Yoeli 2:18-32, Yoeli 3:1-21 NEN

Yoeli 2:18-32

Jibu La Bwana

2:18 Isa 26:11; 42:13; Zek 8:2; 1:14; Kum 32:36; Za 103:13; 72:13Kisha Bwana atakuwa na wivu kwa ajili ya nchi yake

na kuwa na huruma juu ya watu wake.

2:19 Yer 31:12; Eze 34:29; Za 4:7; Law 26:5Bwana atawajibu:

“Ninawapelekea nafaka,

mvinyo mpya na mafuta,

vya kuwatosha ninyi

hadi mridhike kabisa;

kamwe sitawafanya tena

kitu cha kudharauliwa na mataifa.

2:20 Yer 1:14-15; Zek 14:8; Kum 11:24; Kut 10:19; Isa 34:3“Nitafukuza jeshi la kaskazini likae mbali nanyi,

nikilisukuma ndani ya jangwa,

askari wa safu za mbele wakienda

ndani ya bahari ya mashariki

na wale wa safu za nyuma

katika bahari ya magharibi.

Uvundo wake utapaa juu;

harufu yake itapanda juu.”

Hakika ametenda mambo makubwa.

2:21 Sef 3:16-17; Isa 25:1; 29:22; 54:4; 1Yn 4:18Usiogope, ee nchi;

furahi na kushangilia.

Hakika Bwana ametenda mambo makubwa.

2:22 Yoe 1:18-20; Zek 8:12; Za 65:12; Hes 16:14; 1Fal 4:25Msiogope, enyi wanyama pori,

kwa kuwa mbuga za malisho yenu

zinarudia ubichi.

Miti nayo inazaa matunda,

mtini na mzabibu inatoa utajiri wake.

2:23 Hab 3:18; Yak 5:7; Za 28:7; 33:21; Law 26:4Furahini, enyi watu wa Sayuni,

shangilieni katika Bwana Mungu wenu,

kwa kuwa amewapa mvua za vuli

kwa kipimo cha haki.

Anawapelekea mvua nyingi,

mvua ya vuli na ya masika, kama mwanzoni.

2:24 Law 26:10; Mal 3:10; Mit 3:10; Amo 9:13; Yoe 3:18Sakafu za kupuria zitajaa nafaka,

mapipa yatafurika mvinyo mpya na mafuta.

2:25 Kut 14:10; Amo 4:9“Nitawalipa kwa ajili ya miaka ile iliyoliwa na nzige:

parare, madumadu na tunutu,

jeshi langu kubwa ambalo

nililituma katikati yenu.

2:26 Law 23:40; 26:5; Isa 25:1; 29:22; 62:9; Za 126:3; Mik 6:14Mtakuwa na wingi wa vyakula mpaka mshibe,

na mtalisifu jina la Bwana Mungu wenu,

ambaye amefanya maajabu kwa ajili yenu;

kamwe watu wangu hawataaibishwa tena.

2:27 Kut 6:2; Isa 44:8; 45:5; 54:4; Yoe 3:17; Law 26:11; Sef 3:11Ndipo mtakapojua kwamba mimi niko katika Israeli

kwamba mimi ndimi Bwana Mungu wenu,

na kwamba hakuna mwingine;

kamwe watu wangu hawataaibika tena.

Siku Ya Bwana

2:28 Yn 7:38; 11:2; Eze 39:29; Mdo 21:9; Hes 11:17; Gal 3:14; 1Sam 19:20“Hata itakuwa, baada ya hayo,

nitamimina Roho wangu juu ya wote wenye mwili.

Wana wenu na binti zenu watatabiri,

wazee wenu wataota ndoto,

na vijana wenu wataona maono.

2:29 1Kor 12:13; Gal 3:28; Eze 36:27Hata juu ya watumishi wangu, wanaume kwa wanawake,

katika siku zile nitamimina Roho wangu.

2:30 Lk 21:11; Mk 13:24-25Nami nitaonyesha maajabu katika mbingu

na duniani:

damu, moto na mawimbi ya moshi.

2:31 Isa 22:5; Mt 24:29; Isa 13:9-10; Mal 3:2; Yer 4:23; Yoe 1:15Jua litageuzwa kuwa giza

na mwezi kuwa mwekundu kama damu,

kabla ya kuja siku ya Bwana

ile kuu na ya kutisha.

2:32 Rum 9:27; 10:13; Oba 1:17; Mik 4:7; 7:18; Isa 11:11; 46:13; Za 106:8; 50:12; Yer 33:3; Mwa 4:26; Mdo 2:21, 39Na kila mtu atakayeliitia

jina la Bwana ataokolewa.

Kwa maana juu ya Mlima Sayuni na katika Yerusalemu

kutakuwepo wokovu,

kama Bwana alivyosema,

miongoni mwa walionusurika

ambao Bwana awaita.

Read More of Yoeli 2

Yoeli 3:1-21

Mataifa Yahukumiwa

3:1 Kum 30:3; Yer 16:15; 40:5; Eze 3:20; 38:8“Katika siku hizo na wakati huo,

nitakaporejesha neema ya Yuda na Yerusalemu,

3:2 Zek 14:2; Isa 13:9; 2Nya 20:26; Isa 66:16; Yer 2:35; Sef 3:8; Mwa 11:4; Law 26:33nitayakusanya mataifa yote na kuyaleta

katika Bonde la Yehoshafati3:2 Yehoshafati maana yake Bwana huhukumu.

Hapo nitaingia kwenye hukumu dhidi yao

kuhusu urithi wangu, watu wangu Israeli,

kwa kuwa waliwatawanya watu wangu

miongoni mwa mataifa

na kuigawa nchi yangu.

3:3 Oba 1:11; Amo 2:6; Ay 6:27; Eze 24:6Wanawapigia kura watu wangu

na kuwauza wavulana ili kupata makahaba;

waliwauza wasichana

ili wapate kunywa mvinyo.

3:4 Mwa 10:15; Mt 11:21; Yak 2:13; Lk 18:7; Amo 1:6-9; Isa 14:29-31; 34:8; Za 87:4; Eze 25:15-17“Sasa una nini dhidi yangu, ee Tiro na Sidoni, nanyi nchi zote za Ufilisti? Je, mnanilipiza kwa yale niliyoyafanya? Kama mnalipa, mimi nitalipiza juu ya vichwa vyenu kwa kasi na kwa haraka yale mliyoyatenda. 3:5 1Fal 15:18; 2Nya 21:16-17Kwa kuwa mlichukua fedha na dhahabu yangu pia mkabeba hazina zangu nzuri sana mkapeleka kwenye mahekalu yenu. 3:6 Eze 27:13; Zek 9:13Mliwauza watu wa Yuda na Yerusalemu kwa Wayunani, ili kwamba mpate kuwapeleka mbali na nchi yao.

3:7 Isa 43:5-6; 66:6; Yer 23:8“Tazama nitawaamsha kutoka zile sehemu mlizowauza, nami nitawalipiza juu ya vichwa vyenu kile mlichofanya. 3:8 Eze 23:42; Isa 14:2; 60:14; Mwa 10:7; Yer 30:16; 2Nya 9:1Nitawauza wana wenu na binti zenu kwa watu wa Yuda, nao watawauza kwa Waseba, taifa lililo mbali.” Bwana amesema.

3:9 Isa 8:9; Yer 46:4Tangazeni hili miongoni mwa mataifa:

Jiandaeni kwa vita!

Amsha askari!

Wanaume wote wapiganaji

wasogee karibu na kushambulia.

3:10 Zek 12:8; Isa 2:4; Mik 4:3; Hes 25:7Majembe yenu yafueni yawe panga

na miundu yenu ya kukatia iwe mikuki.

Aliye dhaifu na aseme,

“Mimi nina nguvu!”

3:11 Eze 38:15-16; Sef 3:8; Isa 13:3Njooni haraka, ninyi mataifa yote kutoka pande zote,

kusanyikeni huko.

Shusha wapiganaji wako, Ee Bwana!

3:12 Za 96:13; 82:1; 2Nya 20:26; Isa 2:4“Mataifa na yaamshwe;

na yasonge mbele kuelekea Bonde la Yehoshafati,

kwa kuwa nitaketi mahali pale

kuhukumu mataifa yote yaliyoko kila upande.

3:13 Isa 17:5; Ufu 14:15-20; Amu 6:11; Mt 13:39; Mk 4:29; Yer 51:33; Hos 6:11Tia mundu,

kwa kuwa mavuno yamekomaa.

Njooni, mkanyage zabibu,

kwa kuwa shinikizo la kukamua zabibu limejaa

na mapipa yanafurika:

kwa kuwa uovu wao ni mkubwa!”

3:14 Isa 2:4; 13:4; 34:2-8; Sef 1:7; Yoe 1:15; Eze 36:5Umati mkubwa, umati mkubwa

katika bonde la uamuzi!

Kwa kuwa siku ya Bwana ni karibu

katika bonde la uamuzi.

Jua na mwezi vitatiwa giza,

na nyota hazitatoa mwanga wake tena.

3:16 Amu 5:4; Isa 14:16; 25:4; 42:13; 2Sam 22:3; Zek 9:12; Eze 38:19Bwana atanguruma kutoka Sayuni

na mshindo wa ngurumo kutoka Yerusalemu;

dunia na mbingu vitatikisika.

Lakini Bwana atakuwa kimbilio la watu wake,

ngome imara kwa ajili ya watu wa Israeli.

Baraka Kwa Watu Wa Mungu

3:17 Yoe 2:27; Za 74:2; Isa 4:3; 35:8; Ufu 21:27; Nah 1:15; Kut 6:7; Yer 31:40; Eze 44:9“Ndipo mtakapojua kwamba Mimi, Bwana Mungu wenu,

nakaa Sayuni, mlima wangu mtakatifu.

Yerusalemu utakuwa mtakatifu;

kamwe wageni hawatavamia tena.

3:18 Kut 3:8; Eze 47:1; Zek 13:1; Wim 5:1; Isa 25:6; 30:25; 35:6; 44:3; Ufu 22:1-2; Hes 25:1; Yoe 2:24“Katika siku hiyo milima itadondosha divai mpya,

na vilima vitatiririka maziwa;

mabonde yote ya Yuda yatatiririka maji.

Chemchemi itatiririka kutoka kwenye nyumba ya Bwana

na kunywesha Bonde la Shitimu.3:18 Au: Bonde la Migunga.

3:19 Yer 51:35; Oba 1:10; Isa 11:14; 34:11Lakini Misri itakuwa ukiwa,

Edomu itakuwa jangwa tupu,

kwa sababu ya jeuri waliofanya kwa watu wa Yuda,

ambao katika nchi yao

walimwaga damu isiyo na hatia.

3:20 Ezr 9:12; Amo 9:15Yuda itakaliwa na watu milele

na Yerusalemu itadumu vizazi vyote.

3:21 Eze 36:25; 48:35; Isa 1:15; 59:20; Za 74:2; Zek 8:3Hatia yao ya damu, ambayo sijasamehe,

nitasamehe.”

Bwana anakaa Sayuni!

Read More of Yoeli 3