Waebrania 9:16-28 NEN

Waebrania 9:16-28

Kwa habari ya wosia,9:16 Wosia hapa kwa neno la Kiyunani ni agano. ni muhimu kuthibitisha kifo cha yule aliyeutoa, 9:17 Gal 3:15kwa sababu wosia huwa na nguvu tu wakati mtu ameshakufa; kamwe hauwezi kutumika wakati yule aliyeuandika bado yuko hai. 9:18 Kut 24:6-8Hii ndiyo sababu hata lile agano la kwanza halikuweza kutekelezwa pasipo damu. 9:19 Kut 24:5, 6, 8; Law 16:14, 15, 18; 14:4, 6, 7, 49, 51, 52Mose alipotangaza kila amri kwa watu wote, alichukua damu ya ndama na ya mbuzi, pamoja na maji, sufu nyekundu na matawi ya mti wa hisopo, akanyunyizia kile kitabu na watu wote. 9:20 Kut 24:8; Mt 26; 28Alisema, “Hii ndiyo damu ya agano, ambalo Mungu amewaamuru kulitii.” 9:21 Kut 29:12, 36; Law 8:15, 19; 16:1, 15, 16, 18, 19Vivyo hivyo alinyunyizia damu hiyo kwenye ile hema pamoja na kila kifaa kilichotumika ndani yake kwa taratibu za ibada. 9:22 Law 17:11; Kut 29:21; Law 8:15Kwa kweli sheria hudai kwamba, karibu kila kitu kitakaswe kwa damu, wala pasipo kumwaga damu, hakuna msamaha wa dhambi.

9:23 Ebr 8:5Kwa hiyo, ilikuwa muhimu kwa nakala za vitu vile vya mbinguni vitakaswe kwa dhabihu hizi, lakini vitu halisi vya mbinguni vilihitaji dhabihu bora kuliko hizi. 9:24 Ebr 6:20; 8:2; Rum 8:34; Ebr 7:25; 1Yn 2:1Kwa maana Kristo hakuingia kwenye patakatifu palipofanywa kwa mikono ya mwanadamu, ambao ni mfano wa kile kilicho halisi. Yeye aliingia mbinguni penyewe, ili sasa aonekane mbele za Mungu kwa ajili yetu. 9:25 Ebr 9:7; 10:19Wala hakuingia mbinguni ili apate kujitoa mwenyewe mara kwa mara, kama vile kuhani mkuu aingiavyo Patakatifu pa Patakatifu kila mwaka kwa damu ambayo si yake mwenyewe. 9:26 Ebr 9:12; 7:27; 10:10; 1Pet 3:18; 1Kor 10:11; Gal 4:4; Efe 1:10Ingekuwa hivyo, ingempasa Kristo kuteswa mara nyingi tangu kuumbwa kwa ulimwengu. Lakini sasa ametokea mara moja tu katika mwisho wa nyakati aiondoe dhambi kwa kujitoa mwenyewe kuwa dhabihu. 9:27 Mwa 3:19; Mhu 3:20; 2Kor 5:10; Ufu 20:12, 13Kama vile mwanadamu alivyowekewa kufa mara moja tu na baada ya kufa akabili hukumu, 9:28 Rum 6:10; 1Pet 3:18; 2:24; 1Yn 3:5; Mt 26:28; Rum 5:15; Tit 2:13vivyo hivyo Kristo alitolewa mara moja tu kuwa dhabihu ili azichukue dhambi za watu wengi. Naye atakuja mara ya pili, sio kuchukua dhambi, bali kuwaletea wokovu wale wanaomngoja kwa shauku.

Read More of Waebrania 9