Isaya 20:1-6, Isaya 21:1-17, Isaya 22:1-25, Isaya 23:1-18 NEN

Isaya 20:1-6

Unabii Dhidi Ya Misri Na Kushi

20:1 2Fal 18:17; Yos 11:22; 13:3Katika mwaka ule ambao jemadari mkuu alitumwa na Mfalme Sargoni wa Ashuru, naye akaja mpaka Ashdodi, akaushambulia na kuuteka, 20:2 Zek 13:4; Mt 3:4; Isa 3:24; Eze 4:1-12; 24:17, 23; 1Sam 19:24; Isa 13:1; 1Fal 1:8; Mik 1:8wakati ule Bwana alisema kwa kinywa cha Isaya mwana wa Amozi. Akamwambia, “Vua nguo ya gunia kutoka mwilini mwako na viatu kutoka miguuni mwako.” Naye akafanya hivyo, akatembea huku na huko uchi, bila viatu.

20:3 Kut 3:12; Yer 7:25; Isa 8:18; 22:20; 41:8-9; Mwa 10:6; Mdo 21:11Kisha Bwana akasema, “Kama vile mtumishi wangu Isaya alivyotembea uchi na bila viatu kwa miaka mitatu, kama ishara na dalili mbaya dhidi ya nchi ya Misri na Kushi, 20:4 Yer 13:22-26; Isa 19:4; 47:3; Nah 3:5; Yer 46:19; 2Sam 10:4; Ay 12:17vivyo hivyo mfalme wa Ashuru atawaongoza mateka wa Wamisri, na watu wa uhamisho wa Kushi, uchi na bila viatu, vijana hata wazee, wakiwa matako wazi, kwa aibu ya Wamisri. 20:5 2Fal 18:21; Isa 31:1-3; 8:12; 30:5; Eze 29:16Wale waliotegemea Kushi na kujivunia Misri wataogopa na kuaibika. 20:6 Isa 10:3; 2:11Katika siku ile watu wanaoishi katika pwani hii watasema, ‘Tazama lililowapata wale tuliowategemea, wale tuliowakimbilia kwa msaada na wokovu kutoka mikononi mwa mfalme wa Ashuru! Tutawezaje basi kupona?’ ”

Read More of Isaya 20

Isaya 21:1-17

Unabii Dhidi Ya Babeli

Neno kuhusu Jangwa kando ya Bahari:

Kama upepo wa kisulisuli unaopita katika nchi hadi kusini,

mshambuliaji anakuja kutoka jangwani,

kutoka nchi inayotisha.

21:2 1Sam 24:13-16; Mwa 10:22; Za 60:3; Yer 49:34; Isa 22:6; 13:3; Yer 25:25Nimeonyeshwa maono ya kutisha:

Msaliti anasaliti, mteka nyara anateka nyara.

Elamu, shambulia! Umedi, izunguke kwa jeshi!

Nitakomesha huzuni zote alizosababisha.

21:3 Mwa 3:16; Yn 16:2; Ay 14:22; Za 48:6; Isa 26:17; Yer 30:6; Dan 7:28Katika hili mwili wangu umeteswa na maumivu,

maumivu makali ya ghafula yamenishika,

kama yale ya mwanamke mwenye utungu wa kuzaa.

Nimeduwazwa na lile ninalolisikia,

nimeshangazwa na lile ninaloliona.

21:4 Isa 7:4; 35:4; 13:8; Dan 5:9; Za 55:5Moyo wangu unababaika,

woga unanifanya nitetemeke,

gizagiza la jioni nililolitamani sana,

limekuwa hofu kuu kwangu.

21:5 Yer 25:16, 27; Dan 5:2-5; Isa 5:12; 23:7; Yer 46:3; 1Sam 1:21Wanaandaa meza,

wanatandaza mazulia,

wanakula, wanakunywa!

Amkeni, enyi maafisa,

zitieni ngao mafuta!

21:6 2Fal 9:17Hili ndilo Bwana analoniambia:

“Nenda, weka mlinzi,

na atoe taarifa ya kile anachokiona.

21:7 Amu 6:5; Isa 21:9Anapoona magari ya vita

pamoja na kundi la farasi,

wapanda punda au wapanda ngamia,

na awe macho, awe macho kikamilifu.”

21:8 Mik 7:7; Hab 2:1Naye mlinzi alipaza sauti,

“Mchana baada ya mchana, bwana wangu, ninasimama katika mnara wa ulinzi,

kila usiku ninakaa mahali pangu nilipoamriwa.

21:9 Isa 13:19; Ufu 14:8; Dan 5:30; Ufu 18:2; Yer 50:2; Isa 47:11; Yer 51:8Tazama, yuaja mtu anayepanda gari la vita

pamoja na kundi la farasi.

Naye anajibu:

‘Babeli umeanguka, umeanguka!

Vinyago vyote vya miungu yake

vimelala chini vikiwa vimevunjwa!’ ”

21:10 Yer 51:33; Mt 3:12; Mik 4:13; Isa 27:12; Hab 3:12Ee watu wangu, mliopondwa kwenye sakafu ya kupuria,

ninawaambia kile nilichokisikia

kutoka kwa Bwana Mwenye Nguvu Zote,

kutoka kwa Mungu wa Israeli.

Unabii Dhidi Ya Edomu

21:11 Mwa 32:3; 1Nya 1:30; Eze 35:2; Oba 1:1Neno kuhusu Duma:

Mtu fulani ananiita kutoka Seiri,

“Mlinzi, usiku utaisha lini?

Mlinzi, usiku utaisha lini?”

Mlinzi anajibu,

“Asubuhi inakuja, lakini pia usiku.

Kama ungeliuliza, basi uliza;

bado na urudi tena.”

Unabii Dhidi Ya Arabia

21:13 Isa 13:1; 2Nya 9:14; Mwa 10:7; 25:3; 1Nya 1:9Neno kuhusu Arabia:

Enyi misafara ya Wadedani,

mnaopiga kambi katika vichaka vya Arabia,

21:14 Mwa 25:15; Ay 6:19leteni maji kwa wenye kiu,

ninyi mnaoishi Tema,

leteni chakula kwa ajili ya wakimbizi.

21:15 Isa 13:14; 31:8Wanaukimbia upanga,

kutoka upanga uliochomolewa alani,

kutoka upinde uliopindwa,

na kutoka kwenye joto la vita.

21:16 Law 25:50; Mwa 25:13; 25:13; Isa 17:3; 16:14; Za 120:5; Law 25:50; Wim 1:5; Mwa 25:13Hili ndilo Bwana analoniambia: “Katika muda wa mwaka mmoja, kama vile mtumishi aliyefungwa na mkataba angeihesabu, majivuno yote ya Kedari yatafikia mwisho. 21:17 Hes 23:19; Kum 4:27; Isa 10; 19; 1:20; 16:14; Lk 21:33; 1Sam 15:29; Mt 24:35; Mk 13:31; 1Pet 1:25Wanaume wavutao pinde walionusurika, mashujaa wa Kedari, watakuwa wachache.” Bwana, Mungu wa Israeli, amesema.

Read More of Isaya 21

Isaya 22:1-25

Unabii Kuhusu Yerusalemu

22:1 Za 125:2; Yoe 3:2-14; Yos 2:8; Isa 13:1; Yer 48:38; 21:13Neno kuhusu Bonde la Maono:

Nini kinachokutaabisha sasa,

kwamba ninyi nyote mmepanda juu ya mapaa?

22:2 Isa 5:14; 32:13; Eze 22:5; Isa 21:5; 10:4; 2Fal 25:3Ewe mji uliojaa ghasia,

ewe mji wa makelele na sherehe!

Watu wenu waliokufa hawakuuawa kwa upanga,

wala hawakufa vitani.

22:3 Isa 13:14; 2Fal 25:6Viongozi wako wote wamekimbia pamoja,

wamekamatwa bila kutumia upinde.

Ninyi nyote mliokamatwa mlichukuliwa wafungwa pamoja,

mlikimbia wakati adui alipokuwa bado mbali.

22:4 Mao 1:16; Lk 19:41; Yer 9:1; Eze 21:6; Isa 15:3; Lk 19:41Kwa hiyo nilisema, “Geukia mbali nami,

niache nilie kwa uchungu.

Usijaribu kunifariji

juu ya maangamizi ya watu wangu.”

22:5 Amo 5:18-20; Es 3:15; Sef 1:15; Isa 2:12; Ay 40:12; 2Sam 22:43; Eze 8:17-18; 13:14; Mao 1:5Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, anayo siku

ya ghasia, ya kukanyaga, na ya kuogofya

katika Bonde la Maono,

siku ya kuangusha kuta

na ya kupiga kelele mpaka milimani.

22:6 Isa 21:2; 2Fal 16:9; Yer 51:56; 49:35; Za 46:9Elamu analichukua podo,

pamoja na waendesha magari ya vita na farasi.

Kiri anaifungua ngao.

22:7 Yos 15:18; 2Nya 32:1-2Mabonde yako yaliyo mazuri sana yamejaa magari ya vita,

nao wapanda farasi wamewekwa kwenye malango ya mji;

22:8 2Nya 32:5; 1Fal 7:2; Isa 2:12ulinzi wa Yuda umeondolewa.

Nawe ulitazama siku ile

silaha katika Jumba la Kifalme la Mwituni,

22:9 2Fal 18:17; 2Nya 32:4-5; Wim 4:4; 2Fal 20:20mkaona kuwa Mji wa Daudi

una matundu mengi katika ulinzi wake,

mkaweka akiba ya maji

kwenye Bwawa la Chini.

22:10 Yer 33:4; 2Nya 32:15; 32:5; Yer 33:4Mlihesabu majengo katika Yerusalemu

nanyi mkabomoa nyumba ili kuimarisha ukuta.

22:11 Yer 39:4; Neh 3:16; 2Fal 25:4; 19:25; 1Sam 12:24Mlijenga bwawa la maji katikati ya kuta mbili

kwa ajili ya maji ya Bwawa la Zamani,

lakini hamkumtazama Yule aliyelitengeneza,

au kuwa na heshima kwa Yule aliyeubuni tangu zamani za kale.

22:12 Yoe 2:17; Law 13:40; Mik 1:16; Isa 3:24; Yoe 1:9-13Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote,

aliwaita siku ile

ili kulia na kuomboleza,

kungʼoa nywele zenu na kuvaa nguo ya gunia.

22:13 Mhu 8:15; Isa 5:12; 21:5; Lk 17:26-29; 1Kor 15:32; 1Sam 25:36; Isa 28:7-8Lakini tazama, kuna furaha na sherehe,

kuchinja ngʼombe na kuchinja kondoo,

kula nyama na kunywa mvinyo!

Mnasema, “Tuleni na kunywa,

kwa kuwa kesho tutakufa!”

22:14 Eze 24:13; Isa 5:9; 1Sam 2:25; Isa 13:11; 30:13-14; 1Sam 3:14Bwana Mwenye Nguvu Zote amelifunua hili nikiwa ninasikia: Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, asema: “Mpaka siku ya kufa kwenu, dhambi hii haitafanyiwa upatanisho.”

22:15 2Fal 6:30; 18:18; Mwa 41:40; Isa 36:3; 1Fal 4:6Hili ndilo Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, asemalo:

“Nenda ukamwambie huyu wakili Shebna,

ambaye ni msimamizi wa jumba la kifalme:

22:16 Mt 27:60; Hes 32:42Unafanya nini hapa, na ni nani aliyekupa ruhusa

kujikatia kaburi lako mwenyewe,

ukichonga kaburi lako mahali palipo juu,

na kutoboa kwa patasi mahali pako pa kupumzikia katika mwamba?

22:17 Yer 10:18; 13:18; 22:26“Jihadhari, Bwana yu karibu kukukamata thabiti,

na kukutupa mbali, ewe mtu mwenye nguvu.

22:18 Ay 18:11; Isa 14:19; Mwa 41:43Atakuvingirisha uwe kama mpira

na kukutupa katika nchi kubwa.

Huko ndiko utakakofia,

na huko ndiko magari yako ya vita ya fahari yatabakia,

wewe unayeifedhehesha nyumba ya bwana wako!

22:19 Za 52:5; Lk 16:3Nitakuondoa kutoka kazi yako,

nawe utaondoshwa kutoka nafasi yako.

22:20 2Fal 18:18“Katika siku ile, nitamwita mtumishi wangu, Eliakimu mwana wa Hilkia. 22:21 Ay 29:16Nitamvika joho lako, nami nitamfunga mshipi wako kiunoni mwake, na kumkabidhi mamlaka yako. Yeye atakuwa baba kwa wale wanaoishi Yerusalemu na kwa nyumba ya Yuda. 22:22 1Nya 9:27; Mt 16:19; Ay 12:14; Ufu 3:7; Isa 7:2Nitaweka mabegani mwake ufunguo wa nyumba ya Daudi. Kile afunguacho hakuna awezaye kufunga, na kile afungacho hakuna awezaye kufungua. 22:23 Eze 15:3; Zek 10:4; Ezr 9:8; Ay 6:25; 1Sam 2:7-8; Ay 36:7Nitamgongomea kama kigingi kilicho mahali palipo imara, naye atakuwa kiti cha enzi cha heshima kwa ajili ya nyumba ya baba yake. Utukufu wote wa jamaa yake utakuwa juu yake: Watoto wa jamaa hiyo na machipukizi yake, vyombo vyake vyote vidogo, tangu bakuli hadi magudulia yote.”

22:25 Isa 46:11; Mik 4:4Bwana Mwenye Nguvu Zote asema, “Katika siku ile, kigingi kilichogongomewa mahali imara kitaachia njia. Kitakatwa, nacho kitaanguka na mzigo ulioningʼinia juu yake utaanguka chini.” Bwana amesema.

Read More of Isaya 22

Isaya 23:1-18

Unabii Kuhusu Tiro

23:1 Zek 9:2-4; Amo 1:9-10; Eze 26:1-21; Mwa 10:4; 1Fal 10:22; Yos 19:29; Yer 47:4Neno kuhusu Tiro:

Ombolezeni, enyi meli za Tarshishi!

Kwa kuwa Tiro imeangamizwa,

imeachwa bila nyumba wala bandari.

Kuanzia nchi ya Kitimu23:1 Kitimu hapa ni Kipro, kisiwa katika Bahari ya Mediterania.

neno limewajia.

23:2 Ay 2:13; Eze 27:1-24; Amu 1:31Nyamazeni kimya, enyi watu wa kisiwani,

pia ninyi wafanyabiashara wa Sidoni,

ambao mabaharia wamewatajirisha.

23:3 Isa 19:7; Za 83:7; Eze 27:3; Mwa 41:5Kwenye maji makuu

nafaka za Shihori zilikuja;

mavuno ya Naili yalikuwa mapato ya Tiro,

naye akawa soko la mataifa.

23:4 Mwa 10:15, 19Uaibishwe ee Sidoni, nawe ee ngome la bahari,

kwa kuwa bahari imesema:

“Sijapata kuwa na uchungu wa kuzaa wala sijapata kuzaa,

wala sijapata kulea wana wala kutunza mabinti.”

23:5 Eze 30:9; 26:17-18Habari ifikapo Misri,

watakuwa katika maumivu makuu kwa ajili ya taarifa kutoka Tiro.

23:6 Mwa 10:4Vukeni mpaka Tarshishi,

ombolezeni, enyi watu wa kisiwani.

23:7 Isa 5:14; 32:13; 22:2; Eze 26:13; Isa 23:12Je, huu ndio mji wenu uliojaa sherehe,

mji wa zamani, zamani kabisa

ambao miguu yake imeuchukua

kufanya makao nchi za mbali sana?

23:8 Isa 2:12; Eze 28:2; 1Tim 3:4; Nah 3:16; Eze 28:5; Ufu 18:23Ni nani amepanga hili dhidi ya Tiro,

mji utoao mataji,

ambao wafanyabiashara wake ni wana wa mfalme

na wachuuzi wake ni watu mashuhuri wa dunia?

23:9 Ay 40:11; Isa 13:11; 5:13; Eze 27:3; Isa 14:24; 9:15Bwana Mwenye Nguvu Zote ndiye alipanga jambo hili,

ili kukishusha kiburi cha utukufu wote

na kuwanyenyekesha wale wote

ambao ni mashuhuri duniani.

Ee Binti Tarshishi,

pita katika nchi yako kama vile Mto Naili

kwa kuwa huna tena bandari.

23:11 Kut 14:21; Eze 26:4; Zek 9:3-4; Za 46:6Bwana amenyoosha mkono wake juu ya bahari

na kuzifanya falme zake zitetemeke.

Ametoa amri kuhusu Kanaani

kwamba ngome zake ziangamizwe.

23:12 Ufu 18:22; Sef 3:14; Zek 2:10; Isa 37:22; Yer 14:17; Mao 2:13; Mwa 10:4Alisema, “Usizidi kufurahi,

ee Bikira Binti Sidoni, sasa umepondwa!

“Simama, vuka uende Kitimu;

hata huko hutapata pumziko.”

23:13 Isa 43:14; Yer 51:12; Za 74:14; Isa 18:6Tazama katika nchi ya Wakaldayo,

watu hawa ambao sasa hawaonekani kama wapo!

Waashuru wameifanya nchi hiyo

kuwa mahali pa viumbe wa jangwani.

Wamesimamisha minara yao ya vita kuuzunguka,

wameziteka ngome zake na kuziacha tupu

na kuufanya kuwa magofu.

23:14 Mwa 10:4; Isa 2:16; Eze 27:25; 1Fal 10:22Ombolezeni, enyi meli za Tarshishi;

ngome yenu imeangamizwa!

23:15 Yer 25:22; Za 90:10Wakati huo Tiro utasahauliwa kwa miaka sabini, muda wa maisha ya mfalme. Lakini mwisho wa miaka hiyo sabini, itakuwa kwa Tiro kama ilivyo katika wimbo wa kahaba:

23:16 Mit 7:10“Twaa kinubi, tembea mjini kote,

ewe kahaba uliyesahauliwa;

piga kinubi vizuri, imba nyimbo nyingi,

ili upate kukumbukwa.”

23:17 Kum 23:17-18; Mwa 10:15-19; Ufu 17:1; 18:3-9; Eze 16:26; Yer 25:26; Nah 3:4Mwishoni mwa miaka sabini, Bwana atashughulika na Tiro. Naye atarudia ajira yake ya ukahaba, na atafanya biashara yake na falme zote juu ya uso wa dunia. 23:18 Yos 6:17-19; Za 72:10; Zek 14:20-21; Isa 61:6; Mik 4:13; Kut 28:36; Isa 18:7; 60:5-9; Amo 1:9-10Lakini faida na mapato yake yatawekwa wakfu kwa Bwana; hayatahifadhiwa wala kufichwa. Faida zake zitakwenda kwa wale wakaao mbele za Bwana kwa ajili ya chakula tele na mavazi mazuri.

Read More of Isaya 23