Isaya 17:1-14, Isaya 18:1-7, Isaya 19:1-25 NEN

Isaya 17:1-14

Neno Dhidi Ya Dameski

17:1 Yer 49:23; Mdo 9:2; Kum 13:16; Zek 9:1; Mwa 14:15; Isa 25:2Neno kuhusu Dameski:

“Tazama, Dameski haitakuwa tena mji

bali itakuwa lundo la magofu.

17:2 Yer 7:33; Mik 4:4; Isa 5:17; 2Fal 10:33; Isa 7:21; 27:10; Eze 25:5; Law 26:6Miji ya Aroeri itaachwa

na itaachiwa mifugo ambayo italala huko,

bila yeyote wa kuyaogopesha.

17:3 Isa 7:8, 16; 21:16; Hos 9:11; Isa 8:4; Hos 10:14; Isa 25:2, 12Mji wenye ngome utatoweka kutoka Efraimu,

nao uweza wa ufalme kutoka Dameski;

mabaki ya Aramu yatakuwa

kama utukufu wa Waisraeli,”

asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.

17:4 Isa 2:11; 10:16“Katika siku ile utukufu wa Yakobo utafifia,

unono wa mwili wake utadhoofika.

17:5 Yoe 3:13; Mt 13:30; Ufu 14:15-19; Isa 33:4; Yer 51:33; Ay 24:24; Yos 17:1517:5 Yos 17:15; 1Nya 11:15Itakuwa kama mvunaji akusanyavyo nafaka

na kuvuna nafaka kwa mikono yake,

kama wakati mtu aokotapo masazo ya masuke

katika Bonde la Warefai.

17:6 Kum 4:24; Isa 10:19; 27:12; 24:3Hata hivyo baadhi ya masazo yatabaki,

kama vile mti wa mzeituni unavyopigwa,

kukiachwa zeituni mbili au tatu juu ya matawi kileleni,

nne au tano katika matawi yazaayo sana,”

asema Bwana, Mungu wa Israeli.

17:7 Isa 9:13; 12:6; Zek 12:10; Mik 7:7; Isa 2:12; 10:20; Za 95:6Katika siku ile watu watamwangalia Muumba wao,

na kuelekeza macho yao kwa yule Aliye Mtakatifu wa Israeli.

17:8 2Nya 32:19; Ufu 9:20; 2Fal 17:10Hawataziangalia tena madhabahu,

kazi za mikono yao,

nao hawataheshimu nguzo za Ashera,17:8 Ashera hapa maana yake ni mungu mke aliyekuwa akiabudiwa pamoja na Baali.

na madhabahu za kufukizia uvumba zilizofanywa kwa mikono yao.

17:9 Isa 7:19Katika siku ile miji yao iliyo imara, ambayo waliihama kwa sababu ya Waisraeli, itakuwa kama mahali palipoachwa pa vichaka na magugu. Nayo yote itakuwa ukiwa.

17:10 Eze 22:12; Hos 8:14; Za 68:19; Kum 6:12; Yer 2:32; Za 50:22Mmemsahau Mungu Mwokozi wenu,

hamkumkumbuka Mwamba aliye ngome yenu.

Kwa hiyo, hata ingawa mlipandikiza mimea iliyo mizuri sana

na kuotesha mizabibu ya kigeni,

17:11 Za 90:6; Ay 4:8; Kum 28:39; Yer 10:19; 30:12; Law 26:30hata kama siku ile unapoipandikiza, unaifanya iote

na asubuhi ile ile unayoipanda, unaifanya ichipue,

hata hivyo mavuno yatakuwa kama si kitu

katika siku ile ya ugonjwa na maumivu yasiyoponyeka.

17:12 Yer 6:23; Lk 21:25; Isa 41:11; Za 18:4; 46:6; Isa 8:7-9Lo! Ghadhabu ya mataifa mengi,

wanaghadhibika kama bahari iliyochafuka!

Lo! Makelele ya mataifa

wanavuma kama ngurumo za maji mengi!

17:13 Kum 28:20; Isa 13:14; Ay 13:25; Dan 2:35; Za 65:7; 46:3; Ay 21:18Ingawa mataifa yanavuma kama ngurumo za maji yanayofanya mawimbi,

wakati anapoyakemea yanakimbia mbali,

yanafukuzwa mbele ya upepo kama makapi juu ya milima,

kama jani livingirishwapo na dhoruba.

17:14 2Fal 19:35; Amu 5:31; Isa 29:5; 30:13; 33:18; 54:14Wakati wa jioni, hofu ya ghafula!

Kabla ya asubuhi, wametoweka!

Hili ndilo fungu la wale wanaotupora,

fungu la wale wanaotunyangʼanya mali zetu.

Read More of Isaya 17

Isaya 18:1-7

Unabii Dhidi Ya Kushi

18:1 Mwa 10:6; Sef 2:12; Isa 5:8; Za 68:31; Eze 29:10; Oba 1:1Ole kwa nchi ya mvumo wa mabawa,18:1 Au: wa nzige.

kando ya mito ya Kushi,

18:2 Mwa 10:8-9; 2Nya 12:3; Kut 2:3; Ay 9:26; Mwa 41:14iwapelekayo wajumbe wake kwa njia ya bahari

kwa mashua za mafunjo juu ya maji.

Nendeni, wajumbe wepesi,

kwa taifa la watu warefu wenye ngozi nyororo,

kwa taifa linaloogopwa mbali na karibu,

taifa gomvi lenye lugha ngeni,

ambalo nchi yao imegawanywa kwa mito.

18:3 Za 60:4; Yer 4:21; Za 33:8; Isa 5:26; 5:26; 31:9; Yos 6:21; Amu 3:27Enyi mataifa yote ya ulimwengu,

ninyi mnaoishi duniani

wakati bendera itakapoinuliwa milimani,

mtaiona,

nayo tarumbeta itakapolia,

mtaisikia.

18:4 Hos 5:15; 2Sam 1:21; Za 133:3; Isa 64:12; 26:21; Amu 5:31; Za 18:12; Isa 26:19Hili ndilo Bwana aliloniambia:

“Nitatulia kimya na kutazama

kutoka maskani yangu,

kama joto linalometameta katika mwanga wa jua,

kama wingu la umande

katika joto la wakati wa mavuno.”

18:5 Isa 17:10-11; Eze 17:6; Isa 10:33Kwa maana, kabla ya mavuno,

wakati wa kuchanua ukishapita

na maua yakawa zabibu zinazoiva,

atayakata machipukizi kwa mundu wa kupogolea matawi,

naye atakata na kuyaondoa matawi yaliyopanuka.

18:6 Yer 7:33; Eze 32:4; 39:17; Isa 37:36; 8:8; 56:9Yote yataachwa kwa ajili ya ndege wawindao wa mlimani

na wanyama pori,

ndege watajilisha juu yake wakati wote wa kiangazi,

nao wanyama pori wakati wote wa masika.

18:7 Sef 3:10; Za 68:31; 2Nya 9:24; Isa 60:7; Mwa 41:4; 41:14Wakati huo matoleo yataletwa kwa Bwana Mwenye Nguvu Zote

kutoka kwa taifa la watu warefu wenye ngozi nyororo,

kutoka kwa taifa linaloogopwa mbali na karibu,

kutoka taifa gomvi lenye lugha ngeni,

ambalo nchi yao imegawanywa kwa mito,

matoleo yataletwa katika Mlima Sayuni, mahali pa Jina la Bwana Mwenye Nguvu Zote.

Read More of Isaya 18

Isaya 19:1-25

Unabii Kuhusu Misri

19:1 Yer 43:12; Yoe 3:19; Kut 12:12; 2Sam 22:10; Yos 2:11; Isa 20:3; Kum 10:14; Isa 13:1Neno kuhusu Misri:

Tazama, Bwana amepanda juu ya wingu liendalo kwa haraka

naye anakuja Misri.

Sanamu za Misri zinatetemeka mbele yake,

nayo mioyo ya Wamisri inayeyuka ndani yao.

19:2 Amu 7:22; 12:4; Mk 13:8; Mt 10:21, 36; 24:7; 2Nya 15:6; Lk 21:10“Nitamchochea Mmisri dhidi ya Mmisri,

ndugu atapigana dhidi ya ndugu,

jirani dhidi ya jirani,

mji dhidi ya mji,

ufalme dhidi ya ufalme.

19:3 Law 19:31; Dan 2:2, 10; Za 18:45; Ay 5:12; 2Nya 10:13; Isa 47:13Wamisri watakufa moyo,

na nitaibatilisha mipango yao.

Watatafuta ushauri kwa sanamu na kwa roho za waliokufa,

kwa waaguzi na kwa wale waongeao na mizimu.

19:4 Yer 46:26; Eze 32:11; 29:19; Isa 20:4Nitawatia Wamisri

mikononi mwa bwana mkatili

na mfalme mkali atatawala juu yao,”

asema Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote.

19:5 Isa 44:27; Yer 50:38; 2Sam 14:14Maji ya mito yatakauka,

chini ya mto kutakauka kwa jua.

19:6 Kut 7:18; Eze 30:12; Isa 37:25; 15:6; Mwa 41:2; Ay 8:11Mifereji itanuka;

vijito vya Misri vitapungua

na kukauka.

Mafunjo na nyasi vitanyauka,

19:7 Kum 29:23; Isa 23:3; Zek 10:11; Hes 11:5pia mimea iliyoko kando ya Mto Naili,

pale mto unapomwaga maji baharini.

Kila shamba lililopandwa kando ya Mto Naili litakauka,

litapeperushwa na kutoweka kabisa.

19:8 Hes 11:5; Amo 4:2; Hab 1:15; Eze 47:10Wavuvi watalia na kuomboleza,

wale wote watupao ndoano katika Mto Naili,

watadhoofika kwa majonzi.

19:9 Mit 7:16; Eze 16:10; 27:7; Yos 2:10Wale watu wafanyao kazi ya kitani kilichochambuliwa watakata tamaa,

wafumaji wa kitani safi watavunjika moyo.

Wafanyao kazi ya kufuma nguo watahuzunishwa,

nao vibarua wataugua moyoni.

19:11 Hes 13:22; 1Fal 4:30; Mdo 7:22; Mwa 41:37Maafisa wa Soani ni wapumbavu kabisa,

washauri wa Farao wenye busara wanatoa ushauri wa kijinga.

Unawezaje kumwambia Farao,

“Mimi ni mmojawapo wa watu wenye hekima,

mwanafunzi wa wafalme wa zamani”?

19:12 1Kor 1:20; Isa 41:22-23; Rum 9:17; Isa 14:24Wako wapi sasa watu wako wenye hekima?

Wao wakuonyeshe na kukufahamisha

ni nini Bwana Mwenye Nguvu Zote

amepanga dhidi ya Misri.

19:13 Yer 2:16; Hos 9:6; Hes 13:22; Yer 46:14-19; Eze 30:13-16; Za 118:22Maafisa wa Soani wamekuwa wapumbavu,

viongozi wa Memfisi19:13 Memfisi kwa Kiebrania ni Nofu. wamedanganyika,

walio mawe ya pembe ya taifa lake

wameipotosha Misri.

19:14 Mit 12:8; Mt 17:17; Za 107:27Bwana amewamwagia

roho ya kizunguzungu;

wanaifanya Misri iyumbayumbe

katika yale yote inayoyafanya,

kama vile mlevi ayumbayumbavyo

katika kutapika kwake.

19:15 Isa 9:14Misri haiwezi kufanya kitu chochote,

cha kichwa wala cha mkia,

cha tawi la mtende wala cha tete.

19:16 Isa 2:17; 11:10; Nah 3:13; Kum 2:25Katika siku ile Wamisri watakuwa kama wanawake. Watatetemeka kwa hofu mbele ya mkono wa Bwana Mwenye Nguvu Zote anaoinua dhidi yao. 19:17 Mwa 35:5; Isa 14:24Nayo nchi ya Yuda itawatia hofu Wamisri, kila mmoja atakayetajiwa Yuda ataingiwa na hofu, kwa sababu ya kile ambacho Bwana Mwenye Nguvu Zote anapanga dhidi yao.

19:18 Za 22:27; Yer 4:2; 43:13; Isa 10:20; 24:12; 32:19; Sef 3:9; Yer 44:1; Isa 48:1Katika siku hiyo miji mitano ya Misri, itazungumza lugha ya Kanaani, na kuapa kumtii Bwana Mwenye Nguvu Zote. Mji mmojawapo utaitwa Mji wa Uharibifu.19:18 Yaani Heliopoli (Mji wa Jua).

19:19 Yos 22:10; Kut 24:4; Za 68:18; Mwa 12:7; 28:18; Isa 10:20; Za 68:31Katika siku hiyo patakuwepo madhabahu ya Bwana katikati ya Misri na mnara wa kumbukumbu kwa Bwana kwenye mpaka wa Misri. 19:20 Isa 25:9; 49:24-26; Yos 4:20; Mwa 21:30; Amu 2:18; Kum 28:29Itakuwa alama na ushahidi kwa ajili ya Bwana Mwenye Nguvu Zote katika nchi ya Misri. Watakapomlilia Bwana kwa sababu ya watesi wao, Mungu atawapelekea mwokozi na mtetezi, naye atawaokoa. 19:21 Isa 11:9; 43:10; 56:7; Mwa 27:29; Za 86:9; Hes 30:2; Kum 23:21Hivyo Bwana atajijulisha mwenyewe kwa Wamisri, nao katika siku hiyo watamkubali Bwana. Wataabudu kwa kumtolea dhabihu na sadaka za nafaka, watamwekea Bwana nadhiri na kuzitimiza. 19:22 Kut 12:23; 11:10; Ebr 12:11; Eze 33:11; Yoe 2:13; Kum 32:39; Isa 45:14; Hos 10:2Bwana ataipiga Misri kwa tauni; atawapiga na kuwaponya. Watamgeukia Bwana, naye atayasikia maombi yao na kuwaponya.

19:23 Isa 11:15-16; 20:6; 27:13; 66:23; Mik 7:12; Mwa 27:29Katika siku hiyo kutakuwepo na njia kuu kutoka Misri hadi Ashuru. Waashuru watakwenda Misri, na Wamisri watakwenda Ashuru. Wamisri na Waashuru wataabudu pamoja. 19:24 Isa 11:11; Mwa 12:2Katika siku hiyo Israeli itakuwa ya tatu, pamoja na Misri na Ashuru, nao watakuwa baraka kwa dunia. 19:25 Za 87:4; 100:3; Efe 2:10; Kut 34:9; Yer 30:22; Hos 2:23; Mwa 12:3; Isa 29:23; 43:7Bwana Mwenye Nguvu Zote atawabariki, akisema, “Baraka iwe kwa Misri watu wangu, kwa Ashuru kazi ya mikono yangu, na kwa Israeli urithi wangu.”

Read More of Isaya 19