Isaya 1:1-31, Isaya 2:1-22 NEN

Isaya 1:1-31

1:1 1Sam 3:1; Hes 12:6; 2Fal 14:21; 16:1; 1Nya 3:12-13; 2Nya 26:22; 1Sam 22:1, 5; Oba 1:1; Nah 1:1; Isa 40:9; 44:26Maono kuhusu Yuda na Yerusalemu ambayo Isaya mwana wa Amozi aliyaona wakati wa utawala wa Uzia, Yothamu, Ahazi na Hezekia, wafalme wa Yuda.

Taifa Asi

1:2 Hag 1:12; Amu 11:10; Kum 4:26; Yer 42:5; Isa 23:4; 63:16; 65:2; Eze 24:3; Mik 1:2; Isa 63:16; Mal 1:6Sikieni, enyi mbingu! Sikilizeni, enyi dunia!

Kwa maana Bwana amesema:

“Nimewalisha watoto na kuwalea,

lakini wameniasi mimi.

1:3 Yer 4:22; 9:3-6; Hos 2:8; Ay 12:9; Mwa 42:27; Kum 32:28; Isa 42:25; Ay 12:9; Hos 4:1; Isa 48:8; Hos 4:6; 7:9Ngʼombe anamjua bwana wake,

naye punda anajua hori la mmiliki wake,

lakini Israeli hajui,

watu wangu hawaelewi.”

1:4 Yer 23:14; Eze 39:7; 2Fal 19:22; Isa 1:2; Za 14:3; Kum 32:15; Isa 5:19; 31:1; 5:18; 9:17; 14:20; Za 119:87Lo! Taifa lenye dhambi,

watu waliolemewa na uovu,

uzao wa watenda mabaya,

watoto waliozoelea upotovu!

Wamemwacha Bwana,

Wamemkataa kwa dharau

yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli

na kumgeuzia kisogo.

1:5 Yer 2:20; 30:17; 44:16-17; 2:30; 5:3; Ebr 3:16; Isa 31:6; 44:16-17; Mit 20:30; Mao 2:11Kwa nini mzidi kupigwa?

Kwa nini kudumu katika uasi?

Kichwa chako chote kimejeruhiwa,

moyo wako wote ni mgonjwa.

1:6 Kum 28:35; Yer 8:22; 14:19; 30:17; Mao 2:13; Eze 34:4; Lk 10:34; 2Sam 14:2; Za 45:7; 104:15; 38:3; Isa 61:3; 53:5; 30:26Kutoka wayo wako wa mguu hadi kwenye utosi wa kichwa chako

hakuna uzima:

ni majeraha matupu na makovu

na vidonda vitokavyo damu,

havikusafishwa au kufungwa

wala kulainishwa kwa mafuta.

1:7 Kum 28:51; Amu 6:3-6; Isa 62:8; 2Fal 18:13; Law 26:34; 26:16; Yer 5:17; Za 109:11Nchi yenu imekuwa ukiwa,

miji yenu imeteketezwa kwa moto;

nchi yenu imeachwa tupu na wageni

mbele ya macho yenu,

imeharibiwa kama vile imepinduliwa na wageni.

1:8 Za 9:14; Isa 10:32; 30:17; 49:21; Ay 27:18Binti Sayuni ameachwa kama kipenu

katika shamba la mizabibu,

kama kibanda katika shamba la matikitimaji,

kama mji uliohusuriwa.

1:9 Rum 9:29; 2Fal 21:14; Mwa 45:7; 19:24; Isa 4:2; 6:13; 27:12; Yer 23:3; Yoe 2:32Kama Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote1:9 Bwana Mwenye Nguvu Zote hapa ni Yehova Sabaoth, yaani Bwana wa Majeshi; pia Warumi 9:29 na Yakobo 5:4.

asingelituachia walionusurika,

tungelikuwa kama Sodoma,

tungelifanana na Gomora.

1:10 Isa 30:9; 28:14; 5:24; 8:20; 13:19; Ufu 11:8; Mwa 13:13; Eze 16:49; Rum 9:29Sikieni neno la Bwana,

ninyi watawala wa Sodoma;

sikilizeni sheria ya Mungu wetu,

enyi watu wa Gomora!

1:11 Amo 6:4; Yer 6:20; Ebr 10:4; Za 50:8; 40:6; Ay 22:3; Isa 66:3; 1Sam 15:22; Mal 1:10Bwana anasema, “Wingi wa sadaka zenu,

ni kitu gani kwangu?

Ninazo sadaka za kuteketezwa nyingi kupita kiasi,

za kondoo dume na mafuta ya wanyama walionona.

Sipendezwi na damu za mafahali

wala za wana-kondoo na mbuzi.

1:12 Kut 23:17; Kum 31:11Mnapokuja kujihudhurisha mbele zangu,

ni nani aliyewataka ninyi mfanye hivyo,

huku kuzikanyaga nyua zangu?

1:13 Mit 15:8; 1Nya 23:31; Hag 2:14; Yer 18:15; 44:8; 1Fal 11:24; Mit 28:9; Yer 7:9; Isa 41:24; 66:3Acheni kuniletea sadaka zisizokuwa na maana!

Uvumba wenu ni chukizo kwangu.

Miandamo ya Mwezi, Sabato na makusanyiko ya ibada:

siwezi kuvumilia makusanyiko yenu maovu.

1:14 Za 69:3; Kut 12:16; Mal 3:14; Kum 16:1-7; Neh 10:33; Ay 7:12; Hes 28:11-29; Law 23:1-44Sikukuu zenu za Miandamo ya Mwezi, na sikukuu zenu zilizoamriwa:

moyo wangu unazichukia.

Zimekuwa mzigo kwangu,

nimechoka kuzivumilia.

1:15 Ay 27:9; Kum 31:17; 1:45; Mik 3:4; Hos 4:2; Isa 57:17; 59:2; Kut 9:29; Yoe 3:21; 1Sam 8:18Mnaponyoosha mikono yenu katika maombi,

nitaficha macho yangu nisiwaone;

hata mkiomba maombi mengi

sitasikiliza.

Mikono yenu imejaa damu;

1:16 Yer 4:14; 25:5; Hes 19:11-16; Isa 52:11; Rut 3:3; Yak 4:8; Mt 27:24jiosheni na mkajitakase.

Yaondoeni matendo yenu maovu

mbele zangu!

Acheni kutenda mabaya,

1:17 Mik 6:8; Sef 2:3; Ay 22:9; Isa 33:5; Kut 22:22; Amo 5:14-15; Za 34:14; 72:1; Isa 11:4jifunzeni kutenda mema!

Tafuteni haki,

watieni moyo walioonewa.

Teteeni shauri la yatima,

wateteeni wajane.

1:18 1Sam 2:25; Isa 41:21; 55:7; Ufu 7:14; Za 51:7; Isa 43:9; 41:1; 43:26“Njooni basi tuhojiane,”

asema Bwana.

“Ingawa dhambi zenu ni kama rangi nyekundu,

zitakuwa nyeupe kama theluji;

ingawa ni nyekundu sana kama damu,

zitakuwa nyeupe kama sufu.

1:19 Ezr 9:12; Za 34:10; Ay 36:11; Isa 50:10; 62:9; Kum 30:15-16; Isa 58:14; 65:13; 30:32Kama mkikubali na kutii,

mtakula mema ya nchi,

1:20 Yer 17:27; Hes 23:19; Ay 15:22; 1Sam 12:15; Isa 3:25; 21:17; 34:16; 27:1; 65:12lakini kama mkikataa na kuasi,

mtaangamizwa kwa upanga.”

Kwa kuwa kinywa cha Bwana kimenena.

1:21 Isa 57:3-9; Yer 2:20; 3:2-9; 13:27; Eze 23:3; Hos 2:1-13; Amo 6:12; Isa 46:13; 59:14; Mit 6:17Tazama jinsi mji uliokuwa mwaminifu

umekuwa kahaba!

Mwanzoni ulikuwa umejaa unyofu,

haki ilikuwa inakaa ndani yake,

lakini sasa ni wauaji!

1:22 Za 119:119Fedha yenu imekuwa takataka,

divai yenu nzuri imechanganywa na maji.

1:23 Kum 19:14; Amo 5:8; Yer 5:28; Mik 2:1-2; 6:12; Kut 23:8; Isa 10:2; Eze 22:6-7; Isa 1:2; Mik 3:9; Amo 5:12; Hab 1:4Watawala wenu ni waasi,

rafiki wa wevi,

wote wanapenda rushwa

na kukimbilia hongo.

Hawatetei yatima,

shauri la mjane haliletwi mbele yao lisikilizwe.

1:24 Mwa 49:24; Isa 34:2, 8; 47:3; 59:17; 63:4; Yer 51:6; Eze 5:13; Kum 32:43Kwa hiyo Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote,

Mwenye Nguvu wa Israeli, asema hivi:

“Lo, nitapata faraja kutoka kwa adui zangu

na kujilipizia kisasi juu ya watesi wangu.

1:25 Yer 9:7; 6:29; Ufu 3:19; Isa 48:10; Kum 28:63; Za 78:38; 2Nya 29:15; Eze 22:22; Za 119:119Nitauelekeza mkono wangu dhidi yenu,

nitawasafisha takataka zenu zote

na kuwaondolea unajisi wenu wote.

1:26 Mik 4:8; Zek 8:3; Yer 31:23; 33:7; Kum 9:24; Mwa 32:28; Isa 32:16; 46:13; 4:3; 48:2Nitawarudishia waamuzi wenu kama ilivyokuwa siku za zamani,

nao washauri wenu kama ilivyokuwa mwanzoni.

Baadaye utaitwa,

Mji wa Haki,

Mji Mwaminifu.”

1:27 Isa 31:6; 59:20; 35:10; 41:14; 62:12; 63:4; 30:15; Hos 2:19; Eze 18:30Sayuni itakombolewa kwa haki,

wale waliomo ndani yake waliotubu kwa uaminifu.

1:28 Yer 4:18; 44:12; 2The 1:8-9; Isa 33:14; 43:27; 48:8; 16:2; Kum 32:18; 32:15; Za 9:5; Yer 16:4Lakini waasi na wenye dhambi wote wataangamizwa,

nao wanaomwacha Bwana wataangamia.

1:29 Eze 6:13; Hos 4:13; Isa 65:3; 42:17; 44:9; 57:5; Za 97:7; Yer 10:14; Za 97:7“Mtaaibika kwa sababu ya hiyo mialoni

ambayo mlifurahia,

mtafadhaika kwa sababu ya bustani

mlizozichagua.

1:30 Za 1:3Mtakuwa kama mwaloni wenye majani yanayonyauka,

kama bustani isiyokuwa na maji.

1:31 Isa 4:4; 5:24; 9:18-19; 24:6; 33:14; 66:15-16, 24; Yer 5:14; 7:20; Mal 3:2; Mt 25:41Mtu mwenye nguvu atatoweka kama majani makavu yawakayo moto,

na kazi yake kama cheche ya moto;

vyote vitaungua pamoja,

wala hakuna wa kuuzima huo moto.”

Read More of Isaya 1

Isaya 2:1-22

Mlima Wa Bwana

(Mika 4:1-3)

2:1 Isa 1:1Hili ndilo aliloliona Isaya mwana wa Amozi kuhusu Yuda na Yerusalemu:

2:2 Dan 2:35; 11:45; Yoe 3:17; Mdo 2:17; Isa 11:9; 65:9; Zek 14:10; Yer 16:19Katika siku za mwisho

mlima wa Hekalu la Bwana utaimarishwa

kama mlima mkuu miongoni mwa milima yote,

utainuliwa juu ya vilima,

na mataifa yote yatamiminika huko.

2:3 Zek 8:21; Lk 24:47; Yn 4:22; Isa 33:22; 45:23; Yer 3:17; Kum 33:19Mataifa mengi yatakuja na kusema,

“Njooni, twendeni mlimani mwa Bwana,

kwenye nyumba ya Mungu wa Yakobo.

Atatufundisha njia zake,

ili tuweze kuenenda katika mapito yake.”

Sheria itatoka Sayuni,

neno la Bwana litatoka Yerusalemu.

2:4 Hos 2:18; Yer 30:11; Za 96:13; 51:4; 46:9; Yoe 3:10; Mwa 49:10; Zek 9:10Atahukumu kati ya mataifa

na ataamua migogoro ya mataifa mengi.

Watafua panga zao ziwe majembe,

na mikuki yao kuwa miundu ya kukata matawi.

Taifa halitainua upanga dhidi ya taifa jingine,

wala hawatajifunza vita tena.

2:5 Isa 60:19-20; 1Yn 1:5-7; Isa 58:1; 60:1Njooni, enyi nyumba ya Yakobo,

tutembeeni katika nuru ya Bwana.

Siku Ya Bwana

2:6 Kum 18:10, 14; 31:17; Yer 12:7; 2Nya 16:7; Isa 44:25; 2Fal 16:7; Kum 31:17Umewatelekeza watu wako,

nyumba ya Yakobo.

Wamejaa ushirikina utokao Mashariki,

wanapiga ramli kama Wafilisti

na wanashikana mikono na wapagani.

2:7 Mwa 41:43; Kum 17:16; Mik 5:10; Za 17:14; Isa 31:1; Kum 17:17Nchi yao imejaa fedha na dhahabu,

hakuna mwisho wa hazina zao.

Nchi yao imejaa farasi,

hakuna mwisho wa magari yao.

2:8 Isa 10:9-11; 17:8; 44:17; Ufu 9:20; 2Nya 32:19; Mik 5:13; Isa 44:17; Za 135:15Nchi yao imejaa sanamu,

wanasujudia kazi za mikono yao,

vitu vile vidole vyao vimevitengeneza.

2:9 Za 62:9; Isa 13:11; 5:15; 2:11, 17; Hes 4:5; Neh 4:5Kwa hiyo mwanadamu atashushwa

na binadamu atanyenyekezwa:

usiwasamehe.

2:10 Ufu 6:15-16; Nah 3:11; Za 145:12; Isa 2:19; 2The 1:9Ingieni kwenye miamba,

jificheni ardhini

kutokana na utisho wa Bwana

na utukufu wa enzi yake!

2:11 Isa 24:21-23; 37:23; 10:12; 5:15; Eze 31:10; Oba 1:8; Neh 9:29; Ay 40:11; Za 46:10; Hab 2:5Macho ya mtu mwenye majivuno yatanyenyekezwa

na kiburi cha wanadamu kitashushwa,

Bwana peke yake ndiye atakayetukuzwa siku hiyo.

2:12 Za 76:12; 59:12; Eze 7:7; Ay 40:11; Isa 13:6-9; 34:8; Yer 30:7; Mao 1:12; 2Sam 22:28; Yoe 1:15; Amo 5:18Bwana Mwenye Nguvu Zote anayo siku aliyoiweka akiba

kwa wote wenye kujivuna na wenye kiburi,

kwa wote wanaojikweza

(nao watanyenyekezwa),

2:13 Amu 9:15; Isa 10:33, 34; 29:17; Eze 27:5; Za 22:12; Zek 11:2kwa mierezi yote ya Lebanoni iliyo mirefu sana,

na mialoni yote ya Bashani,

2:14 Isa 30:25; 40:4kwa milima yote mirefu

na vilima vyote vilivyoinuka,

2:15 Isa 25:2, 12; 30:25; 32:14; 33:18; Sef 1:16kwa kila mnara ulio mrefu sana

na kila ukuta wenye ngome,

2:16 Mwa 10:4; 1Fal 10:22; 9:26kwa kila meli ya biashara,2:16 Au: ya Tarshishi (ona pia 1Fal 10:22; 22:48; 2Nya 9:21; 20:36; Isa 60:9.)

na kila chombo cha baharini cha fahari.

2:17 2Sam 22:28; Ay 40:112:17 Nah 3:13; Ebr 10:31; Kum 2:25; Isa 11:10, 15Majivuno ya mwanadamu yatashushwa,

na kiburi cha wanadamu kitanyenyekezwa,

Bwana peke yake ndiye atatukuzwa siku hiyo,

2:18 Kum 9:21; Mik 5:13; Eze 36:25; Isa 21:9; Yer 10:11; 1Sam 5:2nazo sanamu zitatoweka kabisa.

2:19 Hos 10:8; Nah 1:3-6; Ay 9:6; 30:9; Ebr 12:26; Hab 3:6; Amu 6:2; Isa 7:19; 14:16; Ay 30:6; Lk 23:30; Ufu 6:15Watu watakimbilia kwenye mapango ndani ya miamba,

na kwenye mahandaki ardhini

kutokana na utisho wa Bwana

na utukufu wa enzi yake,

ainukapo kuitikisa dunia.

2:20 Law 11:19; Eze 36:25; 7:19-20; 14:6; Ufu 9:20; Isa 2:11; Ay 22:24Siku ile, watu watawatupia

panya na popo

sanamu zao za fedha na za dhahabu,

walizozitengeneza ili waziabudu.

2:21 Kut 33:22; Za 145:12; Isa 33:10; 2:19Watakimbilia kwenye mapango miambani

na kwenye nyufa za miamba

kutokana na utisho wa Bwana

na utukufu wa enzi yake,

ainukapo kuitikisa dunia.

2:22 Mit 23:4; Yer 17:5; Yak 4:14; Ay 12:19; Za 119:8-9; Isa 51:12; 40:15; Za 18:42; 118:6, 8; 146:3Acheni kumtumainia mwanadamu,

ambaye hana kitu ila pumzi katika pua zake.

Yeye ana thamani gani?

Read More of Isaya 2