Yeremia 11:18-23, Yeremia 12:1-17, Yeremia 13:1-27 NEN

Yeremia 11:18-23

Shauri Baya Dhidi Ya Yeremia

Kwa sababu Bwana alinifunulia hila zao mbaya, nilizifahamu, kwa kuwa wakati ule alinionyesha yale waliyokuwa wanayafanya. 11:19 Za 54:3; Yer 20:10; Ay 28:13; Za 83:4; 44:22; Yer 18:18; Ay 28:13; Isa 53:8Nilikuwa kama mwana-kondoo mpole aliyeongozwa machinjoni; mimi sikutambua kwamba walikuwa wamefanya shauri baya dhidi yangu, wakisema,

“Sisi na tuuangamize mti na matunda yake;

nasi tumkatilie mbali kutoka nchi ya walio hai,

ili jina lake lisikumbukwe tena.”

11:20 Mdo 17:31; Za 7:8-9, 11; 1Sam 2:3; 1Nya 29:17; Za 58:10; Mao 3:60Lakini, Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, wewe uhukumuye kwa haki,

nawe uchunguzaye moyo na akili,

wacha nione ukiwalipiza wao kisasi,

kwa maana kwako nimeweka shauri langu.

11:21 Yer 12:6; Amo 2:12; Yer 38:4; Ay 21:18; Yer 21:7; 34:20; Isa 30:10“Kwa hiyo hili ndilo Bwana asemalo kuhusu watu wa Anathothi wale wanaotafuta uhai wako wakisema, ‘Usitoe unabii kwa jina la Bwana, la sivyo utakufa kwa mikono yetu’: 11:22 Isa 9:17; Yer 18:21kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote asemalo: ‘Nitawaadhibu. Vijana wao waume watakufa kwa upanga, wana wao na binti zao kwa njaa. 11:23 Lk 19:44; Yer 6:9; 23:12Hawatasaziwa hata mabaki kwao, kwa sababu nitaleta maafa kwa watu wa Anathothi katika mwaka wa adhabu yao.’ ”

Read More of Yeremia 11

Yeremia 12:1-17

Lalamiko La Yeremia

12:1 Ay 8:3; 12:6; Dan 9:14; Ay 21:7, 13; Ezr 9:15; Ay 5:8; Eze 18:25; Yer 5:27-28Wewe daima u mwenye haki, Ee Bwana,

niletapo mashtaka mbele yako.

Hata hivyo nitazungumza nawe kuhusu hukumu yako:

Kwa nini njia ya waovu inafanikiwa?

Kwa nini wasio waaminifu

wote wanaishi kwa raha?

12:2 Isa 29:13; Eze 22:27; Yer 11:17; Mk 7:6; Ay 5:3; Yer 3:10; Mt 15:8; Tit 1:16Umewapanda, nao wameota,

wanakua na kuzaa matunda.

Daima u midomoni mwao,

lakini mbali na mioyo yao.

12:3 Yer 17:18; Za 7:9; 11:5; Yer 20:11; 16:18Hata hivyo unanijua mimi, Ee Bwana;

unaniona na kuyachunguza mawazo yangu kukuhusu wewe.

Wakokote kama kondoo wanaokwenda kuchinjwa!

Watenge kwa ajili ya siku ya kuchinjwa!

12:4 Yer 4:25-28; Yoe 1:10-12; Kum 28:15-18; Za 107:34; Yer 4:26; 9:10Je, nchi itakaa katika hali ya kuomboleza mpaka lini,

na majani katika kila shamba kunyauka?

Kwa sababu wale waishio ndani yake ni waovu,

wanyama na ndege wameangamia.

Zaidi ya hayo, watu wanasema,

Bwana hataona yatakayotupata sisi.”

Jibu La Mungu

12:5 Yer 49:19; 50:44“Ikiwa umeshindana mbio na watu kwa mguu na wakakushinda,

unawezaje kushindana na farasi?

Ikiwa unajikwaa kwenye nchi ambayo ni salama,

utawezaje kwenye vichaka kando ya Yordani?

12:6 Mit 26:24-25; Yer 9:4; Za 12:2Ndugu zako, watu wa jamaa yako mwenyewe:

hata wao wamekusaliti;

wameinua kilio kikubwa dhidi yako.

Usiwaamini, ingawa wanazungumza

mema juu yako.

“Nitaiacha nyumba yangu,

nitupe urithi wangu;

nitamtia yeye nimpendaye

mikononi mwa adui zake.

12:8 Amo 6:8; 2Nya 36:16; Za 17:12; Hos 9:15Urithi wangu umekuwa kwangu

kama simba wa msituni.

Huningurumia mimi,

kwa hiyo ninamchukia.

12:9 Kum 28:26; Isa 56:9; Yer 15:3; Eze 23:25; 39:17-20Je, urithi wangu haukuwa

kama ndege wa mawindo wa madoadoa

ambaye ndege wengine wawindao

humzunguka na kumshambulia?

Nenda ukawakusanye pamoja wanyama wote wa mwituni;

walete ili wale.

12:10 Yer 25:34; Eze 33:2; Isa 5:1-7; Yer 9:10; 25:11Wachungaji wengi wataliharibu shamba langu la mizabibu

na kulikanyaga shamba langu;

watalifanya shamba langu zuri

kuwa jangwa la ukiwa.

12:11 Isa 42:25; Yer 23:10; Isa 5:6; 24:4; Yer 9:12; 14:4Litafanywa kuwa jangwa,

lililokauka na kuachwa ukiwa mbele zangu;

nchi yote itafanywa jangwa

kwa sababu hakuna hata mmoja anayejali.

12:12 Kum 32:41; Eze 33:2; Yer 3:2; Eze 21:3-4; Isa 31:8; Yer 46:10; Eze 14:17Juu ya miinuko yote ilivyo kama jangwani

mharabu atajaa,

kwa maana upanga wa Bwana utawala,

kuanzia ncha moja ya nchi hadi nyingine;

hakuna hata mmoja atakayekuwa salama.

12:13 Mik 6:15; Kut 15:7; Yer 4:26; Law 26:16-20; Kum 28:38Watapanda ngano lakini watavuna miiba;

watajitaabisha lakini hawatafaidi chochote.

Kwa hiyo beba aibu ya mavuno yako

kwa sababu ya hasira kali ya Bwana Mungu.”

12:14 Zek 2:7-9; Sef 2:8-10; Yer 32:37; 2Nya 7:20; Za 9:6; Kum 29:28Hili ndilo asemalo Bwana: “Kwa habari ya majirani zangu wote wabaya wanaonyangʼanya urithi ambao ninawapa watu wangu Israeli, nitawangʼoa kutoka nchi zao, nami nitaingʼoa nyumba ya Yuda kutoka katikati yao. 12:15 Kum 30:3; Amo 9:14-15; Eze 28:25; Za 6:2Lakini baada ya kuwangʼoa, nitawahurumia tena na kumrudisha kila mmoja wao kwenye urithi wake mwenyewe na kwenye nchi yake mwenyewe. 12:16 Yer 4:2; Yos 23:7; Efe 2:20; Isa 26:18; 49:6; Yer 18:8; 3:17Ikiwa watajifunza vyema njia za watu wangu na kuapa kwa Jina langu, wakisema, ‘Hakika kama Bwana aishivyo,’ hata kama wakati fulani walifundisha watu wangu kuapa kwa Baali, ndipo watakapofanywa imara katikati ya watu wangu. 12:17 Mwa 27:29; Isa 60:12; Za 2:8-9Lakini kama taifa lolote halitasikiliza na kutii, nitalingʼoa kabisa na kuliangamiza,” asema Bwana.

Read More of Yeremia 12

Yeremia 13:1-27

Mkanda Wa Kitani

Hili ndilo Bwana aliloniambia: “Nenda ununue mkanda wa kitani, ujivike kiunoni mwako, lakini usiuache uguse maji.” Kwa hiyo nikanunua mkanda, kama Bwana alivyoniagiza, nikajivika kiunoni.

13:3 Yer 33:1Ndipo neno la Bwana likanijia kwa mara ya pili: 13:4 Mwa 2:14“Chukua mkanda ulionunua ambao umeuvaa kiunoni mwako, uende sasa Frati uufiche ndani ya ufa mdogo kwenye mwamba.” 13:5 Kut 40:16Ndipo nikaenda na kuuficha ule mkanda huko Frati, kama Bwana alivyoniamuru.

Baada ya siku nyingi Bwana akaniambia, “Nenda sasa Frati ukauchukue ule mkanda niliokuambia uufiche huko.” 13:7 Isa 64:6; Yer 24:8; Mao 3:45Hivyo nikaenda Frati na kuuchimbua ule mkanda kutoka pale nilipokuwa nimeuficha, lakini sasa ulikuwa umeharibika na haufai tena kabisa.

Ndipo neno la Bwana likanijia: 13:9 Law 26:19; Mt 23:12; Lk 1:51“Hili ndilo Bwana asemalo: ‘Vivyo hivyo ndivyo nitakavyokiharibu kiburi cha Yuda na kiburi kikuu cha Yerusalemu. 13:10 Mhu 9:3; Yer 16:12; Kum 8:19; 9:14; 22:21; 3:17; Amu 10:13; Eze 15:3Watu hawa waovu, wanaokataa kusikiliza maneno yangu, wafuatao ukaidi wa mioyo yao na kufuata miungu mingine kuitumikia na kuiabudu, watakuwa kama mkanda huu ambao haufai kabisa! 13:11 Kut 19:5-6; Isa 63:12; 43:21; 65:12; Yer 33:9; 7:26; 32:20Kwa maana kama vile mkanda ufungwavyo kiunoni mwa mtu, ndivyo nilivyojifunga nyumba yote ya Israeli na nyumba yote ya Yuda,’ asema Bwana, ‘ili wawe watu wangu kwa ajili ya utukufu wangu, sifa na heshima yangu. Lakini hawajasikiliza.’

Viriba Vya Mvinyo

“Waambie: ‘Hili ndilo Bwana, Mungu wa Israeli, asemalo: kila kiriba inapasa kijazwe mvinyo.’ Kama wao wakikuambia, ‘Kwani hatujui kwamba kila kiriba inapasa kijazwe mvinyo?’ 13:13 Za 60:3; Isa 29:9; Eze 23:32-34; Za 75:8; Yer 25:18; 51:57Kisha uwaambie, ‘Hili ndilo asemalo Bwana: nitawajaza ulevi wote waishio katika nchi hii, pamoja na wafalme waketio juu ya kiti cha enzi cha Daudi, makuhani, manabii na wale wote waishio Yerusalemu. 13:14 Isa 9:17; Yer 16:5; Isa 9:19-21; Mao 2:21; Eze 7:4; Zek 11:6Nitawagonganisha kila mmoja na mwenzake, baba na wana wao, asema Bwana. Sitawarehemu wala kuwahurumia ili niache kuwaangamiza.’ ”

Tishio La Kutekwa

Sikieni na mzingatie,

msiwe na kiburi,

kwa kuwa Bwana amenena.

13:16 Yos 7:19; Law 26:37; 1Sam 2:9; Isa 59:9; Yer 23:12; Za 82:5Mpeni utukufu Bwana Mungu wenu,

kabla hajaleta giza,

kabla miguu yenu haijajikwaa

juu ya vilima vitakavyotiwa giza.

Mlitarajia nuru,

lakini ataifanya kuwa giza nene

na kuibadili kuwa huzuni kubwa.

13:17 Yer 14:18; Mal 2:2; Za 80:1; Yer 29:1Lakini kama hamtasikiliza,

nitalia sirini

kwa ajili ya kiburi chenu;

macho yangu yatalia kwa uchungu,

yakitiririka machozi,

kwa sababu kundi la kondoo la Bwana

litachukuliwa mateka.

13:18 Yer 21:11; Mao 5:16; 2Fal 24:18; 2:19; Eze 16:12Mwambie mfalme na mamaye,

“Shukeni kutoka kwenye viti vyenu vya enzi,

kwa kuwa taji zenu za utukufu

zitaanguka kutoka vichwani mwenu.”

13:19 Yer 52:30; Law 26:31; Yer 20:4Miji iliyoko Negebu itafungwa,

wala hapatakuwa na mtu wa kuifungua.

Watu wa Yuda wote watapelekwa uhamishoni,

wakichukuliwa kabisa waende mbali.

13:20 Yer 6:22; 23:2; Hab 1:6Inua macho yako uone

wale wanaokuja kutoka kaskazini.

Liko wapi lile kundi ulilokabidhiwa,

kondoo wale uliojivunia?

13:21 Za 41:9; Oba 1:7; Yer 4:30; 20:10; 38:22; 4:31Utasema nini Bwana atakapowaweka juu yako

wale ulioungana nao kama marafiki wako maalum?

Je, hutapatwa na utungu kama mwanamke

aliye katika utungu wa kuzaa?

13:22 Yer 9:2-6; 16:10-12; Nah 3:5-6; 1Fal 9:9; Isa 20:4; Eze 16:37; 23:26Nawe kama ukijiuliza,

“Kwa nini haya yamenitokea?”

Ni kwa sababu ya dhambi zako nyingi

ndipo marinda yako yameraruliwa

na mwili wako umetendewa vibaya.

Je, Mkushi aweza kubadili ngozi yake

au chui kubadili madoadoa yake?

Vivyo hivyo nawe huwezi kufanya mema

wewe uliyezoea kutenda mabaya.

13:24 Ay 27:21; 1:19; Law 26:33“Nitawatawanya kama makapi

yapeperushwayo na upepo wa jangwani.

13:25 Ay 20:29; Mt 24:51; Mik 3:11; Isa 17:10; Za 106:19-21Hii ndiyo kura yako,

fungu nililokuamuria,”

asema Bwana,

“kwa sababu umenisahau mimi

na kuamini miungu ya uongo.

13:26 Mao 1:6-8; Hos 2:10; Eze 16:37; Nah 3:5Nitayafunua marinda yako mpaka juu ya uso wako

ili aibu yako ionekane:

13:27 Yer 2:20; Eze 23:29; 6:13; Hos 8:5; Isa 57:7uzinzi wako na kulia kwako kama farasi kulikojaa tamaa,

ukahaba wako usio na aibu!

Nimeyaona matendo yako ya machukizo

juu ya vilima na mashambani.

Ole wako, ee Yerusalemu!

Utaendelea kuwa najisi mpaka lini?”

Read More of Yeremia 13