa ninyi, hata na zaidi. 4:25 Mt 13:12; 25:29Kwa maana kila mtu aliye na kitu atapewa zaidi, naye atakuwa navyo tele. Lakini yule asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyangʼanywa.”

Mfano Wa Mbegu Inayoota

4:26 Mt 13:24Pia akawaambia, “Ufalme wa Mungu unafanana na mtu apandaye mbegu shambani. 4:27 Yak 5:7Akiisha kuzipanda, usiku na mchana, akiwa amelala au ameamka, mbegu huota na kukua pasipo yeye kujua ikuavyo. Udongo huifanya iote kuwa mche, halafu suke, kisha nafaka kamili kwenye suke. 4:29 Ufu 14:15; Yoe 3:13Lakini nafaka inapokuwa imekomaa, mara mkulima huingia shambani na mundu wa kuvunia, maana mavuno yamekuwa tayari.”

Read More of Marko 4