Ayubu 22:1-30
Elifazi Anasema: Uovu Wa Ayubu Ni Mkubwa
22:1 Ay 4:1Ndipo Elifazi Mtemani akajibu:
22:2 Lk 17:10; Za 16:2“Je, mwanadamu aweza kuwa wa faida kwa Mungu?
Je, hata mtu mwenye hekima aweza kumfaidi?
22:3 Isa 1:11; Hag 1:8; Za 143:2; Ay 35:7; Za 9:12Je, Mwenyezi angefurahia nini
kama ungekuwa mwadilifu?
Au je, yeye angepata faida gani
kama njia zako zingekuwa kamilifu?
22:4 Isa 3:14; Eze 20:35“Je, ni kwa ajili ya utaua wako ndiyo maana anakukemea
na kuleta mashtaka dhidi yako?
22:5 Ezr 9:13; Ay 11:6; Ezr 9:13; Ay 15:5; 15:13; 20:29; 29:17Je, uovu wako si mkuu?
Dhambi zako si hazina mwisho?
22:6 Kum 24:6, 17; Eze 18:12-16Umedai dhamana kwa ndugu zako bila sababu;
umewavua watu nguo zao, ukawaacha uchi.
22:7 Ay 31:16-17; Eze 18:7; Mt 25:42Hukumpa maji aliyechoka,
nawe ulimnyima chakula mwenye njaa,
22:8 Ay 15:19; Isa 3:3; 5:13; 9:15; Ay 12:19ingawa ulikuwa mtu mwenye uwezo ukimiliki nchi:
mtu uliyeheshimiwa, ukiishi ndani yake.
22:9 Isa 10:2; Lk 1:53Umewafukuza wajane mikono mitupu
na kuzivunja nguvu za yatima.
22:10 Ay 18:9; 10:3; 15:21Ndiyo sababu mitego imekuzunguka pande zote,
hatari ya ghafula inakutia hofu,
22:11 Ay 5:14; Isa 58:10-11; Mao 3:54ndiyo sababu ni giza sana huwezi kuona,
tena ndiyo sababu mafuriko ya maji yamekufunika.
22:12 Ay 11:8; 16:19“Je, Mungu hayuko katika mbingu za juu?
Juu kuliko nyota zilizo juu sana!
22:13 Eze 9:9; Efe 6:2; Sef 1:12; Za 139:11Hivyo wewe wasema, ‘Mungu anajua nini?’
Je, yeye huhukumu katika giza kama hilo?
22:14 Ay 26:9; Za 97:2; 105:39; 105:13; 2Fal 21:16; Ay 37:18; Za 18:11; Mit 8:27; Yer 23:23-24Mawingu mazito ni pazia lake, hivyo hatuoni sisi
atembeapo juu ya anga la dunia.
22:15 Mwa 6:11-13Je, utaifuata njia ya zamani,
ambayo watu waovu waliikanyaga?
22:16 Ay 15:32; Mwa 7:23; Mt 7:26-27Waliondolewa kabla ya wakati wao,
misingi yao ikachukuliwa na mafuriko.
22:17 Ay 21:15Walimwambia Mungu, ‘Tuache sisi!
Huyo Mwenyezi aweza kutufanyia nini?’
22:18 Ay 12:6; 21:16Lakini ndiye alizijaza nyumba zao na vitu vizuri,
hivyo ninajitenga mbali na mashauri ya waovu.
22:19 Za 64:10; 97:12; Ay 21:3“Wenye haki wanaona maangamizi yao na kufurahi,
nao wasio na hatia huwadhihaki, wakisema,
22:20 Ay 15:30‘Hakika adui zetu wameangamizwa,
nao moto umeteketeza mali zao.’
22:21 Mit 3:10; 1Pet 5:6; Isa 27:5“Mjue sana Mungu ili uwe na amani,
ndipo mema yatakapokujia.
22:22 Kum 8:3; Ay 6:10; Eze 3:10; Mit 2:6; Za 37:31Uyapokee mafundisho toka kinywani mwake,
na maneno yake uyaweke moyoni mwako.
22:23 Isa 19:22; 44:22; Eze 18:32; Mdo 20:32; Ay 11:14Kama ukimrudia Mwenyezi, utarudishwa upya:
Kama ukiuondoa uovu uwe mbali na hema lako,
22:24 Isa 2:20; 30:22kama dhahabu yako ukiihesabu kama mavumbi,
dhahabu yako ya Ofiri kama miamba ya mabondeni,
22:25 2Fal 18:7; Mt 6:20-21ndipo Mwenyezi atakuwa dhahabu yako,
naye atakuwa fedha yako iliyo bora.
22:26 Za 2:8; Isa 61:10Hakika ndipo utakapojifurahisha kwa Mwenyezi,
nawe utamwinulia Mungu uso wako.
22:27 Ay 5:27; Isa 58:9Utamwomba yeye, naye atakusikia,
nawe utazitimiza nadhiri zako.
22:28 Za 103:11; 145:19; Ay 33:28; Mit 4:18; Za 97:11Utakusudia jambo nalo litatendeka,
nao mwanga utaangazia njia zako.
22:29 Za 18:27; 1Pet 5:5Watu watakaposhushwa, nawe ukasema, ‘Wainue!’
ndipo atamwokoa aliyevunjika moyo.
22:30 2Sam 22:21; Ay 42:7-8Atamwokoa hata yule ambaye ana hatia,
ataokolewa kwa sababu ya usafi wa mikono yako.”
Ayubu 23:1-17
Hotuba Ya Nane Ya Ayubu
Ayubu Anajibu: Kulalamika Kwangu Ni Uchungu
Ndipo Ayubu akajibu:
23:2 Ay 6:3; 7:11; 1Sam 1:10“Hata leo malalamiko yangu ni chungu;
mkono wake ni mzito juu yangu hata nikiugua.
23:3 Kum 4:29Laiti ningefahamu mahali pa kumwona;
laiti ningeweza kwenda mahali akaapo!
23:4 Ay 13:18; 9:15Ningeliweka shauri langu mbele zake,
na kukijaza kinywa changu na hoja.
Ningejua kwamba angenijibu nini,
na kuelewa lile ambalo angelisema.
23:6 Ay 9:4, 19; Isa 27:4Je, angenipinga kwa nguvu nyingi?
La, asingenigandamiza.
23:7 Mwa 3:8; Ay 9:3Hapo mtu mwadilifu angeweka shauri lake mbele zake,
nami ningeokolewa milele na mhukumu wangu.
“Lakini nikienda mashariki, hayupo;
nikienda magharibi, simpati.
23:9 Ay 9:11Anapokuwa kazini pande za kaskazini, simwoni;
akigeukia kusini, nako simwoni hata kidogo.
23:10 Za 66:10; 139:1-3; 12:6; 1Pet 1:7; Yak 1:12Lakini anaijua njia niiendeayo;
akiisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu.
23:11 Za 17:5; Ay 31:7; Yer 11:20; Za 44:18; 125:5Nyayo zangu zimefuata hatua zake kwa karibu;
nimeishika njia yake bila kukengeuka.
23:12 Ay 6:10; 15:11; Yn 4:32, 34; Mt 4:4Sijaziacha amri zilizotoka midomoni mwake;
nimeyathamini maneno ya kinywa chake kuliko chakula changu cha kila siku.
23:13 Za 115:3; Isa 55:11; Mhu 3:14; Rum 9:19“Lakini yeye husimama peke yake; ni nani awezaye kumpinga?
Yeye hufanya lolote atakalo.
23:14 1The 3:3; 1Pet 4:12Hutimiliza maagizo yake dhidi yangu,
na bado anayo mipango mingi kama hiyo ambayo ameiweka akiba.
23:15 Mwa 45:3; Yos 24:14; Mhu 3:14; 12:13; 2Kor 5:11Hiyo ndiyo sababu ninaingiwa na hofu mbele zake;
nifikiriapo haya yote ninamwogopa.
23:16 Za 22:14; Yer 51:46; Ay 27:223:16 Kum 20:3; Ay 27:2; Kut 3:6; Ufu 6:16Mungu ameufanya moyo wangu kuzimia;
yeye Mwenyezi amenitia hofu.
23:17 Ay 3:6; 6:9; 19:8Hata hivyo sijanyamazishwa na giza,
wala kwa giza nene linalofunika uso wangu.
Ayubu 24:1-25
Ayubu Analalamikia Jeuri Duniani
24:1 Yer 46:10; 2Pet 3:7; Ay 15:20; Mdo 1:7“Kwa nini Mwenyezi asiweke nyakati kwa ajili ya hukumu?
Kwa nini wale wamjuao wazitafute siku kama hizo bila mafanikio?
24:2 Kum 19:14; 27:17; Mit 23:10Watu husogeza mawe ya mpaka;
huchunga makundi ya wanyama waliyonyangʼanya kwa nguvu.
24:3 Kum 24:6-10; 12:17; Ay 6:27Huwanyangʼanya yatima punda wao,
na kumchukua rehani fahali wa mjane.
24:4 Mit 28:28; Ay 20:19; Isa 11:4; Za 12:5Humsukuma mhitaji kutoka njia,
na kuwafanya maskini wote wa nchi kulazimika kujificha.
24:5 Mwa 16:12; Za 104:23; Ay 30:3Kama punda-mwitu jangwani,
maskini huzunguka katika kazi zao za kutafuta chakula;
mahali palipo jangwa
huwapa chakula cha watoto wao.
24:6 Ay 6:5; Rut 2:22; 1Fal 21:19Hukusanya chakula mashambani na kuokota masazo
katika mashamba ya mizabibu ya waovu.
24:7 Kut 22:26-27; Kum 24:12; Ay 22:6Kwa kukosa nguo, usiku kucha hukaa uchi;
hawana chochote cha kujifunika baridi.
24:8 Dan 4:25, 33; Mao 4:5Hutota kwa mvua za mlimani,
nao huikumbatia miamba kwa ajili ya kukosa pa kujisitiri.
24:9 Kum 24:17Mtoto yatima hupokonywa matitini;
mtoto wachanga wa maskini hunyakuliwa kwa ajili ya deni.
24:10 Kum 24:12-13; Law 19:9Kwa kukosa nguo, hutembea uchi;
hubeba miganda ya ngano, lakini huwa na njaa.
24:11 Isa 5:2; 16:10; Hag 2:16; Mik 6:15Hukamua zeituni katika mawe ya kusagia;
hukanyaga mashinikizo, lakini wanaona kiu.
24:12 Isa 30:19; Ay 9:23; Ufu 6:10; Mhu 8:11Kilio cha huzuni cha wanaokufa kinapaa kutoka mjini,
nazo nafsi za waliojeruhiwa zinalilia msaada.
Lakini Mungu hamlaumu mtu yeyote
kwa kutenda mabaya.
24:13 Ay 38:15; 1The 5:4-5; Za 18:28; Efe 5:8-14“Wako wale wanaoiasi nuru,
wasiofahamu njia zake
wala hawakai katika mapito yake.
24:14 Isa 3:15; Mik 3:3; Ay 20:19; Za 37:32; 10:9Wakati mwanga wa mchana unapotoweka, muuaji huinuka
naye huwaua maskini na mhitaji;
wakati wa usiku hunyemelea kama mwizi.
24:15 Mit 7:8-9; Za 10:11Jicho la mzinzi hungojea wakati wa giza,
naye hufikiri, ‘Hakuna jicho litakaloniona,’
naye huuficha uso wake.
24:16 Kut 22:2; Mt 6:19; Yn 3:20Katika giza, huvunja majumba,
lakini wakati wa mchana hujifungia ndani;
hawataki kufanya lolote nuruni.
24:17 Ay 18:11; 15:22; 18:5Kwa wote hawa, giza nene ndiyo asubuhi yao;
hujifanya rafiki na vitisho vya gizani.
24:18 Ay 9:26; 22:16; Yud 23; Isa 57:20“Lakini wao ni povu juu ya maji;
sehemu yao juu ya nchi imelaaniwa,
hivyo hakuna hata mmoja
aendaye kwenye shamba la mizabibu.
24:19 Ay 6:17; 21:13Kama vile joto na hari vinyakuavyo theluji iliyoyeyuka,
ndivyo kuzimu kuwanyakuavyo waliotenda dhambi.
24:20 Ay 18:17; Mit 10:7; Dan 4:14; Za 31:12Tumbo lililowazaa huwasahau,
nao huwa karamu ya mabuu;
watu waovu hawakumbukwi tena,
lakini huvunjika kama mti.
24:21 Ay 22:9Huwafanya mawindo wanawake tasa na wasio na watoto,
nao hawaonyeshi huruma kwa wajane.
24:22 Kum 28:66; Mt 6:27Lakini Mungu huwakokota wenye nguvu kwa uwezo wake;
ingawa wamestawi, hawana hakika ya maisha.
24:23 Ay 9:24; Amo 6:1; 2Nya 16:9; Ay 10:4Aweza akawaacha wakapumzika wakijihisi salama,
lakini macho yake yanaona njia zao.
24:24 2Fal 19:35; Za 37:35-36; 83:13; Isa 17:5Kwa kitambo kidogo hutukuka, hatimaye hutoweka;
hushushwa na kukusanywa kama wengine wote,
hukatwa kama masuke ya nafaka.
24:25 Ay 16:17; 27:4“Kama hili sivyo, ni nani awezaye kunithibitisha kuwa mwongo,
na kuyafanya maneno yangu kuwa si kitu?”