Yohana 10:22-42 NEN

Yohana 10:22-42

Yesu Akataliwa Na Wayahudi

Wakati huo ilikuwa Sikukuu ya Kuwekwa wakfu kwa Hekalu10:22 Sikukuu ya Kuwekwa wakfu kwa Hekalu ni Hanukkah kwa Kiebrania. huko Yerusalemu, nao ulikuwa wakati wa majira ya baridi. 10:23 Mdo 3:11; 5:12Naye Yesu alikuwa akitembea ndani ya Hekalu katika ukumbi wa Solomoni. 10:24 Yn 1:19; Lk 22:67Wayahudi wakamkusanyikia wakamuuliza, “Utatuweka katika hali ya mashaka mpaka lini? Kama wewe ndiye Kristo10:24 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta. tuambie waziwazi.”

10:25 Yn 4:26; 4:11Yesu akawajibu, “Nimewaambia, lakini hamwamini. Mambo ninayoyatenda kwa jina la Baba yangu yananishuhudia. 10:26 Yn 8:47Lakini hamwamini, kwa sababu ninyi si wa kundi la kondoo wangu. 10:27 Yn 10:4, 14Kondoo wangu huisikia sauti yangu nami nawajua, nao hunifuata, 10:28 Yn 6:39nami ninawapa uzima wa milele, hawataangamia kamwe wala hakuna mtu atakayewapokonya kutoka mikono yangu. 10:29 Yn 17:2, 6, 24; 14:28Baba yangu aliyenipa hawa ni mkuu kuliko wote na hakuna awezaye kuwapokonya kutoka mikononi mwake. 10:30 Kum 6:4; Yn 17:21-24Mimi na Baba yangu tu umoja.”

10:31 Yn 8:59Kwa mara nyingine Wayahudi wakainua mawe ili wampige nayo, lakini Yesu akawaambia, “Nimewaonyesha miujiza mingi mikubwa kutoka kwa Baba yangu. Ni ipi katika hiyo mnataka kunipiga mawe?”

10:33 Law 24:16; Mt 26:63-66Wayahudi wakamjibu, “Hatukupigi mawe kwa sababu ya mambo mema uliyotenda, bali ni kwa kuwa umekufuru. Wewe ingawa ni mwanadamu unajifanya kuwa Mungu.”

10:34 Rum 3:19; 1Kor 14:21; Za 82:6Yesu akawajibu, “Je, haikuandikwa katika Sheria ya kwamba, ‘Nimesema kuwa, ninyi ni miungu?’ 10:35 Rum 13:1; Mt 5:17, 18Kama aliwaita ‘miungu,’ wale ambao neno la Mungu liliwafikia, nayo Maandiko hayawezi kutanguka, 10:36 Yer 1:5; Yn 6:69; 3:17je, mwawezaje kusema kwamba yule ambaye Baba amemweka wakfu na kumtuma ulimwenguni anakufuru, kwa sababu nilisema, ‘Mimi ni Mwana wa Mungu?’ 10:37 Yn 15:24Ikiwa sifanyi kazi za Baba yangu, basi msiniamini, 10:38 Yn 14:10-11; 20:17-21lakini ikiwa nazifanya kazi za Mungu, hata kama hamniamini mimi ziaminini hizo kazi, ili mpate kujua na kuelewa kwamba Baba yu ndani yangu, nami ndani yake.” 10:39 Yn 7:30; Lk 4:30; Yn 8:59Ndipo wakajaribu kumkamata kwa mara nyingine, lakini akaponyoka kutoka mikononi mwao.

10:40 Yn 1:28Akaenda tena ngʼambo ya Mto Yordani mpaka mahali pale ambapo Yohana alikuwa akibatiza hapo awali, naye akakaa huko. 10:41 Yn 2:1; 1:26-34Watu wengi wakamjia, nao wakawa wakisema, “Yohana hakufanya muujiza wowote, lakini kila jambo alilosema kumhusu huyu mtu ni kweli.” 10:42 Yn 7:31Nao wengi wakamwamini Yesu huko.

Read More of Yohana 10