Luka 20:27-47, Luka 21:1-4 NEN

Luka 20:27-47

Ufufuo Na Ndoa

(Mathayo 22:23-33; Marko 12:18-27)

20:27 Mdo 23:8; 1Kor 15:12; Mdo 4:1Baadhi ya Masadukayo, wale wasemao kwamba hakuna ufufuo wa wafu, wakamjia Yesu na kumuuliza, 20:28 Kum 25:5; Mwa 38:8“Mwalimu, Mose alituandikia kwamba kama ndugu wa mtu akifa na kumwacha mkewe bila mtoto, basi huyo mtu inampasa amwoe huyo mjane ili amzalie ndugu yake watoto. Basi palikuwepo ndugu saba. Yule wa kwanza akaoa, akafa bila kuzaa mtoto. Kisha yule wa pili akamwoa huyo mjane, naye akafa bila mtoto, naye wa tatu pia akamwoa. Vivyo hivyo ndugu wote saba wakawa wamemwoa huyo mwanamke, na wote wakafa pasipo yeyote kupata mtoto. Mwishowe, yule mwanamke naye akafa. Sasa basi, siku ya ufufuo huyo mwanamke atakuwa mke wa nani, maana aliolewa na ndugu wote saba?”

Yesu akawajibu, “Katika maisha haya watu huoa na kuolewa. 20:35 Mt 12:32Lakini wale ambao wamehesabiwa kwamba wanastahili kupata nafasi katika ulimwengu ule na katika ufufuo wa wafu, hawaoi wala hawaolewi. 20:36 Yn 1:12; 1Yn 3:1-2Hawa hawawezi kufa tena, kwa maana wao ni kama malaika. Wao ni watoto wa Mungu, kwa sababu ni watoto wa ufufuo. 20:37 Kut 3:6Hata Mose alidhihirisha kuwa wafu wanafufuka, kwa habari ya kile kichaka kilichokuwa kikiwaka moto bila kuteketea, alipomwita Bwana, ‘Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaki, na Mungu wa Yakobo.’ 20:38 Rum 6:10-11Yeye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai, kwa kuwa kwake wote ni hai.”

Baadhi ya walimu wa sheria wakasema, “Mwalimu, umesema sawasawa kabisa!”

20:40 Mt 22:46; Mk 12:34Baada ya hayo hakuna mtu aliyethubutu kumuuliza maswali tena.

Kristo Ni Mwana Wa Nani?

(Mathayo 22:41-46; Marko 12:35-37)

20:41 Mt 22:42; Mk 12:3520:41 Mt 22:41-45; Mk 12:35-37Kisha Yesu akawaambia, “Imekuwaje basi wao husema Kristo20:41 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta. ni Mwana wa Daudi? 20:42 Za 110:1; Mdo 2:34Daudi mwenyewe anasema katika Kitabu cha Zaburi:

“ ‘Bwana alimwambia Bwana wangu:

“Keti mkono wangu wa kuume,

20:43 Za 110:1; Mt 22:44hadi nitakapowaweka adui zako

chini ya miguu yako.” ’

Ikiwa Daudi anamwita yeye ‘Bwana,’ basi atakuwaje mwanawe?”

Yesu Awashutumu Walimu Wa Sheria

(Mathayo 23:1-36; Marko 12:38-40)

20:45 Lk 11:43Wakati watu wote walikuwa wanamsikiliza, Yesu akawaambia wanafunzi wake, 20:46 Lk 11:43“Jihadharini na walimu wa sheria. Wao hupenda kutembea wakiwa wamevaa mavazi marefu, na kusalimiwa kwa heshima masokoni. Hupenda kukaa kwenye viti vya mbele katika masinagogi, na kukaa kwenye nafasi za heshima katika karamu. 20:47 Mt 23:14Wao hula nyumba za wajane, na ili waonekane kuwa wema, wanasali sala ndefu. Watu kama hawa watapata hukumu iliyo kuu sana.”

Read More of Luka 20

Luka 21:1-4

Sadaka Ya Mjane

(Marko 12:41-44)

21:1 Mt 27:6; Yn 8:20Yesu alipoinua macho yake, aliwaona matajiri wakiweka sadaka zao kwenye sanduku la hazina ya Hekalu. Akamwona pia mjane mmoja maskini akiweka humo sarafu mbili ndogo za shaba. 21:3 2Kor 8:12Yesu akasema, “Amin, nawaambia, huyu mjane maskini ameweka humo zaidi ya watu wengine wote. 21:4 2Kor 8:12Hawa watu wengine wote wametoa sadaka kutokana na wingi wa mali zao. Lakini huyu mjane ametoa kutokana na umaskini wake vyote alivyokuwa navyo, hata kile alichohitaji ili kuishi.”

Read More of Luka 21