Luka 2:1-20 NEN

Luka 2:1-20

Kuzaliwa Kwa Yesu

(Mathayo 1:18-25)

2:1 Lk 3:1; Mt 22:17; 24:14Siku zile Kaisari Augusto alitoa amri kwamba watu wote waandikishwe katika ulimwengu wa Kirumi. 2:2 Mdo 21:3; Mt 4:24; Mdo 15:23, 41(Orodha hii ndiyo ya kwanza iliyofanyika wakati Krenio alikuwa mtawala wa Shamu2:2 Shamu inamaanisha Syria.). Kila mtu alikwenda kuandikishwa katika mji wake alikozaliwa.

2:4 Yn 7:42Hivyo Yosefu akapanda kutoka mji wa Nazareti ulioko Galilaya kwenda Uyahudi, mpaka Bethlehemu, mji wa Daudi, kwa sababu yeye alikuwa wa ukoo na wa nyumba ya Daudi. 2:5 Lk 1:27; Mt 1:16Alikwenda huko kujiandikisha pamoja na Maria, ambaye alikuwa amemposa naye alikuwa mjamzito. Wakiwa Bethlehemu, wakati wa Maria wa kujifungua ukawa umetimia, 2:7 Mt 1:25naye akamzaa mwanawe, kifungua mimba. Akamfunika nguo za kitoto na kumlaza katika hori ya kulia ngʼombe, kwa sababu hapakuwa na nafasi katika nyumba ya wageni.

Wachungaji Na Malaika

Katika eneo lile walikuwako wachungaji waliokuwa wakikaa mashambani, wakilinda makundi yao ya kondoo usiku. 2:9 Lk 1:11; Mdo 5:19Ghafula tazama, malaika wa Bwana akawatokea, nao utukufu wa Bwana ukawangʼaria kotekote, wakaingiwa na hofu. 2:10 Mt 14:27Lakini malaika akawaambia: “Msiogope. Kwa maana tazama nawaletea habari njema za furaha itakayokuwa kwa watu wote. 2:11 Yn 3:17; Rum 11:14; Mdo 3:20; 9:22Leo katika mji wa Daudi kwa ajili yenu amezaliwa Mwokozi, ndiye Kristo2:11 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta. Bwana. 2:12 1Sam 10:7; Za 86:17Hii ndiyo itakayokuwa ishara kwenu: Mtamkuta mtoto mchanga amefunikwa nguo za kitoto na kulazwa katika hori ya kulia ngʼombe.”

2:13 Dan 7:10; Mwa 28:12; 32:12; Za 103:20, 21; 148:2; Ebr 1:14; Ufu 5:11Ghafula pakawa na jeshi kubwa la mbinguni pamoja na huyo malaika wakimsifu Mungu wakisema,

2:14 Isa 9:6; Rum 5:1“Atukuzwe Mungu juu mbinguni,

na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia.”

Hao malaika walipokwisha kuondoka na kwenda zao mbinguni, wale wachungaji wakasemezana wao kwa wao, “Twendeni Bethlehemu tukaone mambo haya ya ajabu yaliyotukia, ambayo Bwana ametuambia habari zake.”

2:16 Lk 2:7Hivyo wakaenda haraka Bethlehemu, wakawakuta Maria na Yosefu na yule mtoto mchanga akiwa amelala katika hori la kulia ngʼombe. 2:17 Lk 2:10-12Walipomwona yule mtoto, wakawaeleza yale waliyokuwa wameambiwa kuhusu huyo mtoto. Nao wote waliosikia habari hizi wakastaajabia yale waliyoambiwa na wale wachungaji wa kondoo. 2:19 Lk 2:51Lakini Maria akayaweka mambo haya yote moyoni mwake na kuyatafakari. 2:20 Mt 9:8Wale wachungaji wakarudi, huku wakimtukuza Mungu na kumsifu kwa ajili ya mambo yote waliyokuwa wameambiwa na kuyaona.

Read More of Luka 2