Yohana 18:25-40 NEN

Yohana 18:25-40

Petro Amkana Yesu Tena

(Mathayo 26:71-75; Marko 14:69-72; Luka 22:58-62)

18:25 Yn 18:18; 18:17; Mt 26:69, 71; Mk 14:69; Lk 22:58Wakati huo Simoni Petro alikuwa amesimama akiota moto. Baadhi ya wale waliokuwepo wakamuuliza, “Je, wewe si mmoja wa wanafunzi wake?”

Petro akakana, akasema, “Sio mimi.”

18:26 Yn 18:1; 10Mmoja wa watumishi wa kuhani mkuu, ndugu yake yule mtu ambaye Petro alikuwa amemkata sikio, akamuuliza, “Je, mimi sikukuona kule bustanini ukiwa na Yesu?” 18:27 Yn 13:38Kwa mara nyingine tena Petro akakana, naye jogoo akawika wakati huo huo.

Yesu Apelekwa Kwa Pilato

(Mathayo 27:1-2, 11-14; Marko 15:1-5; Luka 23:1-5)

18:28 Mt 27:2; Yn 18:33; 19:9; 11:55Ndipo Wayahudi wakamchukua Yesu kutoka kwa Kayafa na kumpeleka kwenye jumba la kifalme la mtawala wa Kirumi.18:28 Jumba la mfalme la mtawala wa Kirumi lilikuwa linaitwa Praitorio. Wakati huo ilikuwa ni alfajiri, ili kuepuka kuwa najisi kwa taratibu za ibada, Wayahudi hawakuingia ndani kwa sababu ya sheria za Kiyahudi. Wangehesabiwa kuwa najisi kama wangeingia nyumbani mwa mtu asiye Myahudi na wasingeruhusiwa kushiriki katika Sikukuu ya Pasaka. Hivyo Pilato akatoka nje walikokuwa akawauliza, “Mmeleta mashtaka gani kumhusu mtu huyu?”

Wao wakamjibu, “Kama huyu mtu hakuwa mhalifu tusingemleta kwako.”

Pilato akawaambia, “Basi mchukueni ninyi mkamhukumu kwa kufuata sheria zenu.”

Wayahudi wakamjibu, “Sisi haturuhusiwi kutoa hukumu ya kifo kwa mtu yeyote.” 18:32 Mt 20:19; 26:2Walisema hivyo ili yale maneno aliyosema Yesu kuhusu kifo atakachokufa yapate kutimia.

18:33 Mt 27:11; Yn 19:9; Lk 23:3; Mt 2:2Kwa hiyo Pilato akaingia ndani ya jumba la kifalme, akamwita Yesu, akamuuliza, “Wewe ndiye mfalme wa Wayahudi?”

18:34 Mt 16:13Yesu akamjibu, “Je, unauliza swali hili kutokana na mawazo yako mwenyewe, au uliambiwa na watu kunihusu mimi?”

18:35 Yn 1:11; Mt 21:39Pilato akamjibu, “Mimi si Myahudi, ama sivyo? Taifa lako mwenyewe na viongozi wa makuhani wamekukabidhi kwangu. Umefanya kosa gani?”

18:36 Mt 3:2; 26:53; Lk 17:21; Yn 6:51Yesu akajibu, “Ufalme wangu si wa ulimwengu huu. Ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu, wafuasi wangu wangenipigania ili nisitiwe mikononi mwa Wayahudi. Lakini kama ilivyo, ufalme wangu hautoki hapa ulimwenguni.”

18:37 Yn 3:32; 8:47; 1Yn 4:6Pilato akamuuliza, “Kwa hiyo wewe ni mfalme?” Yesu akajibu, “Wewe wasema kwamba mimi ni mfalme. Kwa kusudi hili nilizaliwa, na kwa ajili ya hili nilikuja ulimwenguni, ili niishuhudie kweli. Mtu yeyote aliye wa kweli husikia sauti yangu.”

18:38 Lk 23:4-6Pilato akamuuliza Yesu, “Kweli ni nini?” Baada ya kusema haya Pilato akaenda nje tena akawaambia wale viongozi wa Wayahudi waliomshtaki Yesu, “Sioni kosa lolote alilotenda mtu huyu. 18:39 Mt 27:15; Mk 15:6; Lk 23:19Lakini ninyi mna desturi yenu kwamba wakati wa Pasaka nimwachie huru mfungwa mmoja mnayemtaka. Je, mnataka niwafungulie huyu ‘Mfalme wa Wayahudi’?”

18:40 Mdo 3:14Wao wakapiga kelele wakisema, “Si huyu mtu, bali tufungulie Baraba!” Yule Baraba alikuwa mnyangʼanyi.

Read More of Yohana 18