Luka 23:26-56 NEN

Luka 23:26-56

Kusulubiwa Kwa Yesu

(Mathayo 27:32-44; Marko 15:21-32; Yohana 19:17-27)

23:26 Mt 27:32; Mk 15:21; Yn 19:17Walipokuwa wakienda naye, wakamkamata mtu mmoja aitwaye Simoni mwenyeji wa Kirene, aliyekuwa anapita zake kuingia mjini kutoka shambani. Wakambebesha msalaba, wakamlazimisha auchukue nyuma ya Yesu. 23:27 Lk 8:52Idadi kubwa ya watu wakamfuata Yesu, wakiwamo wanawake waliokuwa wakimlilia na kumwombolezea. 23:28 Lk 19:41-44; 21:23-24Yesu akawageukia, akawaambia, “Enyi binti za Yerusalemu, msinililie mimi bali jililieni ninyi wenyewe na watoto wenu. 23:29 Mt 24:19Kwa maana wakati utafika mtakaposema, ‘Wamebarikiwa wanawake tasa, ambao matumbo yao hayakuzaa, wala matiti yao hayakunyonyesha!’ 23:30 Hos 10:8; Ufu 6:16Ndipo

“ ‘wataiambia milima, “Tuangukieni!”

na vilima, “Tufunikeni!” ’

23:31 Eze 20:47Kwa maana kama wamefanya hivi kwa mti mbichi, kwa mti mkavu itakuwaje?”

23:32 Isa 53:12; Mt 27:38Watu wengine wawili wahalifu, walipelekwa pamoja na Yesu ili wakasulubiwe. Walipofika mahali paitwapo Fuvu la Kichwa, hapo ndipo walipomsulubisha Yesu pamoja na hao wahalifu, mmoja upande wake wa kuume na mwingine upande wake wa kushoto. 23:34 Mt 11:25; 5:44; Za 22:18Yesu akasema, “Baba, wasamehe, kwa maana hawajui walitendalo!” Wakagawana nguo zake kwa kupiga kura.

23:35 Za 22:17; Isa 42:1; Zek 12:10; Mt 27:39; Mk 15:29Watu wakasimama hapo wakimwangalia, nao viongozi wa Wayahudi wakamdhihaki wakisema, “Aliokoa wengine! Ajiokoe mwenyewe basi, kama yeye ndiye Kristo wa Mungu, Mteule wake.”

23:36 Za 22:7; 69:21; Mt 27:48Askari nao wakaja, wakamdhihaki. Wakamletea siki ili anywe, 23:37 Lk 4:3, 9na wakamwambia, “Kama wewe ni Mfalme wa Wayahudi, jiokoe mwenyewe.”

23:38 Mt 2:2Kwenye msalaba juu ya kichwa chake, kulikuwa na maandishi haya: Huyu ndiye Mfalme wa Wayahudi.

Maandishi haya yalikuwa yameandikwa kwa lugha za Kiyunani, Kilatini na Kiebrania.

23:39 Mt 27:44; Mk 15:32Mmoja wa wale wahalifu waliosulubiwa pamoja naye akamtukana, akasema: “Wewe si ndiye Kristo? Jiokoe mwenyewe na utuokoe na sisi.”

Lakini yule mhalifu mwingine akamkemea mwenzake, akasema, “Je, wewe humwogopi Mungu, wakati uko kwenye adhabu iyo hiyo? 23:41 Lk 23:4Sisi tumehukumiwa kwa haki kwa kuwa tunapata tunayostahili kwa ajili ya matendo yetu. Lakini huyu mtu hajafanya kosa lolote.”

23:42 Mt 16; 27Kisha akasema, “Yesu, unikumbuke utakapokuja katika Ufalme wako.”

23:43 1Kor 12:3-4; Ufu 2:7Yesu akamjibu, “Amin, nakuambia, leo hii utakuwa pamoja nami Paradiso.”23:43 Paradiso maana yake bustani nzuri, hapa ina maana mahali zinapokwenda roho za wacha Mungu, yaani watakatifu.

Kifo Cha Yesu

(Mathayo 27:45-56; Marko 15:33-41; Yohana 19:28-30)

23:44 Amo 8:9Ilikuwa kama saa sita mchana, nalo giza likafunika nchi yote hadi saa tisa, 23:45 Kut 26:31-33; Ebr 3:8; 10:19-20kwa sababu jua liliacha kutoa nuru. Pazia la Hekalu likachanika vipande viwili. 23:46 Mt 27:50; Za 31:5; 1Pet 2:23; Yn 19:30Yesu akapaza sauti yake akasema, “Baba, mikononi mwako naikabidhi roho yangu.” Baada ya kusema haya, akakata roho.

23:47 Mt 9:8Yule jemadari alipoona yaliyotukia, akamsifu Mungu, akasema, “Hakika, mtu huyu alikuwa mwenye haki.” 23:48 Lk 18:13Watu wote waliokuwa wamekusanyika hapo kushuhudia tukio hili walipoyaona hayo, wakapigapiga vifua vyao kwa huzuni na kwenda zao. 23:49 Lk 8:2; Za 38:11Lakini wale wote waliomfahamu, pamoja na wale wanawake waliokuwa wamemfuata kutoka Galilaya, walisimama kwa mbali wakiyatazama mambo haya.

Maziko Ya Yesu

(Mathayo 27:57-61; Marko 15:42-47; Yohana 19:38-42)

23:50 Mt 27:59; Mk 15:46Basi kulikuwa na mtu mmoja mwema na mwenye haki, jina lake Yosefu. Yeye alikuwa mjumbe wa Baraza la Wayahudi,23:50 Baraza la Wayahudi hapa ina maana ya Sanhedrin ambalo lilikuwa ndilo baraza la juu kabisa la utawala wa Kiyahudi, lililoundwa na wazee 70 pamoja na kuhani mkuu. 23:51 Lk 2:25, 38lakini yeye hakuwa amekubaliana na maamuzi na vitendo vya viongozi wenzake. Huyu alikuwa mwenyeji wa Arimathaya huko Uyahudi, naye alikuwa anaungojea Ufalme wa Mungu kwa matarajio makubwa. Yosefu alikwenda kwa Pilato, akaomba apewe mwili wa Yesu. Akaushusha kutoka msalabani, akaufunga katika kitambaa cha kitani safi, na kuuweka katika kaburi lililochongwa kwenye mwamba, ambalo halikuwa limezikiwa mtu mwingine bado. 23:54 Mt 27:62Ilikuwa Siku ya Maandalizi, nayo Sabato ilikuwa karibu kuanza.

23:55 Lk 8:2; Mk 15:47Wale wanawake waliokuwa wamekuja pamoja na Yesu wakimfuata kutoka Galilaya wakamfuata Yosefu, wakaliona kaburi na jinsi mwili wa Yesu ulivyolazwa. 23:56 Mk 16:1; Lk 24:1; Kut 12:16; 20:11Kisha wakarudi nyumbani, wakaandaa manukato na marhamu ya kuupaka huo mwili. Lakini wakapumzika siku ya Sabato kama ilivyoamriwa.

Read More of Luka 23