Isaya 38:1-22, Isaya 39:1-8, Isaya 40:1-31 NEN

Isaya 38:1-22

Kuugua Kwa Mfalme Hezekia

(2 Wafalme 20:1-11; 2 Nyakati 32:24-26)

38:1 Isa 37:2-3; 2Sam 17:23; 2Fal 8:10Katika siku hizo Hezekia akaugua, naye akawa karibu kufa. Nabii Isaya mwana wa Amozi akaenda kwake na kumwambia, “Hili ndilo asemalo Bwana: Tengeneza mambo ya nyumba yako, kwa sababu utakufa, hutapona.”

Hezekia akaelekeza uso wake ukutani, akamwomba Bwana: 38:3 Neh 5:19; 13:14; Kum 6:18; Za 26:3; 1Fal 8:61; 2Nya 29:19; Za 6:8“Ee Bwana, kumbuka jinsi nilivyoenenda mbele zako kwa uaminifu na kujitoa kwa moyo wangu wote, na kufanya yaliyo mema machoni pako.” Naye Hezekia akalia kwa uchungu.

38:4 1Sam 13:13; Isa 39:5Ndipo neno la Bwana likamjia Isaya, kusema: 38:5 2Fal 18:2-3; Za 6:6“Nenda ukamwambie Hezekia, ‘Hili ndilo asemalo Bwana, Mungu wa baba yako Daudi: Nimeyasikia maombi yako na nimeona machozi yako. Nitakuongezea miaka kumi na mitano katika maisha yako. 38:6 Isa 31:5; 37:35Nami nitakuokoa wewe pamoja na mji huu mkononi mwa mfalme wa Ashuru. Nitaulinda mji huu.

38:7 Mwa 24:14; 2Fal 20:8; 2Nya 32:31; Isa 7:11, 14; 20:3“ ‘Hii ndiyo ishara ya Bwana kwako ya kwamba Bwana atafanya kile alichoahidi: 38:8 Yos 10:13Nitafanya kivuli cha jua kwenye ngazi iliyojengwa na Ahazi kirudi nyuma madaraja kumi.’ ” Hivyo jua likarudi nyuma madaraja kumi ambayo lilikuwa limeshuka.

Maandiko ya Hezekia mfalme wa Yuda baada ya kuugua kwake na kupona:

38:10 Ay 17:16; Za 102:24; 2Kor 1:9; Ay 17:11; Za 107:18Nilisema, “Katika ustawi wa maisha yangu,

je, ni lazima nipite katika malango ya mauti,38:10 Mauti hapa maana yake ni Kuzimu.

na kupokonywa miaka yangu iliyobaki?”

38:11 Za 27:13; Ay 28:13; 35:14; Isa 12:2; Za 116:5Nilisema, “Sitamwona tena Bwana,

Bwana katika nchi ya walio hai,

wala sitamtazama tena mwanadamu,

wala kuwa na wale ambao sasa wanakaa katika ulimwengu huu.

38:12 2Kor 5:4; Ay 4:21; Isa 33:20; Ebr 1:12; Hes 11:15; Za 32:4; 1Pet 1:13-14Kama hema la mchunga mifugo,

nyumba yangu imebomolewa na kutwaliwa kutoka kwangu.

Kama mfumaji nimevingirisha maisha yangu,

naye amenikatilia mbali kutoka kitanda cha mfumi.

Mchana na usiku uliyakomesha maisha yangu.

38:13 Ay 9:17; Mao 3:4; Yer 34:17; Za 37:7; 51:8; Ay 10:16; Dan 6:24Nilingoja kwa uvumilivu hadi mapambazuko,

lakini alivunja mifupa yangu yote kama simba.

Mchana na usiku uliyakomesha maisha yangu.

38:14 Isa 59:11; Mwa 50:24; Ay 17:3; Mwa 8:8; Za 6:7Nililia kama mbayuwayu au korongo,

niliomboleza kama hua aombolezaye.

Macho yangu yalififia nilipotazama mbinguni.

Ee Bwana, ninataabika, njoo unisaidie!”

38:15 Ay 7:11; 1Fal 21:27; Za 39:9; 2Sam 7:20Lakini niseme nini?

Amesema nami, naye yeye mwenyewe amelitenda hili.

Nitatembea kwa unyenyekevu

katika miaka yangu yote

kwa sababu ya haya maumivu makali

ya nafsi yangu.

38:16 Ebr 12:9; Za 119:25Bwana, kwa mambo kama haya watu huishi,

nayo roho yangu hupata uzima katika hayo pia.

Uliniponya

na kuniacha niishi.

38:17 Yer 31:34; Mik 7:19; Ay 17:16; Za 103:3, 12; Rum 8:28; Ebr 12:11; Isa 43:25Hakika ilikuwa ya faida yangu

ndiyo maana nikapata maumivu makali.

Katika upendo wako ukaniokoa

kutoka shimo la uharibifu;

umeziweka dhambi zangu zote

nyuma yako.

38:18 Mhu 9:10; Hes 16:30; Za 6:5; 30:9; 88:10-11; 115:17Kwa maana kaburi38:18 Kaburini hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol. haliwezi kukusifu,

mauti haiwezi kuimba sifa zako;

wale washukao chini shimoni

hawawezi kuutarajia uaminifu wako.

38:19 Kum 6:7; 11:19; Za 78:3; 118:7; 119:175Walio hai, walio hai: hao wanakusifu,

kama ninavyofanya leo.

Baba huwaambia watoto wao

habari za uaminifu wako.

38:20 Za 68:25; 9:13; 45:8; 116:17-19; 63:4; 23:6Bwana ataniokoa,

nasi tutaimba kwa vyombo vya nyuzi

siku zote za maisha yetu

katika Hekalu la Bwana.

Isaya alikuwa amesema, “Tengenezeni dawa ya kubandika ya tini, mweke juu ya jipu, naye atapona.”

Hezekia alikuwa ameuliza, “Kutakuwa na ishara gani kwamba nitapanda kwenda Hekalu la Bwana?”

Read More of Isaya 38

Isaya 39:1-8

Wajumbe Kutoka Babeli

(2 Wafalme 20:12-19)

39:1 2Fal 20:12; 2Nya 32:31Wakati huo Merodaki-Baladani, mwana wa Baladani mfalme wa Babeli, akamtumia Hezekia barua na zawadi, kwa sababu alikuwa amesikia habari za kuugua na kupona kwake. 39:2 2Nya 32:31; 2Fal 18:15; 2Nya 32:27-29Hezekia akawapokea wale wajumbe kwa furaha na kuwaonyesha vitu vile vilivyokuwa katika ghala zake: yaani fedha, dhahabu, vikolezo na mafuta safi, ghala la silaha lote, na kila kitu kilichokuwa katika hazina zake. Hapakuwa na kitu chochote katika jumba lake la kifalme au katika ufalme wake wote ambacho Hezekia hakuwaonyesha.

39:3 Kum 28:49Ndipo nabii Isaya akaenda kwa Mfalme Hezekia na kumuuliza, “Watu hao walisema nini, na wametoka wapi?”

Hezekia akamjibu, “Wametoka nchi ya mbali. Walikuja kwangu kutoka Babeli.”

Nabii akauliza, “Waliona nini katika jumba lako la kifalme?”

Hezekia akajibu, “Waliona kila kitu katika jumba langu la kifalme. Hakuna kitu chochote katika hazina yangu ambacho sikuwaonyesha.”

39:5 Isa 38:4Ndipo Isaya akamwambia Hezekia, “Sikia neno la Bwana Mwenye Nguvu Zote: 39:6 Law 26:33; Amu 6:4; Yer 20:5; Amo 5:27; 2Fal 24:13Hakika wakati unakuja ambapo vitu vyote katika jumba lako la kifalme, na vyote ambavyo baba zako waliweka akiba mpaka siku hii, vitachukuliwa kwenda Babeli. Hakuna chochote kitakachosalia, asema Bwana. 39:7 2Fal 24:15; Dan 1:1-7Nao baadhi ya wazao wako, nyama yako na damu yako mwenyewe watakaozaliwa kwako, watachukuliwa mbali, nao watakuwa matowashi katika jumba la mfalme wa Babeli.”

39:8 1Sam 3:18; 2Nya 32:26; Amu 10:15; Ay 1:21; Za 39:9Hezekia akamjibu Isaya, “Neno la Bwana ulilosema ni jema.” Kwa kuwa alifikiri, “Patakuwepo amani na usalama wakati wa uhai wangu.”

Read More of Isaya 39

Isaya 40:1-31

Faraja Kwa Watu Wa Mungu

40:1 Zek 1:17; 2Kor 1:3; Sef 3:14-17; Yer 31:13; Isa 49:13; 57:18Wafarijini, wafarijini watu wangu,

asema Mungu wenu.

40:2 Mwa 34:3; Isa 41:11-13; 49:25; Zek 9:12; Ufu 18:6; Yer 16:18; Law 26:4Sema na Yerusalemu kwa upole,

umtangazie

kwamba kazi yake ngumu imekamilika,

kwamba dhambi yake imefanyiwa fidia,

kwamba amepokea kutoka mkononi mwa Bwana

maradufu kwa ajili ya dhambi zake zote.

40:3 Isa 11:16; Mt 3:3; Mal 3:1; Mk 1:3; Isa 43:19; Yn 1:23Sauti ya mtu aliaye:

“Itengenezeni jangwani njia ya Bwana,

nyoosheni njia kuu nyikani

kwa ajili ya Mungu wetu.

40:4 Za 26:12; Yer 31:9; Isa 2:14; 49:11; 26:7; 45:2Kila bonde litainuliwa,

kila mlima na kilima kitashushwa;

penye mabonde patanyooshwa,

napo palipoparuza patasawazishwa.

40:5 Kut 16:7; Isa 58:14; Lk 3:4-6; Eze 36:23; Hes 14:21; Isa 59:19; Lk 2:20Utukufu wa Bwana utafunuliwa,

nao wanadamu wote watauona pamoja.

Kwa maana kinywa cha Bwana kimenena.”

40:6 Ay 14:2; Mwa 6:3; Isa 29:5Sauti husema, “Piga kelele.”

Nami nikasema, “Nipige kelele gani?”

“Wanadamu wote ni kama majani,

nao utukufu wao wote

ni kama maua ya kondeni.

40:7 Kut 15:10; Ay 41:21; Yos 8:12; Isa 15:6; Za 103:6; Eze 22:21Majani hunyauka na maua huanguka,

kwa sababu pumzi ya Bwana huyapuliza.

Hakika wanadamu ni majani.

40:8 1Pet 1:25; Isa 59:21; Mt 5:18; Za 119:89; Isa 5:24; Yak 1:10; Mit 19:21Majani hunyauka na maua huanguka,

lakini neno la Mungu wetu ladumu milele.”

40:9 Nah 1:15; Isa 25:9; Rum 10:15; Isa 41:27; 52:7-10; 1Kor 15:1-4Wewe uletaye habari njema Sayuni,

panda juu ya mlima mrefu.

Wewe uletaye habari njema Yerusalemu,

inua sauti yako kwa kupiga kelele,

inua sauti, usiogope;

iambie miji ya Yuda,

“Yuko hapa Mungu wenu!”

40:10 Ufu 22:7; Isa 35:4; Za 44:3; Isa 9:6-7; Ufu 22:12; Mt 21:5; Isa 28:2Tazameni, Bwana Mwenyezi anakuja na nguvu,

nao mkono wake ndio utawalao kwa ajili yake.

Tazameni, ujira wake u pamoja naye,

nayo malipo yake yanafuatana naye.

40:11 Za 28:9; Yn 10:11; Ebr 13:20; Mwa 48:15; Mik 5:4; Hes 12:11; Kum 26:19Huchunga kundi lake kama mchungaji wa mifugo:

Hukusanya wana-kondoo katika mikono yake

na kuwachukua karibu na moyo wake,

huwaongoza taratibu wale wanyonyeshao.

40:12 Mit 30:4; Ebr 1:10-12; Ay 38:10; 12:15; Mit 16:11Ni nani aliyepima maji ya bahari

kwenye konzi ya mkono wake,

au kuzipima mbingu kwa shibiri40:12 Shibiri ni sawa na sentimita 20 au inchi 8. yake?

Ni nani aliyeyashika mavumbi ya dunia katika kikapu,

au kupima milima kwenye kipimio

na vilima kwenye mizani?

40:13 Ay 15:8; 1Kor 2:16; Rum 11:34Ni nani aliyeyafahamu mawazo ya Bwana,

au kumfundisha akiwa kama mshauri wake?

40:14 Ay 21:22; Kol 2:3; Ay 12:13; 34:13; Isa 55:9Ni nani ambaye Bwana ametaka shauri kwake ili kumwelimisha,

naye ni nani aliyemfundisha njia iliyo sawa?

Ni nani aliyemfundisha maarifa

au kumwonyesha mapito ya ufahamu?

40:15 Za 62:9; Isa 2:22; Kum 9:21Hakika mataifa ni kama tone ndani ya ndoo,

ni kama vumbi jembamba juu ya mizani,

huvipima visiwa kana kwamba vilikuwa vumbi laini.

40:16 Mik 6:7; Ebr 10:5-9; Isa 37:24; Za 50:9-11Lebanoni hautoshi kwa moto wa madhabahuni,

wala wanyama wake hawatoshi kwa sadaka za kuteketezwa.

40:17 Isa 30:28; Ay 12:19; Isa 29:7; Dan 4:35; Isa 37:19Mbele yake mataifa yote ni kama si kitu,

yanaonekana yasio na thamani

na zaidi ya bure kabisa.

40:18 Mdo 17:29; Kut 8:10; Kum 4:15; 1Sam 2:2Basi, utamlinganisha Mungu na nani?

Utamlinganisha na kitu gani?

40:19 Kut 20:4; Zek 10:2; Yer 10:3-4; Isa 31:7; 37:19; 42:17; Hab 2:18Kwa habari ya sanamu, fundi huisubu,

naye mfua dhahabu huifunika kwa dhahabu

na kuitengenezea mikufu ya fedha.

40:20 Isa 44:19; 5:3Mtu aliye maskini sana asiyeweza kuleta sadaka kama hii

huuchagua mti usiooza.

Humtafuta fundi stadi

wa kusimamisha sanamu ambayo haitatikisika.

40:21 Mdo 14:17; Rum 1:19; Isa 48:13; 51:13; 2Fal 19:25Je, hujui?

Je, hujasikia?

Je, hujaambiwa tangu mwanzo?

Je, hujafahamu tangu kuumbwa kwa dunia?

40:22 Hes 13:33; Ay 22:14; 36:29; 2Nya 6:18; Isa 48:13; Ay 26:7Anakaa kwenye kiti cha enzi juu ya duara ya dunia,

nao watu wakaao ndani yake ni kama panzi.

Huzitandaza mbingu kama chandarua,

na kuzitandaza kama hema la kuishi.

40:23 Ay 12:18; Isa 34:12; Za 107:40; Amo 2:3Huwafanya wakuu kuwa si kitu,

na kuwashusha watawala wa dunia hii kuwa kitu bure.

40:24 2Sam 22:16; Isa 11:4; Ay 5:3; 8:12; 18:16; 24:24; Isa 41:2, 16Mara baada ya kupandwa,

mara baada ya kutiwa ardhini,

mara baada ya kutoa mizizi yao ardhini,

ndipo huwapulizia nao wakanyauka,

nao upepo wa kisulisuli

huwapeperusha kama makapi.

40:25 Kum 4:15; Mdo 17:24-29; 1Nya 16:25; Isa 37:23“Utanilinganisha mimi na nani?

Au ni nani anayelingana nami?” asema yeye Aliye Mtakatifu.

40:26 Za 89:11-13; 2Fal 17:16; Neh 9:6; Isa 34:16; 51:6; Ay 9:4; Efe 1:19Inueni macho yenu mtazame mbinguni:

Ni nani aliyeumba hivi vyote?

Ni yeye aletaye nje jeshi la nyota moja baada ya nyingine

na kuziita kila moja kwa jina lake.

Kwa sababu ya uweza wake mkuu na nguvu zake kuu,

hakuna hata mojawapo inayokosekana.

40:27 Ay 6:29; Lk 18:7-8; Ay 27:2Kwa nini unasema, ee Yakobo,

nanyi ee Israeli, kulalamika,

“Njia yangu imefichwa Bwana asiione,

Mungu wangu hajali shauri langu?”

40:28 Kum 33:27; Za 90:2; Rum 11:33; Isa 37:16; 44:12; Za 147:5Je wewe, hufahamu?

Je wewe, hujasikia?

Bwana ni Mungu wa milele,

Muumba wa miisho ya dunia.

Hatachoka wala kulegea,

wala hakuna hata mmoja

awezaye kuupima ufahamu wake.

40:29 Isa 57:19; Yer 31:25; Mwa 18:14; Za 68:35; 119:28Huwapa nguvu waliolegea

na huongeza nguvu za wadhaifu.

40:30 Isa 9:17; Yer 9:21; Isa 5:27Hata vijana huchoka na kulegea,

nao vijana wanaume hujikwaa na kuanguka,

40:31 2Fal 6:33; Kut 19:4; Ebr 12:1-3; Mao 3:25; 2Kor 4:8-10, 16; Za 37:9; Isa 30:18bali wale wamtumainio Bwana

atafanya upya nguvu zao.

Watapaa juu kwa mbawa kama tai;

watapiga mbio wala hawatachoka,

watatembea kwa miguu wala hawatazimia.

Read More of Isaya 40