Luka 18:31-43, Luka 19:1-10 NEN

Luka 18:31-43

Yesu Atabiri Kifo Chake Mara Ya Tatu

(Mathayo 20:17-19; Marko 10:32-34)

18:31 Lk 9:51; Za 22; Mt 8:20Yesu akawachukua wale wanafunzi wake kumi na wawili kando na kuwaambia, “Tunapanda kwenda Yerusalemu, na kila kitu kilichoandikwa na manabii kumhusu Mwana wa Adamu kitatimizwa. 18:32 Lk 23:1; Mt 16:21; Mdo 2:23Kwa kuwa atatiwa mikononi mwa watu wasiomjua Mungu, nao watamdhihaki, watamtukana na kumtemea mate, watampiga mijeledi na kumuua. 18:33 Mt 16:21Naye siku ya tatu atafufuka.”

18:34 Mk 9:32; Lk 9:45Wanafunzi wake hawakuelewa mambo haya, kwa kuwa maana yake ilikuwa imefichika kwao, nao hawakujua Yesu alikuwa anazungumzia nini.

Yesu Amponya Kipofu Karibu Na Yeriko

(Mathayo 20:29-34; Marko 10:46-52)

18:35 Lk 19:1-418:35 Mt 20:29-34; Mk 10:46-52Yesu alipokuwa anakaribia Yeriko, kipofu mmoja alikuwa ameketi kando ya njia akiomba msaada. Kipofu huyo aliposikia umati wa watu ukipita, akauliza, “Kuna nini?” 18:37 Mt 9:27; 17:15; Lk 18:13Wakamwambia, “Yesu wa Nazareti anapita.”

18:38 Lk 18:39; Mt 9:27; 17:15; Lk 18:13Akapaza sauti, akasema, “Yesu, Mwana wa Daudi, nihurumie!”

18:39 Lk 18:38Wale waliokuwa wametangulia mbele wakamkemea, wakamwambia akae kimya. Lakini yeye akapaza sauti zaidi, “Mwana wa Daudi, nihurumie!”

Yesu akasimama, akawaamuru wamlete huyo mtu kwake. Alipokaribia, Yesu akamuuliza, “Unataka nikufanyie nini?”

Akajibu, “Bwana, nataka kuona.”

18:42 Mt 9:22Yesu akamwambia, “Basi upate kuona. Imani yako imekuponya.” 18:43 Mt 9:8; Lk 13:17Akapata kuona saa ile ile, akamfuata Yesu, huku akimsifu Mungu. Watu wote walipoona mambo hayo, nao wakamsifu Mungu.

Read More of Luka 18

Luka 19:1-10

Zakayo Mtoza Ushuru

19:1 Lk 18:35Yesu akaingia Yeriko, naye alikuwa anapita katikati ya huo mji. Tazama, palikuwa na mtu mmoja mkuu wa watoza ushuru naye alikuwa tajiri, jina lake Zakayo. Yeye alikuwa akijitahidi kumwona Yesu ni mtu wa namna gani. Lakini kutokana na umati mkubwa wa watu hakuweza kwa sababu alikuwa mfupi wa kimo. 19:4 1Fal 10:27; 1Nya 27:28; Lk 18:37Kwa hiyo akatangulia mbio mbele ya umati wa watu akapanda juu ya mkuyu ili amwone Yesu, kwa sababu angeipitia njia ile.

Yesu alipofika pale chini ya huo mkuyu, akatazama juu, akamwambia, “Zakayo, shuka upesi, kwa maana leo nitakuwa mgeni nyumbani kwako!” Hivyo Zakayo akashuka upesi, akamkaribisha Yesu nyumbani kwake kwa furaha kubwa.

19:7 Mt 9:11Watu wote walipoona hivyo, wakaanza kunungʼunika wakisema, “Amekwenda kuwa mgeni wa ‘mtu mwenye dhambi.’ ”

19:8 Lk 7:13; 3:12-13; Hes 5:7; Eze 33:14-15Lakini Zakayo akasimama na kumwambia Bwana, “Tazama, Bwana! Sasa hivi nusu ya mali yangu ninawapa maskini, nami kama nimemdhulumu mtu yeyote kitu chochote, nitamrudishia mara nne ya hicho kiwango.”

19:9 Rum 4:16; Gal 3:17Ndipo Yesu akamwambia, “Leo, wokovu umeingia nyumbani humu, kwa sababu huyu naye ni mwana wa Abrahamu. 19:10 Eze 34:12-16; Yn 3:17Kwa maana Mwana wa Adamu amekuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea.”

Read More of Luka 19