Walawi 26:14-46, Walawi 27:1-34 NEN

Walawi 26:14-46

Adhabu Ya Kutokutii

(Kumbukumbu 28:15-68)

26:14 Kum 28:15-68; Mal 2:2“ ‘Lakini kama hamtanisikiliza na kutimiza maagizo haya yote, 26:15 Mwa 17:7; 2Fal 17:15nanyi kama mtazikataa amri zangu na kuzichukia sheria zangu, tena mkishindwa kutimiza amri zangu na hivyo mkavunja agano langu, 26:16 Kum 28:22, 35; Za 78:33; 107:17; 1Sam 2:33; Eze 4:17; 24:23; 33:10; Amu 6:3-6; Ay 31:8ndipo nitakapowafanyia hili: Nitawaletea juu yenu hofu ya ghafula, magonjwa ya kufisha, na homa itakayopofusha macho yenu na kuwaondolea uhai wenu. Mtapanda mbegu bila mafanikio, kwa sababu adui zenu wataila. 26:17 Law 17:10; Eze 15:7; Kum 28:7, 25, 48; Yos 7:4, 12; Amu 2:15; 1Fal 8:33; 2Nya 6:24; Yer 9:17; 21:7; Za 106:41; 53:5; Mit 28:1; Isa 30:17Nitauelekeza uso wangu dhidi yenu ili mshindwe na adui zenu; wale wanaowachukia watawatawala, nanyi mtakimbia ingawa hakuna mtu anayewafukuza.

26:18 Za 99:8; Yer 21:14; Amo 3:14“ ‘Kama baada ya haya yote hamtanisikiliza, nitawaadhibu mara saba zaidi kwa ajili ya dhambi zenu. 26:19 Za 10:4; 73:6; Isa 16:6; 25:11; 28:1-3; Yer 13:9; 48:29; Eze 24:21; Amo 6:8; Sef 3:11; Kum 28:23; Ay 28:28Nitakivunja kiburi chenu cha ukaidi na kuifanya anga iliyo juu yenu iwe kama chuma, na ardhi yenu kama shaba. 26:20 Kum 11:17; 28:24, 38; Za 127:1; Isa 17:11; 49:4; Yer 12:13; Mik 6:15; Hag 1:6Nguvu zenu zitatumika bila ya mafanikio, kwa sababu ardhi yenu haitawazalia mazao yake, wala miti ya nchi yenu haitazaa matunda yake.

26:21 Mwa 4:15“ ‘Kama mtaendelea kuwa na uadui nami, na kukataa kunisikiliza, nitawazidishia mateso yenu mara saba zaidi, kama dhambi zenu zinavyostahili. 26:22 Mwa 37:20; Kum 28:62; Yer 42:2; 5:6; 14:16; 15:3; 16:4; Eze 14:15Nitawatuma wanyama mwitu dhidi yenu, nao watawaibieni watoto wenu, watawaangamiza ngʼombe wenu, na kuifanya idadi yenu kuwa ndogo, hivi kwamba barabara zenu zitakuwa hazina watu.

26:23 Yer 2:30; 5:3; 7:28; 17:23; 32:33; Sef 3:2“ ‘Ikiwa pamoja na mambo haya hamtakubali maonyo yangu lakini mkaendelea kuweka uadui nami, 26:24 2Sam 22:27mimi mwenyewe nitaweka uadui nanyi, na kuwatesa kwa ajili ya dhambi zenu mara saba zaidi. 26:25 Yer 5:17; 15:3; 47:6; 50:28; 51:6, 11; Eze 11:8; 14:17; 21:4; 33:2; Kut 5:3; 9:3; Hes 16:46; 1Fal 8:37; Hab 3:5Nitawaletea upanga juu yenu ili kuwapatiliza kwa kuvunja Agano langu. Mtakapokimbilia mijini mwenu, nitatuma tauni katikati yenu, nanyi mtatiwa mikononi mwa adui zenu. 26:26 1Fal 8:37; 18:2; 2Fal 4:38; 6:25; 25:3; Za 105:16; Isa 3:1; 9:20; Yer 37:21; 52:6; Eze 4:16-17; 5:16; 14:13; Hos 4:10; Mik 6:14Nitakapowaondolea upatikanaji wa mkate wenu, wanawake kumi wataoka mkate wenu katika tanuru moja, nao wataugawa mkate kidogo kwa kupima. Mtakula, lakini hamtashiba.

“ ‘Kama hata baada ya haya bado hamtanisikiliza lakini mkaendelea kuweka uadui nami, 26:28 Kum 32:19; Amu 2:14; Za 78:59; 106:40; Kum 7:10; Ay 34:11; Isa 59:18; 65:5-7; 66:6; Yer 17:10; 25:29; Yoe 3:4ndipo katika hasira yangu nitaweka uadui nanyi, nami mwenyewe nitawaadhibu mara saba kwa ajili ya dhambi zenu. 26:29 2Fal 6:29; Yer 19:6; Mao 4:10; Eze 5:10; Kum 28:53Mtakula nyama ya wana wenu na nyama ya binti zenu. 26:30 Kum 12:2; 1Sam 9:12; 10:5; 1Fal 3:2, 4; 12:31; 13:2, 32; 2Fal 17:29; 23:20; 2Nya 34:3, 4; Za 78:58; 106:40; Eze 6:3, 6, 13; 16:16; Amo 6:8; 7:9; Isa 17:8; 27:9; 21:9; Yer 50:2Nitapaharibu mahali penu pa juu pa kuabudia miungu, nibomoe madhabahu zenu za kufukizia uvumba, na kuzilundika maiti zenu juu ya sanamu zenu zisizo na uhai, nami nitawachukia ninyi sana. 26:31 Neh 1:3; Isa 1:7; 3:8, 26; 6:11; 24:12; 61:4; 63:18; 64:11; Yer 4:7; 9:11; 25:11; 34:22; 44:2-6, 22; Eze 36:33; 24:21; Mik 2:4; 3:12; Sef 2:5; 3:6; 2Fal 22:19; Za 74:3-7; Mao 2:7; Amo 7:9; 5:21; 8:10Nitaifanya miji yenu kuwa magofu, na kuharibu mahali patakatifu penu pa kuabudia, nami sitapendezwa na harufu nzuri ya sadaka zenu. 26:32 Isa 5:6; 52:14; Yer 9:11; 12:11; 25:11; 26:9; 33:10; 34:22; 44:22; 18:16; 19:8; 48:39; 1Fal 9:8; 2Nya 29:8; Eze 5:14; 26:16; 27:35; 28:19Nitaiharibu nchi, ili adui zenu watakaokuja kuishi humo washangae. 26:33 Yer 4:11; 7:34; 9:16; 13:24; 31:10; 40:3, 15; 50:17; 42:16; Eze 5:10; 12:15; 17:21; 20:23; 22:15; 34:6; Yoe 3:2; Kum 4:27; 28:64; Neh 1:8; Za 44:11; 106:27; Zek 7:14; Amo 9:4; Isa 49:19; 1Sam 15:22; Ay 36:11Nitawatawanya ninyi miongoni mwa mataifa, na kuufuta upanga wangu na kuwafuatia. Nchi yenu itaharibiwa, nayo miji yenu itakuwa magofu. 26:34 Isa 1:7; Yer 7:34; 25:11; 44:6; Eze 33:29; 2Nya 36:21Ndipo nchi itafurahia Sabato zake muda wote ule itakapokuwa ukiwa, nanyi mkiwa katika nchi ya adui zenu. Ndipo nchi itapumzika na kufurahia Sabato zake. 26:35 Law 25:4Wakati wote nchi itakapobaki ukiwa, itapumzika na kufurahia Sabato zake ambazo haikuzipata mlipokuwa mnaishi humo.

26:36 Ay 13:25; 2Fal 25:5; Za 58:7; Mao 1:3-6; 4:19; Eze 21:7“ ‘Kwa habari ya wenzenu wale watakaobaki, nitaifanya mioyo yao kuwa na hofu kuu katika nchi za adui zao, kiasi kwamba sauti ya jani linalopeperushwa na upepo itawafanya wakimbie. Watakimbia kana kwamba wanakimbia upanga, nao wataanguka, ingawa hakuna anayewafukuza. 26:37 Yer 6:21; 13:16; 46:16; Eze 3:20; Nah 3:3; Yos 7:12Watajikwaa mmoja juu ya mwingine kama wakimbiao upanga, hata ingawa hakuna anayewafuatia. Hivyo hamtaweza kusimama mbele ya adui zenu. 26:38 Ay 4:9; 36:12; Isa 1:28; Yer 16:4; 44:27; Kum 4:26Mtaangamia katikati ya mataifa; nchi ya adui zenu itawala. 26:39 Kut 20:5; Isa 14:21; 24:16; Eze 4:17Wale wenu watakaobaki wataangamia katika nchi za adui zao kwa sababu ya dhambi zao; pia kwa sababu ya dhambi za baba zao wataangamia.

26:40 Law 5:5; Za 32:5; 38:18; 106:6; Neh 9:2; Yer 3:12-15; 14:20; Hos 5:15; Lk 15:18; 1Yn 1:9“ ‘Lakini kama watatubu dhambi zao na dhambi za baba zao, udanganyifu wao dhidi yangu na uadui wao kwangu, 26:41 Kum 10:16; 4:31; 30:6; Yer 4:4; 9:25-26; 4:27; 5:10; 30:11; 31:37; 33:26; 51:5; Eze 20:43; 44:7-9; Mdo 7:51; 2Nya 7:14; 12:6; Isa 6:7; 33:24; 40:2; 53:6-11; Amu 2:1ambao ulinifanya niwe na uadui nao hata nikawapeleka katika nchi ya adui zao, wakati mioyo yao isiyotahiriwa itanyenyekea na kutubu dhambi yao, 26:42 Za 69:25; 106:24; Isa 6:11; 32:14; 62:4; Yer 2:15; 44:2; Eze 20:13; 36:4; Hes 11:20; 14:31; 1Sam 8:7nami nitakumbuka agano langu na Yakobo, na agano langu na Isaki, na agano langu na Abrahamu, nami nitaikumbuka nchi. Kwa kuwa wataiacha nchi ukiwa, nayo itafurahia Sabato zake wakati itakuwa ukiwa bila wao. Wataadhibiwa kwa ajili ya dhambi zao, kwa sababu walizikataa sheria zangu na kuzichukia amri zangu. 26:44 2Fal 17:20; 25:11; 2Nya 6:36; 36:20; Rum 11:2; Kut 6:8; Law 25:38Lakini pamoja na hili, wakati watakuwa katika nchi ya adui zao, sitawakataa wala kuwachukia kiasi cha kuwaharibu kabisa na kuvunja agano langu nao. Mimi ndimi Bwana Mungu wao. 26:45 Kum 4:31Lakini kwa ajili yao nitalikumbuka agano langu na baba zao, ambao niliwatoa Misri mbele ya mataifa ili niwe Mungu wao. Mimi ndimi Bwana.’ ”

26:46 Kut 19:11; Law 7:38; 27:34Hizi ndizo amri, sheria na pia masharti ambazo Bwana alifanya kati yake mwenyewe na Waisraeli katika Mlima Sinai kupitia kwa Mose.

Read More of Walawi 26

Walawi 27:1-34

Kukomboa Kile Kilicho Cha Bwana

Bwana akamwambia Mose, 27:2 Mwa 28:20; Hes 6:2; Kum 23:21-23; Amu 11:30-39; Ay 22:27; Yn 1:16; Mdo 21:23“Sema na Waisraeli uwaambie: ‘Kama mtu yeyote ataweka nadhiri maalum ili kuweka watu wakfu kwa Bwana, kwa kutoa kiasi cha thamani inayolingana, 27:3 Kut 30:13; Hes 3:47; 18:16; Eze 45:12thamani ya kukomboa mwanaume mwenye kati ya umri wa miaka ishirini na miaka sitini itakuwa shekeli hamsini27:3 Shekeli 50 za fedha ni sawa na gramu 600. za fedha, kulingana na shekeli ya mahali patakatifu; ikiwa ni mwanamke, weka thamani yake kwa shekeli thelathini.27:4 Shekeli 30 za fedha ni sawa na gramu 360. 27:5 Mwa 37:28Kama ni mtu mwenye umri wa miaka kati ya mitano na ishirini, weka thamani ya mwanaume kuwa shekeli ishirini,27:5 Shekeli 20 za fedha ni sawa na gramu 240. na mwanamke shekeli kumi.27:5 Shekeli 10 za fedha ni sawa na gramu 120. 27:6 Hes 3:47; 18:16Kama ni mtu mwenye umri kati ya mwezi mmoja na miaka mitano, weka thamani ya mwanaume kuwa shekeli tano za fedha, na ile ya mwanamke kuwa shekeli tatu27:6 Shekeli tatu za fedha ni sawa na gramu 36. za fedha. Kama ni mtu mwenye miaka sitini na zaidi, weka thamani ya mwanaume kuwa shekeli kumi na tano,27:7 Shekeli 15 za fedha ni sawa na gramu 180. na mwanamke shekeli kumi. 27:8 Law 5:11; 12:8; 14:21-22; Lk 21:1; 2Kor 8:12Kama mtu yeyote anayeweka nadhiri ni maskini mno kuweza kulipa kiasi kilichowekwa, atampeleka huyo mtu kwa kuhani, ambaye ataweka thamani yake kulingana na kile mweka nadhiri anachoweza kulipa.

27:9 Mwa 28:20; Kut 40:9; Hes 6:20; 18:17; Kum 15:19“ ‘Kama kile mtu alichokiwekea nadhiri ni mnyama anayekubalika kama sadaka kwa Bwana, mnyama wa namna hiyo aliyetolewa kwa Bwana anakuwa mtakatifu. Mtu haruhusiwi kumbadilisha au kutoa mnyama mzuri kwa mbaya, au mnyama mbaya kwa mzuri. Kama atatoa mnyama badala ya mwingine, wanyama wote wawili, yaani yule aliyetolewa na yule aliyebadiliwa, ni watakatifu. 27:11 Kut 13:13; Hes 18:15Kama alichokiwekea nadhiri ni mnyama aliye najisi kiibada, yaani yule asiye kubalika kuwa sadaka kwa Bwana, huyo mnyama lazima aletwe kwa kuhani, ambaye ataamua ubora wa mnyama huyo, kama ni mzuri au mbaya. Thamani yoyote atakayoweka kuhani, hivyo ndivyo itakavyokuwa. 27:13 Law 25:25; 5:16Kama mwenye mnyama atapenda kumkomboa mnyama huyo, lazima aongeze sehemu ya tano ya thamani yake.

27:14 Law 25:29-31; Hes 18:14; 2Kor 9:10“ ‘Kama mtu ataweka nyumba yake wakfu kama kitu kitakatifu kwa Bwana, kuhani ataamua ubora wa nyumba hiyo, kama ni nzuri au mbaya. Thamani yoyote kuhani atakayoweka, basi hivyo ndivyo itakavyokuwa. Kama mtu aliyeweka nyumba yake wakfu ataikomboa, lazima aongeze sehemu ya tano ya thamani yake, nayo nyumba itakuwa yake tena.

“ ‘Kama mtu anaweka sehemu ya ardhi ya jamaa yake wakfu kwa Bwana, thamani yake itawekwa kulingana na kiasi cha mbegu inayohitajiwa kupandwa katika ardhi hiyo, yaani homeri27:16 Homeri moja ni sawa na efa 10, ambazo ni sawa na kilo 100. moja ya mbegu za shayiri kwa shekeli hamsini za fedha. Kama akiweka shamba lake wakfu katika Mwaka wa Yubile, ile thamani iliyokwisha wekwa itakuwa iyo hiyo. 27:18 Law 25:10-15; 25:15-16Lakini kama akiweka shamba lake wakfu baada ya Yubile, kuhani ataweka thamani kulingana na idadi ya miaka iliyobaki kufikia Mwaka wa Yubile unaofuata, na thamani yake iliyoamuliwa itapunguzwa. 27:19 Law 25:25Kama mtu anayeweka wakfu shamba anataka kulikomboa, lazima aongeze sehemu ya tano ya thamani yake, nalo shamba litakuwa lake tena. Kama pengine halikomboi shamba hilo, au kama ameliuza kwa mtu mwingine, kamwe haliwezi kukombolewa. 27:21 Law 25:10; Hes 18:14; Eze 44:29Shamba hilo litakapoachiwa mwaka wa Yubile, litakuwa takatifu, kama shamba lililotolewa kwa Bwana, nalo litakuwa mali ya makuhani.

“ ‘Kama mtu ameweka wakfu kwa Bwana shamba alilonunua, ambalo si sehemu ya ardhi ya jamaa yake, 27:23 Law 25:15kuhani ataamua thamani yake hadi Mwaka wa Yubile, naye huyo mtu atalazimika kulipa thamani yake siku hiyo kama kitu kitakatifu kwa Bwana. 27:24 Law 25:28Katika Mwaka wa Yubile, shamba litarudishwa kwa mtu yule ambaye lilinunuliwa kutoka kwake, yule ambaye ardhi ilikuwa mali yake. 27:25 Kut 30:13; Hes 3:47; Eze 45:12; Hes 18:16Kila thamani lazima iwekwe kulingana na shekeli ya mahali patakatifu,27:25 Shekeli moja ya mahali patakatifu ni sawa na gramu 11. gera ishirini kwa shekeli.

27:26 Kut 13:12; 22:30; Hes 18:17; Kut 15:19“ ‘Lakini hakuna mtu atakayeweka wakfu mzaliwa wa kwanza wa mnyama, kwa kuwa mzaliwa wa kwanza tayari ni mali ya Bwana; awe ngʼombe au kondoo, ni wa Bwana. Kama ni mmoja wa wanyama walio najisi, aweza kumnunua kwa bei iliyowekwa, akiongeza sehemu ya tano ya thamani yake. Kama hatamkomboa, mnyama huyo atauzwa kwa bei iliyowekwa.

27:28 Hes 18:14; Yos 6:17-19; Amu 11:30-31“ ‘Lakini chochote kile mtu alicho nacho na akakiweka wakfu27:28 Akakiweka wakfu ina maana ya kumpa Mungu kabisa, daima, bila kurudiwa. kwa Bwana, iwe ni binadamu, au mnyama, au ardhi ya jamaa, hakiwezi kuuzwa au kukombolewa. Chochote kilichowekwa wakfu ni kitakatifu sana kwa Bwana.

27:29 Kum 7:26“ ‘Mtu yeyote aliyewekwa wakfu ili kuangamizwa, hawezi kukombolewa. Mtu kama huyo lazima auawe.

27:30 Hes 18:26; Kum 7:6; 12:6, 17; 14:22-28; 2Nya 31:6; Neh 10:37; 12:44; 13:5; Mal 3:8; Ezr 9:2; Isa 6:13“ ‘Zaka ya kila kitu kutoka shambani, iwe ni nafaka kutoka kwa ardhi, au tunda kutoka kwa miti, ni mali ya Bwana; ni takatifu kwa Bwana. 27:31 Law 25:25; 5:16Kama mtu akikomboa chochote cha zaka yake, lazima aongeze sehemu ya tano ya thamani yake. 27:32 Za 89:32; Yer 33:13; Eze 20:37; Mik 7:14Zaka yote ya kundi la ngʼombe au la kondoo na mbuzi, kila mnyama wa kumi apitaye chini ya fimbo ya yule awachungaye, atakuwa mtakatifu kwa Bwana. 27:33 Hes 18:21Yule mnyama wa kumi hatachaguliwa kwa kigezo cha uzuri au ubaya, naye haruhusiwi kubadiliwa. Ikiwa atabadiliwa, basi mnyama yule wa kwanza na huyo aliyebadiliwa wote watahesabiwa kuwa watakatifu, na haiwezekani kuwakomboa.’ ”

27:34 Kut 19:11; Law 7:38; Kum 4:5; Mdo 7:38Haya ndiyo maagizo Bwana aliyompa Mose juu ya Mlima Sinai kwa ajili ya Waisraeli.

Read More of Walawi 27