Hosea 11:1-12, Hosea 12:1-14, Hosea 13:1-16, Hosea 14:1-9 NEN

Hosea 11:1-12

Upendo Wa Mungu Kwa Israeli

11:1 Kut 4:22; Mt 2:15; Yer 2:2; Eze 16:22; Hos 12:9; 13:4“Wakati Israeli alipokuwa mtoto, nilimpenda,

nilimwita mwanangu kutoka Misri.

11:2 Hos 2:13; 4:13; 2Fal 17:15; Isa 65:7; Yer 18:15Lakini kadiri nilivyomwita Israeli,

ndivyo walivyokwenda mbali nami.

Walitoa dhabihu kwa Mabaali

na kufukiza uvumba kwa vinyago.

11:3 Kum 1:31; 32:11; Kut 15:26; Yer 30:17Mimi ndiye niliyemfundisha Efraimu kutembea,

nikiwashika mikono;

lakini hawakutambua

kuwa ni mimi niliyewaponya.

11:4 Yer 31:2-3, 20; Law 26:13; Kut 16:32; Za 78:25Niliwaongoza kwa kamba za huruma ya kibinadamu,

kwa vifungo vya upendo;

niliondoa nira shingoni mwao

nami nikainama kuwalisha.

11:5 Yer 8:4-6; Hos 7:16; 10:6; Kut 13:17“Je, hawatarudi Misri,

nayo Ashuru haitawatawala

kwa sababu wamekataa kutubu?

11:6 Hos 13:16; Mao 2:9Panga zitametameta katika miji yao,

zitaharibu makomeo ya malango yao

na kukomesha mipango yao.

11:7 Yer 3:6-7; 8:5; Isa 26:10Watu wangu wamedhamiria kuniacha.

Hata kama wakimwita Yeye Aliye Juu Sana,

kwa vyovyote hatawainua.

11:8 Mwa 14:8; 19:25; Hos 6:4; Mao 3:32; Yer 7:29; Za 25:6; 1Fal 3:26“Efraimu, ninawezaje kukuacha?

Ee Israeli, ninawezaje kukutoa?

Nitawezaje kukutendea kama Adma?

Nitawezaje kukufanya kama Seboimu?

Moyo wangu umegeuka ndani yangu,

huruma zangu zote zimeamshwa.

11:9 Kum 13:17Sitatimiza hasira yangu kali,

wala sitageuka na kumharibu Efraimu.

Kwa kuwa mimi ndimi Mungu,

wala si mwanadamu,

Aliye Mtakatifu miongoni mwenu.

Sitakuja kwa ghadhabu.

11:10 Hos 3:5; 6:1-3; Isa 31:4; 42:13; Za 18:45Watamfuata Bwana;

atanguruma kama simba.

Wakati angurumapo,

watoto wake watakuja wakitetemeka

kutoka magharibi.

11:11 Isa 11:11; Mwa 8:8; Eze 28:26; 34:25-28Watakuja wakitetemeka

kama ndege wakitoka Misri,

kama hua wakitoka Ashuru.

Nitawakalisha katika nyumba zao,”

asema Bwana.

Dhambi Ya Israeli

11:12 Hos 4:2; 10:13; Kum 7:9Efraimu amenizunguka kwa uongo,

nyumba ya Israeli kwa udanganyifu.

Naye Yuda ni mkaidi dhidi ya Mungu,

hata kinyume cha yule mwaminifu Aliye Mtakatifu.

Read More of Hosea 11

Hosea 12:1-14

12:1 Mwa 41:6; Eze 17:10; 2Fal 17:4; Za 78:67; Hos 4:19; 5:13Efraimu anajilisha upepo;

hufukuzia upepo wa mashariki kutwa nzima

na kuzidisha uongo na jeuri.

Anafanya mkataba na Ashuru

na kutuma mafuta ya zeituni Misri.

12:2 Ay 10:212:2 Mik 6:2; Hos 4:9; 9:15; Kut 32:34; Amo 2:4Bwana analo shtaka dhidi ya Yuda,

atamwadhibu Yakobo kwa kadiri ya njia zake

na kumlipa kwa kadiri ya matendo yake.

12:3 Mwa 25:26; 32:24-29Yakobo akiwa tumboni alishika kisigino cha kaka yake;

kama mwanadamu, alishindana na Mungu.

12:4 Mwa 12:8; 28:12-15; 35:15Alishindana na malaika na kumshinda;

alilia na kuomba upendeleo wake.

Alimkuta huko Betheli

na kuzungumza naye huko:

12:5 Kut 3:15Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote,

Bwana ndilo jina lake!

12:6 Mik 6:8; 7:7; Za 106:13; Eze 18:30; Isa 19:22; Yoe 2:12; Yer 22:3Lakini ni lazima urudi kwa Mungu wako;

dumisha upendo na haki,

nawe umngojee Mungu wako siku zote.

12:7 Law 19:26; Amo 8:5Mfanyabiashara hutumia vipimo vya udanganyifu;

hupenda kupunja.

12:8 Za 62:10; Ufu 3:17; Eze 28:5Efraimu hujisifu akisema,

“Mimi ni tajiri sana; nimetajirika.

Pamoja na utajiri wangu wote hawatakuta ndani yangu

uovu wowote au dhambi.”

12:9 Law 23:43; Hos 2:15; Neh 8:17“Mimi ndimi Bwana Mungu wenu

niliyewaleta kutoka Misri;

nitawafanya mkae tena kwenye mahema,

kama vile katika siku

za sikukuu zenu zilizoamriwa.

12:10 Amu 14:12; Eze 20:49; 2Fal 17:13; Yer 7:25Niliongea na manabii, nikawapa maono mengi

na kusema mifano kupitia wao.”

12:11 Amo 4:4; Hos 4:15; 6:8; 8:11Je, Gileadi si mwovu?

Watu wake hawafai kitu!

Je, hawatoi dhabihu za mafahali huko Gilgali?

Madhabahu zao zitakuwa

kama malundo ya mawe

katika shamba lililolimwa.

12:12 Mwa 28:5; 29:18Yakobo alikimbilia katika nchi ya Aramu;

Israeli alitumika ili apate mke,

ili aweze kulipa kwa ajili yake alichunga kondoo.

12:13 Kut 14:19-22; Isa 63:11-14; Kut 13:3; Hos 11:1Bwana alimtumia nabii

kumpandisha Israeli kutoka Misri,

kwa njia ya nabii alimtunza.

12:14 Eze 18:13; Dan 11:18Lakini Efraimu amemchochea sana hasira;

Bwana wake ataleta juu yake

hatia yake ya kumwaga damu naye atamlipiza

kwa ajili ya dharau yake.

Read More of Hosea 12

Hosea 13:1-16

Hasira Ya Bwana Dhidi Ya Israeli

13:1 Mit 18:12; Amu 8:1; 12:1; Hos 11:2Wakati Efraimu alipozungumza, watu walitetemeka,

alikuwa ametukuzwa katika Israeli.

Lakini alikuwa na hatia ya kumwabudu Baali

naye akafa.

13:2 Isa 46:6; Yer 10:4; 44:8; Isa 44:17-20; Hos 8:4; 1Fal 19:18Sasa wanatenda dhambi zaidi na zaidi;

wanajitengenezea sanamu

kutokana na fedha yao,

vinyago vilivyotengenezwa kwa uhodari,

vyote kazi ya fundi stadi.

Inasemekana kuhusu hawa watu,

“Hutoa dhabihu za binadamu

na kubusu sanamu za ndama.”

13:3 Hos 6:4; Ay 13:25; Dan 2:35; Za 68:213:3 Isa 17:13Kwa hiyo watakuwa kama ukungu wa asubuhi,

kama umande wa alfajiri utowekao,

kama makapi yapeperushwayo

kutoka sakafu ya kupuria nafaka,

kama moshi utorokao kupitia dirishani.

13:4 Yer 2:6; Isa 43:10; 45:21-22; Hos 2:20; 12:9; Kut 20:3; Za 18:46“Bali mimi ndimi Bwana Mungu wenu,

niliyewaleta ninyi toka Misri.

Msimkubali Mungu mwingine ila mimi,

hakuna Mwokozi isipokuwa mimi.

13:5 Kum 1:19; 2:7; 32:10; 8:15; 32:10Niliwatunza huko jangwani,

katika nchi yenye joto liunguzalo.

13:6 Mit 30:7-9; Yer 7:5; Eze 28:5; Kum 32:18; Isa 17:10; Hos 2:13; 4:7Nilipowalisha, walishiba,

waliposhiba, wakajivuna,

kisha wakanisahau mimi.

13:7 Ay 10:16; Yer 4:7; Mao 3:10Kwa hiyo nitakuja juu yao kama simba,

kama chui nitawavizia kando ya njia.

13:8 2Sam 17:8; Za 17:12; 50:22; Mao 3:10; Hos 2:12Kama dubu aliyenyangʼanywa watoto wake,

nitawashambulia na kurarua vifua vyenu.

Kama simba nitawala;

mnyama pori atawararua vipande vipande.

13:9 Yer 2:17-19; Kum 33:29“Ee Israeli, umeangamizwa,

kwa sababu wewe u kinyume nami,

kinyume na msaidizi wako.

13:10 2Fal 17:4; 1Sam 8:6; Hos 7:7; 8:4Yuko wapi mfalme wako,

ili apate kukuokoa?

Wako wapi watawala wako katika miji yako yote

ambao ulisema kuwahusu,

‘Nipe mfalme na wakuu’?

13:11 Yos 24:20; 1Sam 13:14; Hes 11:20; 1Fal 14:10; Hos 10:7Hivyo katika hasira yangu nilikupa mfalme

na katika ghadhabu yangu nilimwondoa.

13:12 Kum 32:34; Ay 14:7Kosa la Efraimu limehifadhiwa,

dhambi zake zimewekwa katika kumbukumbu.

13:13 Isa 13:8; Mik 4:9-10; Isa 66:9; 2Fal 19:3Utungu kama wa mwanamke anayejifungua mtoto humjia,

lakini yeye ni mtoto asiyekuwa na hekima;

wakati utakapowadia hatatoka

katika tumbo la mama yake.

13:14 1The 4:14-17; Za 16:10; 49:15; Eze 37:12-13; 1Kor 15:54-55; Ufu 21:4“Nitawakomboa watu hawa kutoka nguvu za kaburi,

nitawakomboa kutoka mautini.

Yako wapi, ee mauti, mateso yako?

Uko wapi, ee kuzimu, uharibifu wako?

“Sitakuwa na huruma,

13:15 Ay 1:19; Eze 19:12; Yer 20:5; 51:36; Hos 4:19hata ingawa Efraimu atastawi

miongoni mwa ndugu zake.

Upepo wa mashariki kutoka kwa Bwana utakuja,

ukivuma kutoka jangwani,

chemchemi yake haitatoa maji

na kisima chake kitakauka.

Ghala lake litatekwa

hazina zake zote.

13:16 2Fal 8:12; 15:16; 17:5; Hos 7:14; 10:2, 14; Isa 13:16; Amo 1:13Watu wa Samaria ni lazima wabebe hatia yao,

kwa sababu wameasi dhidi ya Mungu wao.

Wataanguka kwa upanga;

watoto wao wadogo watatupwa kwa nguvu ardhini,

wanawake wao walio na mimba watatumbuliwa.”

Read More of Hosea 13

Hosea 14:1-9

Toba Iletayo Baraka

14:1 Hos 5:5; 9:7; 12:6; Yer 3:12; Isa 19:22Rudi, ee Israeli, kwa Bwana Mungu wako.

Dhambi zako zimekuwa

ndilo anguko lako!

14:2 Rum 8:26; Za 51:16-17; Mik 7:18-19; Ebr 13:15; Kut 34:9Chukueni maneno pamoja nanyi,

mkamrudie Bwana.

Mwambieni:

“Samehe dhambi zetu zote

na utupokee kwa neema,

ili tuweze kutoa matunda yetu

kama sadaka za mafahali.

14:3 Mik 5:10; Isa 31:1; Hos 5:13; 8:6; Yer 49:11; Za 10:14; 33:17Ashuru hawezi kutuokoa,

hatutapanda farasi wa vita.

Kamwe hatutasema tena ‘Miungu yetu’

kwa kile ambacho mikono yetu wenyewe imetengeneza,

kwa kuwa kwako wewe yatima hupata huruma.”

14:4 Isa 30:26; 55:1; Hos 6:1; Yer 2:19; 31:20; Sef 3:17; Ay 13:16“Nitaponya ukaidi wao

na kuwapenda kwa hiari yangu,

kwa kuwa hasira yangu imeondoka kwao.

14:5 Wim 2:1; Isa 18:4; 35:2; Ay 29:19; Mwa 27:28Nitakuwa kama umande kwa Israeli;

atachanua kama yungiyungi.

Kama mwerezi wa Lebanoni

atashusha mizizi yake chini;

14:6 Za 52:8; 92:12; Yer 11:16; Wim 4:11matawi yake yatatanda.

Fahari yake itakuwa kama mti wa mzeituni,

harufu yake nzuri kama mwerezi wa Lebanoni.

14:7 Za 91:1-4; Hos 2:22; Eze 17:23; Mwa 40:10Watu wataishi tena kwenye kivuli chake.

Atastawi kama nafaka.

Atachanua kama mzabibu,

nao umaarufu wake utakuwa

kama divai itokayo Lebanoni.

14:8 Yer 31:18; Yak 1:17; Isa 37:24Ee Efraimu, nina shughuli gani tena na sanamu?

Nitamjibu na kumtunza.

Mimi ni kama msunobari wenye majani mabichi;

kuzaa kwako matunda kunatoka kwangu.”

14:9 Za 107:43; Mit 10:29; Dan 12:10; Sef 3:5; Mdo 13:10; Isa 1:28; 26:7Ni nani mwenye hekima? Atayatambua mambo haya.

Ni nani mwenye ufahamu? Huyu atayaelewa.

Njia za Bwana ni adili;

wenye haki huenda katika njia hizo,

lakini waasi watajikwaa ndani yake.

Read More of Hosea 14