Ayubu 25:1-6, Ayubu 26:1-14, Ayubu 27:1-23, Ayubu 28:1-28, Ayubu 29:1-25 NEN

Ayubu 25:1-6

Bildadi Anasema: Mwanadamu Awezaje Kuwa Mwadilifu Mbele Za Mungu?

25:1 Ay 8:1Ndipo Bildadi Mshuhi akajibu:

25:2 Zek 9:2; Ufu 1:6“Mamlaka na kuheshimiwa ni vyake Mungu;

yeye huthibitisha amani katika mbingu juu.

25:3 Mt 5:45; Yak 1:17; Mwa 1:14-16Je, majeshi yake yaweza kuhesabika?

Ni nani asiyeangaziwa na nuru yake?

25:4 Ay 4:17; 14:4; Rum 3:19-20Mtu awezaje kuwa mwadilifu mbele za Mungu?

Awezaje mtu aliyezaliwa na mwanamke kuwa safi?

25:5 Ay 31:26; 4:18Ikiwa hata mwezi sio mwangavu

nazo nyota si safi machoni pake,

25:6 Za 22:6; 80:17; Eze 2:1; Ay 7:5sembuse mtu ambaye ni funza:

mwanadamu ambaye ni buu tu!”

Read More of Ayubu 25

Ayubu 26:1-14

Hotuba Ya Tisa Ya Ayubu

Ayubu Anajibu: Utukufu Wa Mungu Hauchunguziki

Kisha Ayubu akajibu:

26:2 Ay 6:12; 4:3; Za 71:9; Mit 25:11“Tazama jinsi ulivyomsaidia mtu asiye na uwezo!

Jinsi ulivyouokoa mkono ulio dhaifu!

26:3 Ay 34:35Ni shauri gani ulilompa yeye asiye na hekima?

Nayo ni busara gani kubwa uliyoonyesha!

26:4 1Fal 22:24Ni nani aliyekusaidia kutamka maneno hayo?

Nayo ni roho ya nani iliyosema kutoka kinywani mwako?

26:5 Za 88:10; Isa 14:9“Wafu wako katika maumivu makuu,

wale walio chini ya maji na wale waishio ndani yake.

26:6 Za 139:8; Mit 15:11; Ebr 4:13; Amo 9:2Mauti26:6 Yaani Kuzimu; Kiebrania ni Sheol. iko wazi mbele za Mungu;

Uharibifu26:6 Kwa Kiebrania ni Abadon. haukufunikwa.

26:7 Ay 9:826:7 Ay 8:22; 31:35Hutandaza anga la kaskazini mahali patupu;

naye huiningʼiniza dunia mahali pasipo na kitu.

26:8 Mit 30:4; Za 147:8Huyafungia maji kwenye mawingu yake,

hata hivyo mawingu hayapasuki kwa uzito wake.

26:9 2Sam 22:10; Za 97:2Huufunika uso wa mwezi mpevu,

akitandaza mawingu juu yake.

26:10 Mit 8:27; Isa 40:22; Ay 28:3Amechora mstari wa upeo juu ya uso wa maji,

ameweka mpaka wa nuru na giza.

26:11 2Sam 22:8Nguzo za mbingu nazo zatetemeka,

zinatishika anapozikemea.

26:12 Isa 51:15; Kut 14:21; Yer 31:35; Ay 12:13; Kut 14:21; Ay 12:13; 9:13Kwa nguvu zake aliisukasuka bahari;

kwa hekima yake alimkata Rahabu26:12 Rahabu hapa ni fumbo la kumaanisha Lewiathani, mnyama mkubwa wa baharini mwenye magamba anayefanana na joka kubwa, mwenye umbo la kutisha, asiyeweza kuvuliwa. vipande vipande.

26:13 Za 33:6; Isa 27:1Aliisafisha anga kwa pumzi yake;

kwa mkono wake alimchoma joka aendaye mbio.

26:14 Ay 9:6; 36:29Haya ni mambo madogo tu katika matendo yake;

tazama jinsi ulivyo mdogo mnongʼono tunaousikia kumhusu!

Ni nani basi awezaye kuelewa

ngurumo za nguvu zake?”

Read More of Ayubu 26

Ayubu 27:1-23

Hotuba Ya Mwisho Ya Ayubu

Ayubu Anadumisha Uadilifu Wake

27:1 Ay 29:1Ndipo Ayubu akaendelea na hoja yake, akasema:

27:2 Ay 9:18; 34:5; Isa 45:9; 1Sam 1:10“Hakika kama Mungu aishivyo, aliyeninyima haki yangu,

Mwenyezi ambaye amenifanya

nionje uchungu wa nafsi,

27:3 Mwa 2:7; Za 144:4kwa muda wote nitakaokuwa na uhai ndani yangu,

nayo pumzi ya Mungu ikiwa puani mwangu,

27:4 Ay 6:28; 12:16; 16:17midomo yangu haitanena uovu,

wala ulimi wangu hautatamka udanganyifu.

27:5 Ay 2:9; 10:7; 32:2Sitakubaliana nanyi kabisa kuwa mko sahihi;

hadi nife, sitakana uadilifu wangu.

27:6 Ay 29:14; Za 119:121; Isa 59:17; 61:10; Rum 2:15Nitadumisha haki yangu wala sitaiacha;

dhamiri yangu haitanisuta muda wote ninaoishi.

“Watesi wangu wawe kama waovu,

nao adui zangu wawe kama wasio haki!

27:8 Ay 8:13; Hes 16:22; Lk 12:20; Mt 16:26Kwa maana mtu asiyemcha Mungu

analo tegemeo gani anapokatiliwa mbali,

Mungu anapouondoa uhai wake?

27:9 Zek 7:13; Mik 3:4; 1Sam 8:18Je, Mungu husikiliza kilio chake,

shida zimjiapo?

27:10 Ay 22:26Je, anaweza kumfurahia Mwenyezi?

Je, atamwita Mungu nyakati zote?

27:11 Ay 36:23; 27:13“Nitawafundisha juu ya uweza wa Mungu;

njia za Mwenyezi sitazificha.

Ninyi nyote mmeona hili wenyewe.

Ni ya nini basi mazungumzo haya yasiyo na maana?

27:13 Ay 15:20; 16:19“Hili ndilo fungu ambalo Mungu humpa mtu mwovu,

urithi ule mtu mdhalimu anapokea kutoka kwa Mwenyezi:

27:14 Mao 2:22; Es 9:10; Hos 9:13; Ay 20:10; 2Fal 10:6-10Hata kama watoto wake watakuwa wengi kiasi gani,

fungu lao ni kuuawa kwa upanga;

wazao wake hawatakuwa kamwe

na chakula cha kuwatosha.

27:15 Za 78:64Tauni itawazika wale watakaonusurika miongoni mwao,

nao wajane wao hawatawaombolezea.

27:16 Zek 9:3Ajapokusanya fedha nyingi kama mavumbi,

na mavazi kama malundo ya udongo wa mfinyanzi,

27:17 Mit 13:22; Mhu 2:26yale yote mtu mwovu aliyojiwekea akiba, mwenye haki atayavaa,

naye asiye na hatia ataigawanya fedha yake.

27:18 Ay 8:14; Isa 1:8; 24:20; Mao 2:6Nyumba aijengayo ni kama utando wa buibui,

kama kibanda alichotengeneza mlinzi.

27:19 Ay 3:13; Hes 20:26Yeye hulala akiwa tajiri, lakini ndiyo mara ya mwisho;

afunguapo macho yake, yote yametoweka.

27:20 Ay 15:21; 20:8Vitisho humjia kama mafuriko;

dhoruba humkumba ghafula usiku.

27:21 Ay 38:24; Yer 13:24; Ay 30:22; 7:10; Yer 22:22Upepo mkali wa mashariki humchukua, naye hutoweka;

humzoa kutoka mahali pake.

27:22 Yer 13:14; Eze 5:11; Ay 11:20Humvurumisha bila huruma,

huku akikimbia kasi kukwepa nguvu zake.

27:23 Ay 7:10; 18:18Upepo humpigia makofi kwa dharau,

na kumfukuza atoke mahali pake.

Read More of Ayubu 27

Ayubu 28:1-28

Mapumziko: Imani Inakopatikana

28:1 Za 12:6; 66:10; Yer 9:7; Mal 3:3; Dan 11:35“Kuna machimbo ya fedha,

na mahali dhahabu isafishwapo.

28:2 Kum 8:9Chuma hupatikana ardhini,

nayo shaba huyeyushwa kutoka mawe ya madini.

28:3 Mhu 7:25; 8:17; Mit 2:4Mwanadamu hukomesha giza;

huyatafuta hadi sehemu iliyo mbali,

kwa ajili ya kuchimbua mawe yenye madini

katika giza jeusi sana.

28:4 2Sam 5:8Huchimba shimo jembamba mbali na makao ya watu,

mahali paliposahaulika na nyayo za wanadamu;

mbali na wanadamu huningʼinia na kupembea kwa kamba.

28:5 Mwa 1:29; Za 145:15Ardhi, ambako chakula hutoka,

chini hugeuzwa kwa moto;

28:6 Isa 54:11; Wim 5:14; Ay 22:24yakuti samawi hutoka katika miamba yake,

nalo vumbi lake lina vipande vya dhahabu.

28:7 Ay 28:21Hakuna ndege awindaye aijuaye njia ile iliyofichika,

wala hakuna jicho la mwewe lililoiona.

28:8 Ay 41:34; Isa 35:9Wanyama wa porini wanaotamba hawajawahi kupakanyaga,

wala simba azungukaye huko.

28:9 Kum 8:15; Yn 2:6Mikono ya mwanadamu hushambulia miamba migumu sana,

na kuiacha wazi mizizi ya milima.

28:10 Mit 2:4; Ay 28:4Hutoboa shimo refu la kupenya chini kwa chini kwenye miamba;

macho yake huona hazina zake zote.

28:11 Mwa 7:11; Isa 48:6; Yer 33:3Hutafuta vyanzo vya mito

na kuvileta vitu vilivyofichika katika nuru.

28:12 Mit 1:20; Mhu 7:24“Lakini hekima inaweza kupatikana wapi?

Ufahamu unakaa wapi?

28:13 Mit 3:15; Mt 13:44-46Mwanadamu hatambui thamani yake;

haiwezi kupatikana katika nchi ya walio hai.

Kilindi husema, ‘Haiko ndani yangu’;

bahari nayo husema, ‘Haiko pamoja nami.’

28:15 Mit 16:16; Mdo 8:20Haiwezi kununuliwa kwa dhahabu safi kuliko zote,

wala thamani yake haiwezi kupimwa kwa fedha.

Haiwezi kununuliwa kwa dhahabu ya Ofiri,

kwa shohamu ya thamani kubwa au yakuti samawi ya thamani kubwa.

28:17 Za 119:72; Mit 8:10; Ay 28:15Dhahabu wala mawe maangavu haviwezi kulinganishwa nayo,

wala haiwezi hubadilishwa na vito vya dhahabu.

Marijani na yaspi hazistahili kutajwa;

thamani ya hekima ni zaidi ya akiki nyekundu.

28:19 Mit 3:14-15; 8:10-19Yakuti manjano ipatikanayo Kushi haiwezi kulinganishwa nayo,

wala haiwezi kununuliwa kwa dhahabu safi.

“Ni wapi basi hekima itokako?

Ufahamu hukaa wapi?

28:21 Ay 28:7Imefichika machoni pa kila kitu kilicho hai,

imesitiriwa hata kwa ndege wa angani.

28:22 Ay 26:6Uharibifu na Mauti husema,

‘Ni uvumi wake tu uliotufikia masikioni mwetu.’

28:23 Mdo 15:18; Ay 22:22; Mit 8:22-31Mungu anaifahamu njia ya kuiendea hekima

na ndiye peke yake anayefahamu inakokaa,

28:24 Isa 11:12; Yos 3:11; Ebr 4:13; Za 66:7kwa maana yeye huitazama miisho ya dunia

na huona kila kitu chini ya mbingu.

28:25 Ay 38:8-11; Za 135:7Alipofanyiza nguvu za upepo

na kuyapima maji,

28:26 Ay 38:25-27; Isa 35:7; Yer 14:22alipofanya maagizo kwa ajili ya mvua

na njia kwa ajili ya umeme wa radi,

ndipo alipoitazama hekima na kuikadiria thamani yake,

akaithibitisha na kuihakikisha.

28:28 Kut 20:20; Kum 4:6Naye Mungu akamwambia mwanadamu,

‘Kumcha Bwana: hiyo ndiyo hekima,

nako kujitenga na uovu ndio ufahamu.’ ”

Read More of Ayubu 28

Ayubu 29:1-25

Ayubu Anamaliza Utetezi Wake

29:1 Za 18:28; Ay 13:12Ayubu akaendelea na hoja yake, akasema:

29:2 Yer 1:12; 44:27“Tazama jinsi ninavyoitamani miezi iliyopita,

zile siku ambazo Mungu alikuwa akinilinda,

29:3 Ay 11:17; 12:25wakati taa yake iliniangazia kichwani changu,

na kwa mwanga wake Mungu nikapita katikati ya giza!

29:4 Za 25:14; Mit 3:32Natamani siku zile nilizokuwa katika ustawi wangu,

wakati urafiki wa Mungu wa ndani ulipoibariki nyumba yangu,

29:5 Za 127:3-5; 128:3; Rum 4:1wakati Mwenyezi alikuwa pamoja nami,

nao watoto wangu walikuwa wamenizunguka,

29:6 Ay 20:17; Za 81:16; Mwa 49:20; Kum 32:13wakati njia yangu ilikuwa imenyweshewa siagi,

nao mwamba ukanimiminia vijito vya mafuta ya zeituni.

29:7 Ay 5:4; 31:21; Yer 20:2; 38:7“Wakati nilipokwenda kwenye lango la mji

na kuketi katika kiwanja,

29:8 1Tim 5:1; Law 19:32vijana waliniona wakakaa kando,

nao wazee walioketi wakasimama;

29:9 Amu 16:19; Mit 30:32wakuu wakaacha kuzungumza

na kuziba vinywa vyao kwa mikono yao;

29:10 Za 137:6wenye vyeo wakanyamazishwa,

nazo ndimi zao zikagandamana na makaakaa ya vinywa vyao.

29:11 Ay 4:4; Ebr 11:4Yeyote aliyenisikia alinena mema juu yangu,

nao walioniona walinisifu,

29:12 Kum 24:17; Ay 31:17-21; Za 72:12; Mit 21:13kwa sababu nilimwokoa maskini aliyeomba msaada,

naye yatima aliyekuwa hana wa kumsaidia.

29:13 Ay 31:20; 22:9; Kum 10:18Mtu aliyekuwa karibu kufa alinibariki,

nami niliufanya moyo wa mjane kuimba.

29:14 2Sam 8:15; Rum 13:14; Efe 6:14Niliivaa haki kama vazi langu;

uadilifu ulikuwa joho langu na kilemba changu.

29:15 Hes 10:31Nilikuwa macho ya kipofu

na miguu kwa kiwete.

29:16 Ay 24:4; Mit 29:7Nilikuwa baba kwa mhitaji;

nilimtetea mgeni.

29:17 Ay 24:9; 4:10, 11; Za 3:7Niliyavunja meno makali ya waovu,

na kuwapokonya wahanga kwenye meno yao.

29:18 Za 62:2; Mit 3:1-2“Nikafikiri, ‘Nitafia katika nyumba yangu mwenyewe,

nazo siku zangu zitakuwa nyingi kama chembechembe za mchanga.

29:19 Hes 24:6; Yer 17:8Mizizi yangu itafika mpaka kwenye maji,

nao umande utakaa juu ya matawi yangu usiku kucha.

29:20 Za 18:34; Isa 38:12; Mwa 49:24Utukufu wangu utabakia kuwa mpya ndani yangu,

upinde wangu daima utaendelea kuwa mpya mkononi mwangu.’

29:21 Ay 29:21“Watu walinisikiliza kwa tumaini,

wakingojea ushauri wangu kwa utulivu.

29:22 Kum 32:2Baada ya mimi kuzungumza, hawakusema zaidi;

maneno yangu yaliingia masikioni mwao kwa makini.

Waliningojea kama manyunyu ya mvua

na kuyapokea maneno yangu

kama ardhi inyonyavyo mvua ya vuli.

Walipokata tamaa niliwaonyesha uso wa furaha;

nuru ya uso wangu ilikuwa ya thamani kwao.

29:25 Ay 31:31; 4:4Niliwachagulia njia na kukaa kama mkuu wao;

niliishi kama mfalme katikati ya majeshi yake;

nikawa kama yeye anayewafariji waombolezaji.

Read More of Ayubu 29