Yeremia 49:7-39, Yeremia 50:1-10 NEN

Yeremia 49:7-39

Ujumbe Kuhusu Edomu

49:7 Ay 5:12-14; Za 83:6; Eze 25:12; Mwa 36:11-15, 34; 25:30Kuhusu Edomu:

Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote:

“Je, hakuna tena hekima katika Temani?

Je, shauri limewapotea wenye busara?

Je, hekima yao imechakaa?

49:8 Mwa 10:7; Yer 25:23; Isa 2:19; Amu 6:2; Mwa 25:3Geuka na ukimbie, jifiche katika mapango marefu kabisa,

wewe uishiye Dedani,

kwa kuwa nitaleta maafa juu ya Esau

wakati nitakapomwadhibu.

Je, kama wachuma zabibu wangekuja kwako,

wasingebakiza zabibu chache?

Kama wezi wangekujia usiku,

je, si wangeiba tu kiasi ambacho wangehitaji?

49:10 Eze 35:4; Isa 17:14; Mao 1:18; Mwa 3:8; Isa 34:10-12; Yer 11:23Lakini nitamvua Esau nguo abaki uchi,

nitayafunua maficho yake,

ili asiweze kujificha.

Watoto wake, jamaa na majirani wataangamia,

naye hatakuwepo tena.

49:11 Hos 14:3; Mit 23:10-11; Kum 10:18; Yak 1:27Waache yatima wako; nitayalinda maisha yao.

Wajane wako pia

wanaweza kunitumaini mimi.”

49:12 Isa 51:23; Mt 20:22; Mit 11:31; Yer 25:28-29; 25:15Hili ndilo asemalo Bwana: “Kama wale wasiostahili kukinywea kikombe ni lazima wakinywe, kwa nini wewe usiadhibiwe? Hutakwepa kuadhibiwa, ni lazima ukinywe. 49:13 Mwa 22:16; 36:33; Isa 34:6; Yer 42:18; Eze 35:9; Yer 42:18Ninaapa kwa nafsi yangu,” asema Bwana, “kwamba Bosra utakuwa magofu na kitu cha kutisha, cha aibu na cha kulaania; miji yake yote itakuwa magofu milele.”

Nimesikia ujumbe kutoka kwa Bwana:

Mjumbe alitumwa kwa mataifa kusema,

“Jikusanyeni ili kuushambulia!

Inukeni kwa ajili ya vita!”

“Sasa nitakufanya uwe mdogo miongoni mwa mataifa,

aliyedharauliwa miongoni mwa watu.

49:16 Ay 39:27-28; Amo 9:2; Eze 35:13; Oba 1:12Vitisho vyako na kiburi cha moyo wako

vimekudanganya,

wewe unayeishi katika majabali ya miamba,

wewe unayedumu katika miinuko ya kilima.

Ujapojenga kiota chako juu sana kama cha tai,

nitakushusha chini kutoka huko,”

asema Bwana.

49:17 Kum 29:22; Yer 50:13; Eze 35:7“Edomu atakuwa kitu cha kuogofya;

wote wapitao karibu

watashangaa na kuzomea

kwa sababu ya majeraha yake yote.

49:18 Mwa 19:24; Kum 29:23; Amo 4:11; Isa 34:10; Yer 23:14Kama vile Sodoma na Gomora zilivyoangamizwa,

pamoja na miji iliyokuwa jirani nayo,”

asema Bwana,

“vivyo hivyo hakuna mtu yeyote atakayeishi humo.

Naam, hakuna mtu yeyote atakayekaa humo.

49:19 Yer 12:5; Ay 9:19; Yer 50:44; Za 89:6-8; 1Sam 17:34; Kut 8:10; 2Nya 20:6“Kama simba anayepanda kutoka vichaka vya Yordani

kuja kwenye nchi ya malisho mengi,

ndivyo nitamfukuza Edomu kutoka nchi yake ghafula.

Ni nani aliye mteule nitakayemweka kwa ajili ya jambo hili?

Ni nani aliye kama mimi,

na ni nani awezaye kunipinga?

Tena ni mchungaji yupi awezaye

kusimama kinyume nami?”

49:20 Isa 14:27; Yer 50:45; Mao 1:10; Mal 1:3-4; Isa 34:5; Mwa 36:11Kwa hiyo, sikia kile Bwana alichokipanga dhidi ya Edomu,

kile alichokusudia dhidi ya wale waishio Temani:

Aliye mchanga katika kundi ataburutwa mbali;

yeye ataharibu kabisa malisho yao kwa sababu yao.

49:21 Za 114:7; Eze 31:16; Yer 51:29; Eze 26:18; Yer 50:46; Eze 26:15; 27:28Kwa sauti ya anguko lao, dunia itatetemeka.

Kilio chao kitasikika hadi Bahari ya Shamu.49:21 Kwa Kiebrania ni Bahari ya Mafunjo.

49:22 Kum 28:49; Hab 1:8; Isa 13:8; Yer 48:40-41; 4:13; Hos 8:1; Nah 3:13; Mwa 36:33Tazama! Tai atapaa juu angani na kuruka chini kwa ghafula,

akitandaza mabawa yake juu ya Bosra.

Katika siku hiyo, mioyo ya mashujaa wa Edomu

itakuwa kama moyo wa mwanamke katika utungu wa kuzaa.

Ujumbe Kuhusu Dameski

49:23 2Fal 14:28; Mdo 9:2; 1Fal 8:65; Eze 47:16; 2Fal 18:34; Mwa 49:4; Isa 57:20Kuhusu Dameski:

“Hamathi na Arpadi imetahayarika,

kwa kuwa wamesikia habari mbaya.

Wamevunjika moyo na wametaabika

kama bahari iliyochafuka.

49:24 Yer 13:21Dameski amedhoofika,

amegeuka na kukimbia,

hofu ya ghafula imemkamata sana;

amepatwa na uchungu na maumivu,

maumivu kama ya mwanamke katika utungu wa kuzaa.

Kwa nini mji ambao unajulikana haujaachwa,

mji ambao ninaupenda?

49:26 Isa 17:12-14; Yer 50:30; Isa 9:17; 13:18Hakika, vijana wake wanaume wataanguka barabarani;

askari wake wote watanyamazishwa siku hiyo,”

asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.

49:27 Eze 39:6; Amo 1:4; 1Fal 15:18; Yer 21:14; 43:12; Eze 39:6; Mwa 14:15“Nitatia moto kuta za Dameski;

utaangamiza ngome za Ben-Hadadi.”

Ujumbe Kuhusu Kedari Na Hazori

49:28 Mwa 25:13; Amu 6:3; Isa 21:13; Yer 10:22; Yos 11:1Kuhusu Kedari na falme za Hazori, ambazo Nebukadneza mfalme wa Babeli alizishambulia:

Hili ndilo asemalo Bwana:

“Inuka, ushambulie Kedari

na kuwaangamiza watu wa mashariki.

49:29 Yer 6:25; 46:5; Za 120:5Hema zao na makundi yao ya kondoo yatachukuliwa;

vibanda vyao vitatwaliwa

pamoja na mali zao zote na ngamia zao.

Watu watawapigia kelele,

‘Hofu kuu iko kila upande!’

49:30 Amu 6:2; Yos 11:1; Yer 10:22“Kimbieni haraka!

Kaeni kwenye mapango marefu sana, ninyi mkaao Hazori,”

asema Bwana.

“Nebukadneza, mfalme wa Babeli amepanga shauri baya dhidi yenu;

amebuni hila dhidi yenu.

49:31 Eze 38:11; Hes 23:9; Mik 7:14“Inuka na ulishambulie taifa lililo starehe,

linaloishi kwa kujiamini,”

asema Bwana,

“taifa lisilo na malango wala makomeo;

watu wake huishi peke yao.

49:32 Yer 9:26; 25:22; Amu 6:5; Yer 13:24Ngamia wao watakuwa nyara,

nayo makundi yao makubwa ya ngʼombe yatatekwa.

Wale walio maeneo ya mbali

nitawatawanya pande zote,

nami nitaleta maafa juu yao

kutoka kila upande,”

asema Bwana.

49:33 Yer 10:22; 48:9; Isa 13:22; Hos 11:1“Hazori itakuwa makao ya mbweha,

mahali pa ukiwa milele.

Hakuna yeyote atakayeishi humo;

hakuna mtu atakayekaa ndani yake.”

Ujumbe Kuhusu Elamu

49:34 Mwa 10:22; 2Fal 24:18Hili ndilo neno la Bwana lililomjia nabii Yeremia kuhusu Elamu, mapema katika utawala wa Sedekia mfalme wa Yuda:

49:35 Za 37:15; Ezr 4:9; Dan 8:2; Isa 22:6Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote asemalo:

“Tazama, nitavunja upinde wa Elamu,

ulio tegemeo la nguvu zao.

49:36 Dan 11:4Nitaleta pepo nne dhidi ya Elamu

toka pande nne za mbingu,

nitawatawanya katika hizo pande nne,

wala hapatakuwa na taifa

ambalo watu wa Elamu waliofukuzwa

hawatakwenda.

49:37 Yer 44:2; 30:24; 9:16; Eze 32:24Nitamfadhaisha Elamu mbele ya adui zao,

mbele yao wale wanaotafuta uhai wao;

nitaleta maafa juu yao,

naam, hasira yangu kali,”

asema Bwana.

“Nitawafuatia kwa upanga

mpaka nitakapowamaliza.

Nitaweka kiti changu cha enzi huko Elamu

na kumwangamiza mfalme wake na maafisa wake,”

asema Bwana.

49:39 Yer 48:47“Lakini nitarudisha mateka wa Elamu

katika siku zijazo,”

asema Bwana.

Read More of Yeremia 49

Yeremia 50:1-10

Ujumbe Kuhusu Babeli

50:1 Isa 13:1; Za 137:8; Mwa 10:10Hili ndilo neno alilosema Bwana kupitia nabii Yeremia kuhusu Babeli na nchi ya Wakaldayo:

50:2 Kum 30:4; Yer 4:16; 51:31, 47; Isa 21:9; Za 20:5; Isa 13:2; Yer 46:6; Law 26:30“Tangazeni na mhubiri katikati ya mataifa,

twekeni bendera na mkahubiri;

msiache kitu chochote, bali semeni,

‘Babeli utatekwa;

Beli ataaibishwa,

Merodaki atajazwa na hofu kuu.

Sanamu zake zitaaibishwa

na vinyago vyake vitajazwa hofu kuu.’

50:3 Isa 14:22-23; Yer 9:11; Sef 1:3; Isa 13:17; 41:25; Yer 25:26Taifa kutoka kaskazini litamshambulia,

na kuifanya nchi yake ukiwa.

Hakuna hata mmoja atakayeishi ndani yake,

watu na wanyama wataikimbia.

50:4 Eze 37:22; Ezr 3:12; Yer 31:9; Isa 9:13; Hos 3:5; Yer 3:18“Katika siku hizo, wakati huo,”

asema Bwana,

“watu wa Israeli pamoja na watu wa Yuda

wataenda wakilia ili kumtafuta Bwana Mungu wao.

50:5 1Sam 29:1; Yer 33:7; Kum 29:14; Ebr 8:6-10; Isa 11:16; Yer 31:21; 32:40Wataiuliza njia iendayo Sayuni

na kuelekeza nyuso zao huko.

Watakuja na kuambatana na Bwana

katika agano la milele

ambalo halitasahaulika.

50:6 Isa 53:6; Mt 10:6; Yer 3:6; Eze 34:6; Za 119:176; Mt 9:36; Yer 10:21; Za 95:10“Watu wangu wamekuwa kondoo waliopotea;

wachungaji wao wamewapotosha

na kuwasababisha kuzurura

juu ya milima.

Walitangatanga juu ya mlima na kilima,

na kusahau mahali pao wenyewe pa kupumzikia.

50:7 Yer 2:3; 14:8; Za 22:4; Yer 5:17; 10:25; Eze 35:12Yeyote aliyewakuta aliwala;

adui zao walisema, ‘Sisi hatuna hatia,

kwa kuwa wao walitenda dhambi dhidi ya Bwana, malisho yao halisi,

Bwana, aliye tumaini la baba zao.’

50:8 Isa 48:20; Ufu 18:4; Yer 51:6“Kimbieni kutoka Babeli;

ondokeni katika nchi ya Wakaldayo

tena kuweni kama mbuzi wale waongozao kundi.

50:9 Isa 13:17; Yer 25:14; Isa 41:25; Yer 25:26Kwa maana nitaamsha na kuleta dhidi ya Babeli

muungano wa mataifa makubwa kutoka nchi ya kaskazini.

Watashika nafasi zao dhidi yake,

naye kutokea kaskazini atatekwa.

Mishale yao itakuwa kama mishale ya mashujaa walio hodari,

ambao hawawezi kurudi mikono mitupu.

Kwa hiyo Ukaldayo utatekwa nyara;

wote wamtekao nyara watapata za kutosha,”

asema Bwana.

Read More of Yeremia 50