Yohana 4:1-26 NEN

Yohana 4:1-26

Yesu Azungumza Na Mwanamke Msamaria

4:1 Yn 3:22-26Mafarisayo wakasikia kwamba Yesu alikuwa anapata na kubatiza wanafunzi wengi zaidi kuliko Yohana, 4:2 1Kor 1:17ingawa kwa kweli si Yesu mwenyewe aliyekuwa akibatiza, ila ni wanafunzi wake. 4:3 Yn 3:22Bwana alipojua mambo haya, aliondoka Uyahudi akarudi tena Galilaya.

4:4 Lk 9:52Wakati huo ilimlazimu apitie Samaria. 4:5 Mwa 48:22; Yos 24:32Akafika kwenye mji mmoja wa Samaria uitwao Sikari, karibu na lile shamba ambalo Yakobo alimpa mwanawe Yosefu. Huko ndiko kulikokuwa na kile kisima cha Yakobo. Naye Yesu alikuwa amechoka kwa kuwa alikuwa ametoka safarini. Akaketi karibu na hicho kisima. Ilikuwa yapata saa sita mchana.

4:7 Mwa 24:17; 1Fal 17:10Mwanamke mmoja Msamaria akaja kuteka maji, Yesu akamwambia, “Naomba maji ninywe.” 4:8 Yn 4:5, 30(Wakati huo wanafunzi wake walikuwa wamekwenda mjini kununua chakula.)

4:9 Mt 10:5; Lk 9:52-53Yule mwanamke Msamaria akamjibu, “Wewe ni Myahudi na mimi ni Msamaria. Yawezekanaje uniombe nikupe maji ya kunywa?” (Wayahudi walikuwa hawashirikiani kabisa na Wasamaria.)

4:10 Isa 55:1; Ufu 21:6Yesu akajibu akamwambia, “Kama ungelijua karama ya Mungu, naye ni nani anayekuambia, Nipe maji ninywe, wewe ungelimwomba yeye, naye angelikupa maji yaliyo hai.”

Yule mwanamke akamjibu, “Bwana, wewe huna chombo cha kutekea maji na kisima hiki ni kirefu. Hayo maji ya uzima utayapata wapi? 4:12 Yn 4:6; 8:53Kwani wewe ni mkuu kuliko baba yetu Yakobo ambaye alitupatia kisima hiki, ambacho yeye pamoja na watoto wake na mifugo yake walikitumia?”

4:13 Yn 6:58Yesu akamjibu, “Kila mtu anayekunywa maji ya kisima hiki ataona kiu tena. 4:14 Yn 6:35; Isa 12:3; Yn 7:38; Mt 25:46Lakini yeyote anywaye maji nitakayompa hataona kiu kamwe. Maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujika uzima wa milele.”

4:15 Yn 6:34Yule mwanamke akamwambia, “Bwana, tafadhali nipe maji hayo ili nisipate kiu tena na wala nisije tena hapa kuteka maji!”

Yesu akamjibu, “Nenda ukamwite mumeo, uje naye hapa.”

Yule mwanamke akajibu, “Sina mume.”

Yesu akamwambia, “Umesema kweli kuwa huna mume. Kwa maana umeshakuwa na wanaume watano na mwanaume unayeishi naye sasa si mume wako! Umesema ukweli.”

4:19 Mt 21:11Yule mwanamke akasema, “Bwana, naona bila shaka wewe ni nabii. 4:20 Kum 11:29; Yos 8:33; Lk 9:53; 4:21; 4:20; Yn 5:28; 16:2; 1Tim 2:8Baba zetu waliabudu kwenye mlima huu, lakini ninyi Wayahudi mnasema ni lazima tukaabudu huko Yerusalemu.”

4:21 Yn 5:28; 16:2; Mal 1:11; 1Tim 2:8Yesu akamjibu, “Mwanamke, niamini, wakati unakuja ambapo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala huko Yerusalemu. 4:22 2Fal 17:28-41; Isa 2:3; Rum 9:4-5Ninyi Wasamaria mnaabudu msichokijua. Sisi Wayahudi tunamwabudu Mungu tunayemjua kwa sababu wokovu unatoka kwa Wayahudi. 4:23 Yn 5:25; 16:32; Flp 3:3Lakini saa yaja, tena ipo, ambapo wale waabuduo halisi, watamwabudu Baba katika roho na kweli. Watu wanaoabudu namna hii, ndio Baba anawatafuta. 4:24 Flp 3:3Mungu ni Roho na wote wanaomwabudu imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.”

4:25 Mt 1:16; Yn 1:41Yule mwanamke akamwambia, “Ninafahamu kwamba Masiya (aitwaye Kristo) anakuja. Yeye akija, atatueleza mambo yote.”

4:26 Yn 8:24; 9:35-37Yesu akamwambia, “Mimi ninayezungumza nawe, ndiye.”

Read More of Yohana 4