Isaya 43:1-28, Isaya 44:1-23 NEN

Isaya 43:1-28

Mwokozi Pekee Wa Israeli

43:1 Mwa 2:7; 32:28; Isa 45:3-4; Kut 6:6; Isa 42:6; 27:11; Ay 19:25Lakini sasa hili ndilo asemalo Bwana,

yeye aliyekuumba, ee Yakobo,

yeye aliyekuhuluku, ee Israeli:

“Usiogope kwa maana nimekukomboa,

nimekuita wewe kwa jina lako, wewe u wangu.

43:2 Mwa 26:3; Kum 31:6-8; Isa 30:27; 8:7; Dan 3:25-27; Kut 14:22; Isa 29:6Unapopita kwenye maji makuu,

nitakuwa pamoja nawe,

unapopita katika mito ya maji,

hayatakugharikisha.

Utakapopita katika moto,

hutaungua,

miali ya moto haitakuunguza.

43:3 Mit 21:18; Kut 30:2; Isa 20:3; Mwa 10:7; Eze 29:20; Za 68:31; Amu 2:18; Kut 14:30Kwa kuwa Mimi ndimi Bwana, Mungu wako,

yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli, Mwokozi wako.

Ninaitoa Misri kuwa fidia yako,

Kushi na Seba badala yako.

43:4 Isa 63:9; Ufu 3:9; Kut 19:5-6; Isa 49:5Kwa kuwa wewe ni wa thamani na wa kuheshimiwa machoni pangu,

nami kwa kuwa ninakupenda,

nitatoa watu badala yako

na mataifa badala ya maisha yako.

43:5 Isa 44:2; Mwa 21:22; Kut 14:22; Mdo 18:10; Yer 30:10-11; Mt 8:11; Zek 8:7; Isa 24:14Usiogope, kwa kuwa mimi nipo pamoja nawe,

nitawaleta watoto wako kutoka mashariki,

na kukukusanya kutoka magharibi.

43:6 Eze 16:61; 2Kor 6:18; Eze 36:24; Yer 23:8; Kum 30:4; Isa 60:4; 11:12Nitaiambia kaskazini, ‘Watoe!’

nayo kusini, ‘Usiwazuie.’

Walete wana wangu kutoka mbali,

na binti zangu kutoka miisho ya dunia:

43:7 Yak 2:7; Isa 29:23; Yer 15:16; Efe 2:10; Isa 56:5; 62:2; 63:19; Za 89:9kila mmoja ambaye ameitwa kwa Jina langu,

niliyemuumba kwa utukufu wangu,

niliyemhuluku na kumfanya.”

43:8 Isa 6:9-10; 42:20; Eze 12:2Uwaongoze wale wenye macho lakini hawaoni,

wenye masikio lakini hawasikii.

43:9 Isa 45:20; 48:14; 41:26Mataifa yote yanakutanika pamoja,

na makabila yanakusanyika.

Ni nani miongoni mwao aliyetangulia kutuambia haya,

na kututangazia mambo yaliyopita?

Walete mashahidi wao ili kuwathibitisha kuwa walikuwa sahihi,

ili wengine waweze kusikia, waseme, “Ni kweli.”

43:10 Isa 41:8-9; 19:21; Za 86:10; Yer 14:22; Yos 24:22; Kum 4:35; Isa 45:5-6, 14“Ninyi ni mashahidi wangu,” asema Bwana,

“na mtumishi wangu niliyemchagua,

ili mpate kunijua na kuniamini,

na kutambua kwamba Mimi ndiye.

Kabla yangu hakuna mungu aliyefanyizwa,

wala hatakuwepo mwingine baada yangu.

43:11 Isa 42:8; Za 18:31; Isa 25:9; 63:4; Kut 6:2Mimi, naam mimi, ndimi Bwana,

zaidi yangu hakuna mwokozi.

43:12 Kum 32:16; Za 81:9; Isa 44:8Nimedhihirisha, kuokoa na kutangaza:

Mimi, wala si mungu mgeni katikati yenu.

Ninyi ni mashahidi wangu,” asema Bwana,

“kwamba Mimi ndimi Mungu.

43:13 Hes 23:8; Ay 9:12; Za 90:2; Mit 8:23; Kum 32:39; Isa 48:12Naam, tangu siku za kale, Mimi ndiye.

Hakuna hata mmoja awezaye kuokoa

kutoka mkononi wangu.

Mimi ninapotenda,

ni nani awezaye kutangua?”

Huruma Za Mungu, Na Kukosa Uaminifu Kwa Israeli

43:14 Isa 13:14-15; 23:13; Kut 15:13; Ay 19:25; Isa 41:20Hili ndilo Bwana asemalo,

Mkombozi wako, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli:

“Kwa ajili yenu nitatumana Babeli

na kuwaleta Wakaldayo wote kama wakimbizi,

katika meli walizozionea fahari.

43:15 Isa 42:8; 27:11; 45:11; 41:21Mimi ndimi Bwana, yeye Aliye Mtakatifu wako,

Muumba wa Israeli, Mfalme wako.”

43:16 Kut 14:29; Za 77:19; Kut 15:8; Isa 11:15Hili ndilo asemalo Bwana,

yeye aliyefanya njia baharini,

mahali pa kupita kwenye maji mengi,

43:17 Za 118:12; Kut 14:4-9, 22; Za 76:5-6; Ay 13:25; Yer 51:21; Eze 38:4aliyeyakokota magari ya vita na farasi,

jeshi pamoja na askari wa msaada,

nao wakalala huko, wala hawatainuka tena kamwe,

wakakomeshwa, na wakazimika kama utambi:

43:18 Isa 41:22“Msiyakumbuke mambo yaliyopita,

wala msiyatafakari mambo ya zamani.

43:19 Hes 20:11; Yer 23:8-9; Ufu 21:5; Isa 40:3; 41:22; Yer 16:14-15; 2Kor 5:17; Isa 35:7Tazama, nitafanya jambo jipya!

Sasa litachipuka, je, hamtalitambua?

Nitafanya njia jangwani

na vijito vya maji katika nchi kame.

43:20 Hes 20:8; Isa 48:21; 41:17; Za 148:10; Isa 13:22Wanyama wa mwituni wataniheshimu,

mbweha na bundi,

kwa sababu ninawapatia maji jangwani,

na vijito katika nchi kame,

ili kuwapa watu wangu maji, wale niliowachagua,

43:21 Za 66:2; 1Pet 2:9; Mwa 2:7; Mal 3:17; Za 102:18watu wale niliowaumba kwa ajili yangu,

ili wapate kutangaza sifa zangu.

“Hata hivyo hukuniita mimi, ee Yakobo,

hujajitaabisha kwa ajili yangu, ee Israeli.

43:23 Zek 7:5-6; Kut 30:35; Yer 7:22; Amo 5:25; Kut 29:41; Mik 6:3; Mal 1:12-13Hujaniletea kondoo kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa,

wala kuniheshimu kwa dhabihu zako.

Sikukulemea kwa sadaka za nafaka

wala kukuchosha kwa kuhitaji uvumba.

43:24 Kut 30:23; Mal 2:17; Isa 7:13; Yer 8:21; Law 3:9; Yer 44:22Hukuninunulia uvumba wowote wenye manukato,

wala hukunipa kwa ukarimu

mafuta ya wanyama wa dhabihu zako.

Lakini umenilemea kwa dhambi zako,

na kunitaabisha kwa makosa yako.

43:25 2Sam 12:13; Lk 5:21; Eze 20:44; Yer 31:34; Ay 7:21; 2Nya 6:21; Isa 64:9“Mimi, naam mimi, ndimi nizifutaye dhambi zako,

kwa ajili yangu mwenyewe,

wala sizikumbuki dhambi zako tena.

43:26 Isa 1:18; 41:1; 49:25; 50:8Tafakari mambo yaliyopita,

njoo na tuhojiane,

leta shauri lako uweze kupewa haki yako.

43:27 Rum 5:12; Isa 28:7; Yer 5:31; Mwa 12:18; Isa 9:15; 24:20Baba yako wa kwanza alitenda dhambi,

wasemaji wako wameasi dhidi yangu.

43:28 Eze 5:15; Za 39:8; Hes 5:27; Kum 13:15; Isa 42:24; Zek 5:3; Yer 24:9Kwa hiyo nitawaaibisha wakuu wa Hekalu lako,

nami nitamtoa Yakobo aangamizwe,

na Israeli adhihakiwe.

Read More of Isaya 43

Isaya 44:1-23

Israeli Aliyechaguliwa

44:1 Yer 30:10; Isa 41:8-10; Mwa 16:11; Isa 14:1“Lakini sasa sikiliza, ee Yakobo, mtumishi wangu,

Israeli, niliyemchagua.

44:2 Hes 23:21; Kum 32:15; Za 149:2; 139:13; Isa 41:10; Yer 30:10; 46:27Hili ndilo asemalo Bwana,

yeye aliyekuhuluku, aliyekuumba tumboni,

yeye atakayekusaidia:

Usiogope, ee Yakobo, mtumishi wangu,

Yeshuruni,44:2 Yeshuruni hapa maana yake ni Yeye aliye mnyofu, yaani Israeli (ona pia Kum 32:15). niliyekuchagua.

44:3 Yn 4:10; Yoe 3:18; Isa 65:23; Yoe 2:28; Yn 7:37-39; Mit 9:5; Eze 36:27Kwa maana nitamimina maji juu ya nchi yenye kiu,

na vijito vya maji juu ya ardhi iliyokauka;

nitamimina Roho wangu juu ya watoto wako,

nayo baraka yangu juu ya wazao wako.

44:4 Law 23:40; Ay 40:22; 5:25; Za 72:16Nao watachipua kama manyasi katika shamba la majani,

kama mierezi kando ya vijito vya maji yatiririkayo.

44:5 Kut 13:9; Neh 9:38; Zek 13:9; 14:16; 8:20-22; Yer 50:5Mmoja atasema, ‘Mimi ni wa Bwana’;

mwingine atajiita kwa jina la Yakobo;

vilevile mwingine ataandika juu ya mkono wake, ‘Wa Bwana,’

na kujiita kwa jina la Israeli.

Ni Bwana, Siyo Sanamu

44:6 Ay 19:25; Isa 41:4; Ufu 22:13; Isa 43:10; 1Nya 17:20“Hili ndilo asemalo Bwana,

Mfalme wa Israeli na Mkombozi,

Bwana Mwenye Nguvu Zote:

Mimi ni wa kwanza na Mimi ni wa mwisho;

zaidi yangu hakuna Mungu.

44:7 Kum 32:39; Isa 41:22-26Ni nani basi aliye kama mimi? Yeye na atangaze.

Yeye atangaze na kuweka mbele yangu

ni kitu gani kilichotokea tangu nilipoumba watu wangu wa kale,

tena ni nini kitakachotokea:

naam, yeye na atoe unabii ni nini kitakachokuja.

44:8 Isa 43:10; Mwa 49:24; Kum 4:35; Isa 42:9Msitetemeke, msiogope.

Je, sikutangaza hili, na kutoa unabii tangu zamani?

Ninyi ni mashahidi wangu.

Je, yuko Mungu zaidi yangu mimi?

Hasha, hakuna Mwamba mwingine;

mimi simjui mwingine.”

44:9 Isa 41:24; Kum 4:28; Kut 20:4; Law 19:4; Isa 40:19; 1:29; Yer 22:22Wote wachongao sanamu ni ubatili,

navyo vitu wanavyovithamini havifai kitu.

Wale ambao wanazitetea ni vipofu,

ni wajinga, nao waaibika.

44:10 Yer 10:5; Mdo 19:24; Isa 41:29Ni nani atengenezaye mungu na kusubu sanamu,

ambayo haiwezi kumfaidia kitu chochote?

44:11 2Fal 19:18; Isa 42:17; 37:19; 1:29Yeye pamoja na wenziwe wa aina yake wataaibishwa,

mafundi wao si kitu ila ni wanadamu tu.

Wote wakusanyike pamoja na kuwa na msimamo wao,

watashushwa chini kwa hofu na kwa fedheha.

44:12 Isa 40:19; 54:16; Yer 10:3-5; Mdo 17:29; Isa 41:6-7; 40:28Muhunzi huchukua kifaa

na kukifanyia kazi kwenye makaa ya moto,

hutengeneza sanamu kwa nyundo,

huifanyiza kwa nguvu za mkono wake.

Huona njaa na kupoteza nguvu zake,

asipokunywa maji huzimia.

44:13 Isa 41:7; Za 115:4-7; Amu 17:4-5Seremala hupima kwa kutumia kamba

na huuchora mstari kwa kalamu;

huchonga kwa patasi

na kutia alama kwa bikari.

Huifanyiza katika umbo la binadamu,

la mwanadamu katika utukufu wake wote,

ili iweze kukaa katika sehemu yake ya ibada ya miungu.

44:14 Isa 41; 19Hukata miti ya mierezi,

huchukua mtiriza au mwaloni.

Huuacha ukue miongoni mwa miti ya msituni,

au hupanda msunobari, nayo mvua huufanya ukue.

44:15 Ufu 9:20; 2Nya 25:14Ni kuni ya binadamu:

yeye huchukua baadhi yake na kuota moto,

huwasha moto na kuoka mkate.

Lakini pia huutumia kumtengeneza mungu na akamwabudu,

huitengeneza sanamu na kuisujudia.

44:16 Isa 47:14Sehemu ya kuni huziweka motoni,

akapikia chakula chake,

hubanika nyama na kula hadi ashibe.

Huota moto na kusema,

“Aha! Ninahisi joto, ninaona moto.”

44:17 1Fal 18:26; Amu 10:14; Isa 47:15; Kut 20:5; Isa 45:20; 46:7Mabaki yake hutengeneza mungu, sanamu yake;

yeye huisujudia na kuiabudu.

Huiomba na kusema,

“Niokoe; wewe ni mungu wangu.”

44:18 Isa 16:12; Yer 4:22; Isa 29:10; Rum 11:8-10; Isa 6:9-10; Yer 10:8, 14-15Hawajui chochote, hawaelewi chochote,

macho yao yamefungwa hata hawawezi kuona,

akili zao zimefungwa hata hawawezi kufahamu.

44:19 Isa 45:20; Kum 27:15; Isa 5:13; 27:11; 40:20Hakuna anayefikiri,

hakuna mwenye maarifa wala ufahamu wa kusema,

“Sehemu yake nilitumia kwa kuni;

hata pia nilioka mkate juu ya makaa yake,

nikabanika nyama na kuila.

Je, nifanye machukizo kwa kile kilichobaki?

Je, nisujudie gogo la mti?”

44:20 Hos 4:12; Ay 15:31; 2Tim 3:13; Rum 1:25; Za 102; 9; 2The 2:11; Kum 4:28Hujilisha kwa majivu, moyo uliodanganyika humpotosha;

hawezi kujiokoa mwenyewe, au kusema,

“Je, kitu hiki kilichoko katika mkono wangu wa kuume si ni uongo?”

44:21 Isa 46:8; Zek 10:9; Za 27:10; Yer 31:20; Isa 49:15; 27:11“Ee Yakobo, kumbuka mambo haya,

ee Israeli, kwa kuwa wewe ni mtumishi wangu.

Nimekuumba wewe, wewe ni mtumishi wangu.

Ee Israeli, sitakusahau.

44:22 2Nya 6:21; Mdo 3:19; Mt 20:28; Mal 3:7; 2Sam 12:13; Ay 22:23; 1Kor 6:20Nimeyafuta makosa yako kama wingu,

dhambi zako kama ukungu wa asubuhi.

Nirudie mimi,

kwa kuwa nimekukomboa wewe.”

44:23 Za 98:4; Isa 42:10; Za 98:8; Yer 30:19; Isa 12:6; 1Nya 16:31; Za 65:13; Kut 16:7Enyi mbingu, imbeni kwa furaha,

kwa maana Bwana amefanya jambo hili.

Ee vilindi vya dunia, piga kelele.

Enyi milima, pazeni sauti kwa nyimbo,

enyi misitu na miti yenu yote,

kwa maana Bwana amemkomboa Yakobo,

ameuonyesha utukufu wake katika Israeli.

Read More of Isaya 44