Yeremia 40:7-16, Yeremia 41:1-18, Yeremia 42:1-22 NEN

Yeremia 40:7-16

Gedalia Auawa

(2 Wafalme 25:22-26)

40:7 Yer 39:10; Mdo 24:17; Mwa 41:41; Neh 5:14; Yak 2:5; 2Fal 24:14Maafisa wote wa jeshi na watu wao waliokuwa bado wapo kwenye eneo la wazi waliposikia kwamba mfalme wa Babeli amemteua Gedalia mwana wa Ahikamu kuwa mtawala wa nchi, na amemweka kuwa kiongozi wa wanaume, wanawake na watoto waliokuwa maskini zaidi katika nchi ambao hawakuchukuliwa kwenda uhamishoni Babeli, 40:8 Yer 41:1-2; 2Sam 23:28; Kum 3:14wakamjia Gedalia huko Mispa. Hawa walikuwa Ishmaeli mwana wa Nethania, Yohanani na Yonathani wana wa Karea, Seraya mwana wa Tanhumethi, wana wa Efai Mnetofathi, na Yezania mwana wa Mmaaka, pamoja na watu wao. 40:9 Yer 5:19; Efe 6:5-8; Yer 38:20; Rum 13:1-2; Eze 23:23Gedalia mwana wa Ahikamu mwana wa Shafani akaapa ili kuwatia moyo wao na watu wao. Akasema: “Msiogope kuwatumikia Wakaldayo. Kaeni katika nchi na kumtumikia mfalme wa Babeli, na itakuwa vyema kwenu. 40:10 Kum 1:39; 16:13; Mwa 27:28; Kut 7:19; 23:16; 2Kor 4:7Mimi mwenyewe nitakaa Mispa ili kuwawakilisha mbele ya Wakaldayo wanaotujia, lakini ninyi mtavuna divai, matunda ya kiangazi na mafuta, nanyi mtaweka katika vyombo vyenu vya kuhifadhia, na kuishi katika miji mliyojitwalia.”

40:11 Hes 21:11; 25:1; Isa 16:4; Mao 1:14; Yer 24:9; Mwa 25:30; Yer 12:14Wayahudi wote waliokuwa Moabu, Amoni, Edomu na nchi nyingine zote waliposikia kwamba mfalme wa Babeli ameacha mabaki ya watu katika Yuda na amemweka Gedalia mwana wa Ahikamu mwana wa Shafani kuwa mtawala wao, 40:12 Yer 43:5wakarudi wote katika nchi ya Yuda kwa Gedalia huko Mispa, kutoka nchi zote ambazo walikuwa wametawanywa. Nao wakavuna divai na matunda tele wakati wa kiangazi.

Yohanani mwana wa Karea pamoja na maafisa wote wa jeshi waliokuwa bado wapo kwenye eneo la wazi wakamjia Gedalia huko Mispa 40:14 Mwa 19:38; 2Sam 10:1-19; Amo 1:13; Yer 41:10; 25:21; 49:1na kumwambia, “Je, hujui kwamba Baalisi mfalme wa Waamoni amemtuma Ishmaeli mwana wa Nethania akuue?” Lakini Gedalia mwana wa Ahikamu hakuwaamini.

40:15 Kum 5:17; Mt 5:21-22; Mwa 11:4; Mt 26:31; Yn 11:52; Rum 11:5; 2Fal 21:15Kisha Yohanani mwana wa Karea akamwambia Gedalia kwa siri huko Mispa, “Acha niende nikamuue Ishmaeli mwana wa Nethania, wala hakuna atakayejua. Kwa nini akuue na kusababisha Wayahudi wote waliokuzunguka watawanyike, na mabaki wa Yuda waangamie?”

40:16 Yer 43:2Lakini Gedalia mwana wa Ahikamu akamwambia Yohanani mwana wa Karea, “Usifanye jambo kama hilo! Unalosema kuhusu Ishmaeli si kweli.”

Read More of Yeremia 40

Yeremia 41:1-18

41:1 Yer 40:8; Lk 22:21; Za 41:9Katika mwezi wa saba Ishmaeli mwana wa Nethania mwana wa Elishama, aliyekuwa wa uzao wa mfalme na pia alikuwa mmoja wa maafisa wa mfalme, akaja pamoja na watu kumi kwa Gedalia mwana wa Ahikamu huko Mispa. Walipokuwa wakila pamoja huko, 41:2 Za 41:9; Yer 40:5; 2Sam 3:27; Rum 3:15; Yos 11:10; Ebr 11:37; 2Sam 20:9-10; Yer 40:8Ishmaeli mwana wa Nethania pamoja na wale watu kumi waliokuwa pamoja naye waliinuka na kumuua Gedalia mwana wa Ahikamu mwana wa Shafani kwa upanga, wakamuua yule ambaye mfalme wa Babeli alikuwa amemteua awe mtawala wa nchi. Ishmaeli akawaua pia Wayahudi wote waliokuwa na Gedalia huko Mispa, pamoja na askari wa Kikaldayo waliokuwa huko.

Siku moja baada ya kuuawa kwa siri kwa Gedalia, kabla mtu yeyote hajafahamu jambo hilo, 41:5 Law 19:27; Yer 48:37; Mwa 12:6; 1Fal 16:24; 3:2; Isa 15:2; Yer 47:5; Hes 16:40; Amu 9:1-57; Mk 14:63watu themanini waliokuwa wamenyoa ndevu zao, waliorarua nguo zao na kujikatakata walikuja kutoka Shekemu, Shilo na Samaria wakileta sadaka za nafaka na uvumba katika nyumba ya Bwana. 41:6 2Sam 5:16; Ufu 20:10; Hos 7:11; Za 5:9Ishmaeli mwana wa Nethania akaondoka Mispa ili kwenda kuwalaki, huku akilia alipokuwa akienda. Alipokutana nao, akasema, “Karibuni kwa Gedalia mwana wa Ahikamu.” 41:7 Mwa 27:24; 2Fal 10:14Walipoingia mjini, Ishmaeli mwana wa Nethania na wale watu waliokuwa pamoja naye wakawachinja na kuwatupa ndani ya kisima. 41:8 Isa 45:3Lakini watu kumi miongoni mwao wakamwambia Ishmaeli, “Sisi usituue! Tuna ngano na shayiri, mafuta na asali, vilivyofichwa katika shamba.” Kwa hiyo akawaacha na hakuwaua pamoja na wale wengine. 41:9 1Fal 15:22; 2Nya 16:6; Amu 6:2; Yos 10:16-18Basi kile kisima ambacho alitupa zile maiti za watu aliowaua pamoja na Gedalia kilikuwa ni kile kisima ambacho Mfalme Asa alikifanya sehemu ya ulinzi wake dhidi ya Baasha mfalme wa Israeli. Ishmaeli mwana wa Nethania akakijaza kisima hicho kwa maiti.

41:10 Yer 40:7, 12-14; Neh 2:10, 19Ishmaeli akawafanya mateka watu wote ambao Nebuzaradani kiongozi wa walinzi wa mfalme alikuwa amewaacha huko Mispa na kumweka Gedalia mwana wa Ahikamu juu yao: walikuwa binti za mfalme pamoja na watu wote aliokuwa amewaacha huko. Ishmaeli mwana wa Nethania akawachukua mateka na kuondoka nao, akavuka kwenda kwa Waamoni.

41:11 Yer 40:8-13Yohanani mwana wa Karea na maafisa wote wa jeshi waliokuwa pamoja naye waliposikia juu ya uhalifu wote ambao Ishmaeli mwana wa Nethania alikuwa ameufanya, 41:12 2Sam 2:13; Yn 9:7; Kut 14:14; Yn 18:36; Yos 9:3waliwachukua watu wao wote kwenda kupigana na Ishmaeli mwana wa Nethania. Wakakutana naye karibu na bwawa kubwa huko Gibeoni. Ikawa watu wote waliokuwa na Ishmaeli walipomwona Yohanani mwana wa Karea pamoja na maafisa wa jeshi waliokuwa pamoja naye, wakafurahi. Watu wote ambao Ishmaeli alikuwa amewachukua mateka huko Mispa wakageuka na kumfuata Yohanani mwana wa Karea. 41:15 Yos 21:30; Mit 28; 17; 1Sam 30:17Lakini Ishmaeli mwana wa Nethania pamoja na watu wake wanane wakamtoroka Yohanani na kukimbilia kwa Waamoni.

Kukimbilia Misri

41:16 Yer 42:1; 43:2-4; Eze 7:16; 14:22; Sef 2:9Ndipo Yohanani mwana wa Karea pamoja na maafisa wote wa jeshi waliokuwa pamoja naye wakawaongoza wote walionusurika kutoka Mispa, ambao walipona kutoka mikononi mwa Ishmaeli mwana wa Nethania baada yake kumuua Gedalia mwana wa Ahikamu: walikuwa askari, wanawake, watoto na matowashi aliowaleta kutoka Gibeoni. 41:17 2Sam 19:37; Yer 42:14; Mwa 35:19; Mik 5:2Kisha wakaenda mbele na kutua Geruth-Kimhamu karibu na Bethlehemu wakiwa njiani kwenda Misri 41:18 Hes 14:9; Lk 12:4-5; Yer 40:5; Isa 5:12; Yer 42:16; 2Fal 25:22ili kuwatoroka Wakaldayo. Waliwaogopa kwa sababu Ishmaeli mwana wa Nethania alikuwa amemuua Gedalia mwana wa Ahikamu, ambaye alikuwa amewekwa na mfalme wa Babeli kuwa mtawala wa nchi.

Read More of Yeremia 41

Yeremia 42:1-22

Yeremia Ashauri Walionusurika Wasihame Yuda

42:1 Yer 40:13; 6:13; 41:11; 44:12Ndipo maafisa wote wa jeshi, pamoja na Yohanani mwana wa Karea, na Yezania mwana wa Hoshaya, na watu wote kuanzia aliye mdogo kabisa hadi aliye mkuu sana wakamjia 42:2 Mwa 20:7; Yak 5:16; Law 26:22; Mdo 8:24; Yer 36:7Yeremia nabii na kumwambia, “Tafadhali sikia maombi yetu na umwombe Bwana Mungu wako kwa ajili ya watu hawa wote waliosalia. Kwa kuwa kama unavyoona sasa, ingawa wakati fulani tulikuwa wengi, sasa tumesalia wachache tu. 42:3 Ezr 8:21; Za 86:11; Mit 3:6; Yer 15:11Omba ili Bwana Mungu wako atuambie twende wapi na tufanye nini.”

42:4 Kut 8:29; 1Sam 12:23; Hes 22:18; 1Fal 22:14; 1Sam 3:17Nabii Yeremia akajibu, “Nimewasikia. Kwa hakika nitamwomba Bwana Mungu wenu kama mlivyoomba. Nitawaambia kila kitu asemacho Bwana, wala sitawaficha chochote.”

42:5 Kum 4:26; 1Fal 22:16; Za 119:160; Rum 3:4; Yn 8:26; Mwa 31:48; Isa 1:2; Rum 1:9; Ufu 1:5Kisha wakamwambia Yeremia, “Bwana na awe shahidi wa kweli na mwaminifu kati yetu kama hatutafanya sawasawa na kila kitu Bwana Mungu wako atakachokutuma utuambie. 42:6 Kum 5:29; 6:3; Yer 7:23; 43:4; Mhu 3:2; Dan 11:4; 2Nya 34:24; Eze 36:36Likiwa jema au likiwa baya, tutamtii Bwana Mungu wetu, ambaye tunakutuma kwake, ili mambo yote yawe mema kwetu, kwa maana tutamtii Bwana Mungu wetu.”

Baada ya siku kumi, neno la Bwana likamjia Yeremia. 42:8 Ebr 8:11; Lk 7:28; Mk 9:35; Yer 4:16Kwa hiyo akawaita pamoja Yohanani mwana wa Karea, na maafisa wote wa jeshi waliokuwa pamoja naye na watu wote kuanzia mdogo kabisa hadi aliye mkuu sana. Akawaambia, “Hili ndilo asemalo Bwana, Mungu wa Israeli, ambaye mlinituma kuwasilisha maombi yenu: 42:10 Yer 24:6; Kum 30:6; Yer 31:28; 43:4; Mhu 3:2; Dan 11:4; 2Nya 34:24; Eze 36; 36‘Kama mkikaa katika nchi hii, nitawajenga wala sitawabomoa, nitawapanda wala sitawangʼoa, kwani ninahuzunishwa na maafa niliyowapiga nayo. 42:11 Eze 30:18; Hes 14:9; Yer 27:11; Ebr 7:25; Rum 8:31; Mit 20:22; 1Sam 15:24Msimwogope mfalme wa Babeli, ambaye sasa mnamwogopa. Msimwogope, asema Bwana, kwa kuwa niko pamoja nanyi, nami nitawaokoa na kuwaponya kutoka mikononi mwake. 42:12 Mwa 31:3; Neh 1:9; Za 106:45-46; Kut 3:21; 2Sam 24:14; 2Kor 1:3Nitawaonea huruma ili naye awe na huruma nanyi na kuwarudisha katika nchi yenu.’

42:13 Kum 11:28; Yer 44:16“Hata hivyo, kama mkisema, ‘Hatutakaa katika nchi hii,’ hivyo mkaacha kumtii Bwana Mungu wenu, 42:14 Kum 17:16; Isa 30:2; 65:13; Hes 11:4-5; Ay 6:20; Mt 24:31; 4:2-4; Mit 10:3nanyi kama mkisema, ‘Hapana, tutakwenda kuishi Misri, mahali ambapo hatutaona vita au kusikia sauti ya tarumbeta au kuwa na njaa ya chakula,’ basi sikieni neno la Bwana, enyi mabaki ya Yuda. Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: ‘Ikiwa mmekusudia kwenda Misri na kufanya makazi huko, 42:16 Law 26:33; Eze 14:17; 11:8; Yer 41:18; Mwa 41:55; 2:17; Ay 21:20; Eze 3:16; 18:4basi ule upanga mnaouogopa utawapata huko, na njaa mnayoihofia itawafuata huko Misri, nanyi mtafia huko. 42:17 Yer 21:7; 44:13; 24:10Naam, wote waliokusudia kwenda kuishi Misri watakufa kwa upanga, njaa na tauni; hakuna hata mmoja wao atakayenusurika au kuokoka maafa nitakayoyaleta juu yao.’ 42:18 Kum 29:18-20; 2Nya 12:7; 36:19; Yer 29:18; 39:1-9; 25:18; Hes 5:27; Za 44:13Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: ‘Kama vile hasira yangu na ghadhabu yangu ilivyomwagwa juu ya wale walioishi Yerusalemu, ndivyo ghadhabu yangu itakavyomwagwa juu yenu mtakapokwenda Misri. Mtakuwa kitu cha kulaania na cha kutisha, cha kulaumia na cha kushutumia, nanyi kamwe hamtaona mahali hapa tena.’

42:19 Kum 17:16; Isa 30:7; Yer 40:15; 43:2“Enyi mabaki ya Yuda, Bwana amewaambia, ‘Msiende Misri.’ Hakikisheni jambo hili: Ninawaonya leo 42:20 Eze 14:7-8kwamba mmefanya kosa kubwa mioyoni mwenu mliponituma kwa Bwana Mungu wenu na kusema, ‘Mwombe Bwana Mungu wetu kwa ajili yetu, nawe utuambie kila kitu atakachosema, nasi tutafanya.’ 42:21 Zek 7:11-12; Yer 40:3; Eze 2:7; 12:2; Kut 24:7Nimewaambieni leo, lakini bado ninyi hamtaki kumtii Bwana Mungu wenu katika yote aliyonituma niwaambie. 42:22 Yer 24:10; Eze 6:11; Isa 1:28; Yer 15:2; Hos 6:9Basi sasa, hakikisheni jambo hili: Mtakufa kwa upanga, njaa na tauni mahali ambapo mnataka kwenda kuishi.”

Read More of Yeremia 42