Luka 10:25-42, Luka 11:1-4 NEN

Luka 10:25-42

Mfano Wa Msamaria Mwema

10:25 Mt 19:16; Lk 18:18Wakati huo mtaalamu mmoja wa sheria alisimama ili kumjaribu Yesu, akamuuliza, “Mwalimu, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?”

Yesu akamjibu, “Imeandikwaje katika Sheria? Kwani unasoma nini humo?”

10:27 Kum 6:5; Law 19:18; Mt 5:43Akajibu, “ ‘Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote’; tena, ‘Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.’ ”

10:28 Law 18; 5; Rum 7:10Yesu akamwambia, “Umejibu vyema. Fanya hivyo nawe utaishi.”

10:29 Lk 16:15Lakini yule mtaalamu wa sheria, akitaka kujionyesha kuwa mwenye haki, akamuuliza Yesu, “Jirani yangu ni nani?”

Yesu akamjibu akasema, “Mtu mmoja alikuwa akiteremka kutoka Yerusalemu kwenda Yeriko, naye akaangukia mikononi mwa wanyangʼanyi. Wakampiga, wakaondoka, wakamwacha akiwa karibu kufa. 10:31 Law 21:1-3Kuhani mmoja alikuwa akipitia njia ile, alipomwona huyo mtu, akapita upande mwingine, akamwacha hapo barabarani. Vivyo hivyo, Mlawi mmoja naye alipofika mahali pale, alimwona, akapita upande mwingine, akamwacha hapo barabarani 10:33 Mt 10:5Lakini Msamaria mmoja aliyekuwa akisafiri alipomwona, alimhurumia. Akaenda alipokuwa na akasafisha majeraha yake kwa divai na mafuta, kisha akayafunga. Ndipo akampandisha kwenye punda wake, akampeleka mpaka kwenye nyumba ya wageni na kumtunza. Kesho yake, yule Msamaria akachukua dinari mbili10:35 Dinari mbili ni sawa na mshahara wa kibarua wa siku mbili. akampa yule mwenye nyumba ya wageni na kusema, ‘Mtunze, nami nirudipo nitakulipa gharama yoyote ya ziada uliyotumia kwa ajili yake.’

“Ni yupi basi miongoni mwa hawa watatu wewe unadhani ni jirani yake yule mtu aliyeangukia mikononi mwa wanyangʼanyi?”

Yule mtaalamu wa sheria akajibu, “Ni yule aliyemhurumia.”

Ndipo Yesu akamwambia, “Nenda, ukafanye vivyo hivyo.”

Yesu Awatembelea Martha Na Maria

10:38 Yn 11:1; 12:2-3Ikawa Yesu na wanafunzi wake walipokuwa wakienda Yerusalemu, akaingia kwenye kijiji kimoja ambapo mwanamke mmoja aliyeitwa Martha alimkaribisha nyumbani kwake. 10:39 Lk 8:35Martha alikuwa na mdogo wake aliyeitwa Maria, ambaye aliketi chini miguuni mwa Bwana akisikiliza yale aliyokuwa akisema. 10:40 Mk 4:38Lakini Martha alikuwa akihangaika na maandalizi yote yaliyokuwa yafanyike. Martha akaja kwa Yesu na kumuuliza, “Bwana, hujali kwamba ndugu yangu ameniachia kazi zote mwenyewe? Basi mwambie anisaidie.”

10:41 Mt 6:25-34; Lk 12:11, 22Lakini Bwana akamjibu, “Martha, Martha, mbona unasumbuka na kuhangaika na mengi? 10:42 Za 27:4Lakini kunahitajika kitu kimoja tu. Maria amechagua kile kilicho bora, wala hakuna mtu atakayemwondolea.”

Read More of Luka 10

Luka 11:1-4

Yesu Afundisha Wanafunzi Wake Kuomba

(Mathayo 6:9-13; 7:7-11)

11:1 Lk 3:21; Yn 13:13Siku moja, Yesu alikuwa mahali fulani akiomba. Alipomaliza kuomba, mmoja wa wanafunzi wake akamwambia, “Bwana, tufundishe kuomba, kama vile Yohana alivyowafundisha wanafunzi wake.”

11:2 Mt 3:211:2 Mt 6:9-13Akawaambia, “Mnapoomba, semeni:

“ ‘Baba yetu (uliye mbinguni),

jina lako litukuzwe,

ufalme wako uje.

(Mapenzi yako yafanyike

hapa duniani kama huko mbinguni.)

Utupatie kila siku riziki yetu.

11:4 Mt 18:35; Mk 11:25; Mt 26:41; Yak 1:13Utusamehe dhambi zetu,

kwa kuwa na sisi huwasamehe wote wanaotukosea.

Wala usitutie majaribuni

(bali utuokoe kutoka kwa yule mwovu).’ ”

Read More of Luka 11