Waebrania 11:17-40 NEN

Waebrania 11:17-40

11:17 Mwa 22:2-10; Yak 2:21Kwa imani Abrahamu, alipojaribiwa na Mungu, alimtoa Isaki kuwa dhabihu. Yeye aliyekuwa amezipokea ahadi za Mungu alikuwa tayari kumtoa mwanawe, aliyekuwa mwanawe pekee awe dhabihu. 11:18 Mwa 21:12; Rum 9:7Ingawa Mungu alikuwa amemwambia Abrahamu, “Uzao wako utahesabiwa kupitia kwa Isaki,” 11:19 Rum 4:21; Yn 5:21Abrahamu alihesabu kuwa Mungu angaliweza kumfufua Isaki kutoka kwa wafu. Na kwa kusema kwa mfano, alimpata tena Isaki kutoka kwa wafu.

11:20 Mwa 27:27-29Kwa imani Isaki alimbariki Yakobo na Esau kuhusu maisha yao ya baadaye.

11:21 Mwa 48:1; 8:22; 47:31Kwa imani Yakobo alipokuwa anakufa, alimbariki kila mmoja wa mtoto wa Yosefu, akamwabudu Mungu akiwa ameegemea juu ya kichwa cha fimbo yake.

11:22 Mwa 50:24, 25; Kut 13:19; Yos 24:32Kwa imani, Yosefu alipokaribia mwisho wa maisha yake, alinena habari za kutoka kwa wana wa Israeli huko Misri na akatoa maagizo kuhusu mifupa yake.

Imani Ya Mose

11:23 Kut 2:2; 1:16, 22; Mdo 7:20Kwa imani, wazazi wa Mose walimficha kwa miezi mitatu baada ya kuzaliwa, kwa sababu waliona kuwa si mtoto wa kawaida, wala hawakuiogopa amri ya mfalme.

11:24 Kut 2:10, 11Kwa imani, Mose alipokuwa mtu mzima, alikataa kuitwa mwana wa binti Farao. 11:25 Ebr 11:37; Za 84:10Akachagua kupata mateso pamoja na watu wa Mungu kuliko kujifurahisha kwa anasa za dhambi kwa kitambo kidogo tu. 11:26 Ebr 13:13; Lk 14:33; Ebr 10:35Aliona kushutumiwa kwa ajili ya Kristo ni utajiri mkubwa zaidi kuliko hazina za Misri, maana alikuwa anatazamia kupata thawabu baadaye. 11:27 Kut 12:50-51; 10:28-29; 12:37; 13:17; Ebr 11:18Kwa imani Mose aliondoka Misri bila kuogopa ghadhabu ya mfalme. Alivumilia kwa sababu alimwona yeye asiyeonekana kwa macho. 11:28 Kut 12:21; 1Kor 10:10Kwa imani akaadhimisha Pasaka na kunyunyiza damu, ili yule mwenye kuwaangamiza wazaliwa wa kwanza asiwaguse wazaliwa wa Israeli.

Imani Ya Mashujaa Wengine Wa Israeli

11:29 Kut 14:21-31; 14:22Kwa imani, watu walivuka Bahari ya Shamu11:29 Yaani Bahari ya Mafunjo. kama vile juu ya nchi kavu; lakini Wamisri walipojaribu kufanya hivyo, walitoswa ndani ya maji.

11:30 Yos 6:20; 6:12-19Kwa imani kuta za Yeriko zilianguka, baada ya watu kuzizunguka kwa siku saba.

11:31 Yos 2:1; 9; 14; 6:22-25; Yak 2:25Kwa imani, Rahabu, yule kahaba, hakuangamizwa pamoja na wale waliomwasi Mungu, kwa kuwa aliwakaribisha wale wapelelezi.

11:32 Amu 6:8; 4:5; 13:16; 1Sam 16:1, 13; 1:20Basi niseme nini zaidi? Sina wakati wa kusema habari za Gideoni, Baraka, Samsoni, Yeftha, Daudi, Samweli na manabii, 11:33 2Sam 8:1-3; Dan 6:22ambao kwa imani walishinda milki za wafalme, walitekeleza haki, na wakapokea ahadi za Mungu; walifunga vinywa vya simba, 11:34 Dan 3:19-27; Kut 18:4; 2Fal 20:7; Amu 15:8wakazima makali ya miali ya moto, na wakaepuka kuuawa kwa upanga; udhaifu wao uligeuka kuwa nguvu; pia walikuwa hodari vitani na kuyafukuza majeshi ya wageni. 11:35 1Fal 17:22, 23; 2Fal 4:36, 37Wanawake walipokea watu wao waliokuwa wamekufa, wakafufuliwa. Lakini wengine waliteswa, nao wakakataa kufunguliwa, ili wapate ufufuo ulio bora zaidi. Wengine walidhihakiwa na kupigwa, hata walifungwa minyororo na kutiwa gerezani. 11:37 2Nya 24:21; 1Fal 19:10; Yer 26:23; 2Fal 1:8Walipigwa kwa mawe; walipasuliwa vipande viwili kwa msumeno; waliuawa kwa upanga. Walizungukazunguka wakiwa wamevaa ngozi za kondoo na mbuzi, wakiwa maskini, wakiteswa na kutendwa mabaya, 11:38 1Fal 18:4; 19:9watu ambao ulimwengu haukustahili kuwa nao. Walizunguka majangwani na milimani, katika mapango na katika mahandaki ardhini.

11:39 Ebr 11:2, 4, 13; 10:36Hawa wote walishuhudiwa vyema kwa sababu ya imani yao, lakini hakuna hata mmoja wao aliyepokea yale yaliyoahidiwa. 11:40 Ufu 6:11; Ebr 2:10Kwa kuwa Mungu alikuwa ametangulia kutuwekea kitu kilicho bora zaidi ili wao wasikamilishwe pasipo sisi.

Read More of Waebrania 11