Yohana 4:43-54, Yohana 5:1-15 NEN

Yohana 4:43-54

Yesu Amponya Mwana Wa Afisa

Baada ya zile siku mbili, Yesu aliondoka kwenda Galilaya. 4:44 Mt 13:57; Lk 4:24(Basi Yesu mwenyewe alikuwa amesema kwamba nabii hapati heshima katika nchi yake mwenyewe.) 4:45 Yn 2:23Alipofika Galilaya, Wagalilaya walimkaribisha, kwani walikuwa wameona yale aliyoyatenda huko Yerusalemu wakati wa Sikukuu ya Pasaka. Kwa maana wao pia walikuwa wamehudhuria hiyo Sikukuu.

4:46 Yn 21:1-11Hivyo Yesu akaja tena mpaka Kana ya Galilaya, kule alikokuwa amebadili maji kuwa divai. Huko kulikuwepo na afisa mmoja wa mfalme, ambaye mwanawe alikuwa mgonjwa huko Kapernaumu. 4:47 Yn 4:3, 54; Lk 7:2Huyo mtu aliposikia kwamba Yesu alikuwa amewasili Galilaya kutoka Uyahudi, alimwendea na kumwomba ili aje kumponya mwanawe, aliyekuwa mgonjwa karibu ya kufa.

4:48 Dan 4:2-3; Ebr 2:4Yesu akamwambia, “Ninyi watu msipoona ishara na miujiza kamwe hamtaamini.”

Yule afisa wa mfalme akamwambia, “Bwana, tafadhali shuka kabla mwanangu hajafa.”

Yesu akamjibu, “Enenda zako, mwanao yu hai.”

Yule afisa akaamini yale maneno Yesu aliyomwambia, akaondoka akaenda zake. Alipokuwa bado yuko njiani, akakutana na watumishi wake wakamwambia kwamba mwanawe yu mzima. Akawauliza saa ambayo alianza kupata nafuu. Wakamwambia, “Jana yapata saa saba, homa ilimwacha.”

4:53 Mdo 11:14Ndipo baba wa huyo mtoto akakumbuka kuwa huo ndio wakati ambapo Yesu alikuwa amemwambia, “Mwanao yu hai.” Kwa hiyo yeye pamoja na wote wa nyumbani mwake wakamwamini Yesu.

4:54 Yn 4:8; 2:11Hii ilikuwa ishara ya pili ambayo Yesu alifanya aliporudi Galilaya kutoka Uyahudi.

Read More of Yohana 4

Yohana 5:1-15

Yesu Amponya Mtu Kwenye Bwawa La Bethzatha

5:1 Law 23:2; Kum 16:1; Yn 2:13Baada ya haya, kulikuwa na Sikukuu ya Wayahudi, naye Yesu akapanda kwenda Yerusalemu. 5:2 Neh 3:1; 12:39; Mdo 21:40; 26:14Huko Yerusalemu, karibu na mlango uitwao Mlango wa Kondoo, palikuwa na bwawa moja lililoitwa kwa Kiebrania Bethzatha,5:2 Bethzatha ni neno la Kiebrania ambalo maana yake ni Nyumba ya mizeituni; mahali pengine limetajwa kama Bethesda kwa Kiaramu, yaani Nyumba ya huruma, na pengine kama Bethsaida, yaani Nyumba ya uvuvi. ambalo lilikuwa limezungukwa na kumbi tano. Hapa palikuwa na idadi kubwa ya wasiojiweza, yaani, vipofu, viwete, na waliopooza [wakingojea maji yatibuliwe. Kwa maana malaika alikuwa akishuka wakati fulani, akayatibua maji. Yule aliyekuwa wa kwanza kuingia ndani baada ya maji kutibuliwa alipona ugonjwa wowote aliokuwa nao]. Mtu mmoja alikuwako huko ambaye alikuwa ameugua kwa miaka thelathini na minane. Yesu alipomwona akiwa amelala hapo, naye akijua kuwa amekuwa hapo kwa muda mrefu, akamwambia, “Je, wataka kuponywa?”

Yule mgonjwa akamjibu, “Bwana, mimi sina mtu wa kuniingiza bwawani maji yanapotibuliwa. Nami ninapotaka kutumbukia bwawani, mtu mwingine huingia kabla yangu.”

5:8 Mk 2:11; Lk 5:24Yesu akamwambia, “Inuka! Chukua mkeka wako na uende.” 5:9 Mt 12:1-14; Yn 9:14Mara yule mtu akapona, akachukua mkeka wake, akaanza kutembea.

Basi siku hiyo ilikuwa siku ya Sabato. 5:10 Yer 17:21; Mt 12:2Kwa hiyo Wayahudi wakamwambia yule mtu aliyeponywa, “Leo ni Sabato, si halali wewe kubeba mkeka wako.”

Yeye akawajibu, “Yule mtu aliyeniponya aliniambia, ‘Chukua mkeka wako na uende.’ ”

5:12 Lk 5:21Wakamuuliza, “Ni mtu gani huyo aliyekuambia uchukue mkeka wako uende?”

Basi yule mtu aliyeponywa hakufahamu ni nani aliyemponya, kwa sababu Yesu alikuwa amejiondoa katika ule umati wa watu uliokuwa hapo.

5:14 Mk 2:5; Yn 8:11; 8:11Baadaye Yesu akamkuta yule mtu aliyemponya ndani ya Hekalu na kumwambia, “Tazama umeponywa, usitende dhambi tena. La sivyo, lisije likakupata jambo baya zaidi.” 5:15 Yn 1:19Yule mtu akaenda, akawaambia wale Wayahudi kuwa ni Yesu aliyemponya.

Read More of Yohana 5